Athlete Crown sio gari la kubishana nalo ukiwa barabarani acha liende

Moja ya gari ambalo ni noma barabarani basi ni hili ndinga,nakumbuka jana nikiwa natokea maeneo ya RUFIJI kuja DAR ilinipa hii gari kama nimesimama

Nikiwa kwenye mwendo wa speed 100 sehemu yenye mwinuko kidogo huku nikijiona mimi ni bingwa barabarani niliiona gari likija kwa nyuma yangu kwa kasi sana ilikuwa kama mita 130 nyuma yangu basi nikasema haiwezekani nikapitwa kijinga kiasi hicho nikachochea moto nikafikisha speed 125 hivi.....sasa nilichokuja kunishangaza ni namna yule jamaa wa crown alivyokuwa anaomba site apite yaani ilikuwa ni kitendo cha dk 6 ile gari ilinipita na sikuiona tena.

Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuendesha CARINA Ti lakini niliambulia patupu
Hizi crown ni gari za safari ingawa inameza mafuta kama jini ila ni chombo cha maana nami namuomba mungu huku nikijichanga nichukue hii ndinga

Hongereni wote mnaoendesha athletes crown au mnaomiliki hii ndinga hakika hamjakosea
yes kaka hizo gari zinakimbia but still zina wababe road one day natoka mtwara kuja dar nilikua kama na 130 ivi nikamuomba jamaa kagoma nilikuja kumu overtake na 160.....
 
Haitakaa nitembee speed hio tena!! Gari yenyewe nilishaiuza, Sitaki tena nikikimbia Sana mwisho 150km/hr. Nina watoto sasa wakubwa wananitegemea. Sitakiii
Mpwa wacha woga bwana
 
niambieni na hii gari yetu landcruiser prado SKZ ENGINE DIESEL, alafu ni TURBO, niliifungua speed 140 hadi gari inapiga mluzi, na tyre zikitanuka kwenda nje,, nilivipita visubaru na vialtezza, kama napita baiskeli tu. sijui hiyo athlete crown kama ingenikamata kwa kweli.
 
Moja ya gari ambalo ni noma barabarani basi ni hili ndinga,nakumbuka jana nikiwa natokea maeneo ya RUFIJI kuja DAR ilinipa hii gari kama nimesimama

Nikiwa kwenye mwendo wa speed 100 sehemu yenye mwinuko kidogo huku nikijiona mimi ni bingwa barabarani niliiona gari likija kwa nyuma yangu kwa kasi sana ilikuwa kama mita 130 nyuma yangu basi nikasema haiwezekani nikapitwa kijinga kiasi hicho nikachochea moto nikafikisha speed 125 hivi.....sasa nilichokuja kunishangaza ni namna yule jamaa wa crown alivyokuwa anaomba site apite yaani ilikuwa ni kitendo cha dk 6 ile gari ilinipita na sikuiona tena.

Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuendesha CARINA Ti lakini niliambulia patupu
Hizi crown ni gari za safari ingawa inameza mafuta kama jini ila ni chombo cha maana nami namuomba mungu huku nikijichanga nichukue hii ndinga

Hongereni wote mnaoendesha athletes crown au mnaomiliki hii ndinga hakika hamjakosea
carina na crown wapi na wapi. carina mwenzie paso na vits tu. crown na mark x na brevis au aud au benz au bmd apo sawa.

na carina? yerewiiiii
 
Back
Top Bottom