Atheism: Imani nusu na robo

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,880
Reaction score
828,445


kwenye ulimwengu wa vipimo kuna ujazo mbalimbali kama robo nusu na kitu kamili nk.. nusu mbili hutengeneza kitu kamili robo mbili hutengeneza nusu moja

Kuna kamchezo ukimtuma mtu asiye mwaminifu akuletee kitu kinachohusika na vipimo kupiga bao! Ukimtuma kilo moja yeye ataleta nusu na robo.

Duniani tuna imani mbalimbali kuanzia zinazoabudu Mungu mmoja,miungu vitu vinavyoonekana, hata masanamu... kwenye hizi imani kuna mitifuano na mikanganyiko mingi tuu..lakini kiboko ya imani zote ni hii isiyomwamini Mungu mmoja

Jaribu kumuuliza atheist yeyote kwanini huamini katika Mungu atakwambia kwakuwa hajawahi kumuona! Ila muulize kama alishawahi kuiona akili yake au roho yake...hatakupa jibu moja na la moja kwa moja

Hii ni imani isiyotimia isiyojua dhima yake mwanzo wake wala muktadha wa nini inasimamia

Ni imani chongo yenye kengeza barobaro...ikiamini isichokiamini..ikifuata isichokijua

Je atheism ni;
Kuabudu miungu?
Kuabudu shetani?
Kuabudu masanamu?
Kuabudu vitu ?
Ama kutoabudu chochote?

Kila imani ina maelezo fulani kwenye chochote na kila swali lina jibu lake tusiiweke sayansi kwenye kundi la imani..hili ni Somo kama masomo mengine

Kutoamini chochote ni mkanganyiko tu wa akili kwakuwa mwisho wa siku utajikuta unaangukia kwenye imani yoyote japo kwa kificho na imani ya kutoamini chochote ni imani isiyotimia
 
Kama huamini kuwa kuna gravity, panda juu ya mti mrefu halafu ujiachie! You can not see gravity but try to deny its existence by making that experiment.
 

Mkuu Mshana:

Hakuna shida kwa Atheists kutoamini kwamba Mungu yupo.Kumuamini Mungu ni jambo linaloweza kutokea muda wowote,mahali popote na kwa hata tusiyowatarajia.Hapana ubishi kwamba Mungu yupo na "project" yake ya kuhakikisha kila mtu anarudi kwake(kwa kuwa kila mmoja ametoka kwake) sio jambo dogo hata kidogo.Linafanyika ukiwa conscious or subconscious na hata completely unconscious(dead).

Hao Ma-atheist sio ajabu hata muda wa kuondoka kwao duniani hupewa nafasi ya kukiri kwamba huyo ambaye walikuwa hawamkubali ndiye ana-end up sasa life span yao.Unakumbuka jamaa mmoja katika wale waliokuwa wamesulubiwa pamoja na Yesu "alivyoiba" Mbingu dakika za mwisho mwisho? Hii inatufundisha jambo kubwa sana.Hakuna anayejua mtu wakati wa kuondoka duniani huwa anaongea nini na Mungu wake. Kinachoongea na Mungu ni nafsi sio mdomo wala miguu ile inayompeleka mtu kanisani.Mungu ana-deal na nafsi ya mtu zaidi.Ndio maana huwa nawashangaa watu wanaomba kwa makelele wakifikiria ndo "signal" za maombi yao zinamfikia Mungu.Mtu yuko peke yake lakini anapayuka payuka mithili ya Simba nyikani eti yuko kwenye maombi. Mungu "anasikia" hata undetectable/unquantifiable frequencies za maombi yetu.
 
Asante kwa uchambuzi mzuri! Hiki kinachoitwa atheism ni kikundi cha watu wenye imani ya Mungu mmoja waliosoma Misahafu na kutokubaliana nayo kwenye vifungu kadha hasa kwenye vifungu vya kusamehe miujiza visasi kifo na uzima wa milele
Kiuhalisia atheism ni dhana nyepesi isiyo na misingi yoyote bali mtazamo wao mkuu ni kukosoa Biblia takatifu na uwepo wa Mungu mkuu
 
Nakuunga mkono ndugu mshana jr , tatizo kinachowapa jeuri atheist ni baadh ya mikanganyiko iliyopo kwenye vitabu vyetu vya dini… ila kiukwel ulichosema ni sahihi
Hakuna mikanganyiko yoyote..kimacholeta hiyo mikanganyiko ni hizi tafsiri za kibinadamu bila kuongozwa na roho mtakatifu
Ishu za kiroho ni za kiroho na ziko kiimani huwezi kuzitafsiri kwa muktadha wa kibinadamu kwenye akili ya kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…