Athari za kusema Uongo

uvugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,351
Reaction score
1,100
Kusema uongo niligundua kumbe ni kuhatarisha MAISHA , siyo tu kwamba Mungu alikataza katika maandiko yake matakatifu kama Amri tu, HAPANA .

Kusema uongo kuna athari hata kisayansi katika Maisha ya Mwanadamu , na ndiyo 90% ya vifo vya watu , kwa Mujibu wa wataalam wa COGNITIVE DISSONACE.

Shetani ni baba wa uongo , amekuja kupora , kuharibu na haswa tusifikie umilele . ukiona Mungu anasema usiseme uongo , si kwa faida yake tu ni yako mwenyewe na maisha yako.

Mambo mengi Mungu aliyakataza au alisema tusifanye kwa ajili yetu na kutuepusha na litakalo tokea

Kwa Mujibu wa mtaalamu wa uongo ( naweza muita deception expert) Pamela Meyer . mtu huwa anadanganya kila dk 3 za mwanzo za kukutana naye. Yaani ukikutana na mtu dakika chache za mwanzo lazima aseme uongo

Wanajuaje hayo ,. Ukisoma machine ya kupimia uongo kwa wale wanaojua kitu kinaitwa POLYGRAPH TEST , ni machine ambayo wanatumia detectives wa CIA / FBI /Scotlandyard for Forensic investigation , kwa ajili ya kugundua mtu anaongea uongo au ukweli.

Polygraph test ina sensor 4 hadi 6 ambazo zinafungwa kwa mtu , zitaonyesha breathing rate , blood pressure, na perspiration nk . wanapoona mabadiliko ya ghafla katika graph wakati wanakuhoji wanabaini kuwa unasema uongo .ingawa wanasema inafanya kazi 70%.

Kwa Mujibu wa Pamela Meyer na Madaktari bingwa duniani walibaini, kusema uongo kwa kutumia POLYGRAPH TEST , walibaini watu wanaangamia .

Kwani uongo unaleta COGNITIVE DISSONANCE yaani hali ya kutengeneza vita kichwani katika akili yako , kwa kuwa kuna mawazo mawili yanapingana.
Effect kubwa ya COGNITIVE DISSONANCE ni STRESS ( msongo wa mawazo ) , ambao unaleta blood pressure, magonjwa yote ya moyo , cancer , obesity na insomnia.

Nikiangalia maandiko ndiyo maana yesu alisema amani yangu nawaachieni Yohana 14:27 na Mungu akasema usidanganye,,,,walawi 19:11

Kwa lugha nyingine kusema uongo =mshirika wa shetani= magonjwa na kukosa amani= dhambi .

Mambo mengi tunasingizia shetani/Mungu/mazingira nk, kumbe ni sisi wenyewe

Wasema uongo wengi hawana amani chunguza na ndiyo maana ukikubali kuokoka cha kwanza unarejeshewa amani , ili biashara ingine na Mungu ianze .

Be inspired and respired
 
Naunga mkono kwa 100%,tuanzie na adultery inavyowamaliza wahusika..
 
Kumekuwepo mkanganyiko kuhusu matumizi ya polygraph test kwakuwa wengine wanadai siyo effective kutambua kweli kama mtu anasema ukweli au uongo na ni zaidi ya mara nyingi unakuja kugundua kuwa waliyedhania mkosaji kumbe siye na ndiyo maana ushahidi wa polygraph test lazima uambatane na supporting evidence.
Kuhusu uongo ni kweli kabisa uongo ni kitu kibaya na mimi nime experience hilo.
Kuna uongo nilimdanganya mtu, ulianza kama uongo mdogo tu ila kila siku ukazidi kukua na kuongezeka ili kulinda uongo niliyomwambia awali.
Kuja kushtuka nimetengeneza uongo mkubwa kiasi kwanba ninashindwa kumwambia ukweli kwa wakati huo.
Ikaanza kunitafuna ndani kwa ndani, ikawa inankosesha raha na kunikondesha.
Lakini ulikuwa ushakuwa uongo mkubwa kiasi kwamba najiuliza nitaanzaje kumwambia mhusika, ilinitesa kwa mwaka mwisho alikuja kujua ukweli sasa effect yake ni hii
Urafiki wetu tuliotengeneza kwa miaka mingi uliisha.
Uaminifu wangu kwake ni 0
Hatuongei
Pia nalo linanitesa kwakuwa he was more than a friend to me.
Inaniathiri kisaikolojia wish I could turn back the hands of time.

Lakini kwa namna moja ama nyingine alipojua ukweli kuna mzigo niliutua niliokuwa nimeubeba kuna relief niliipata.

Jamani uongo ni kitu kibaya sana, uanza kama uongo mdogo tu lakini unaweza kukua na kuwa kitu kikubwa na tena cha hatari.
Experience is the best teacher
 
hiyo poligraph test yenyewe siku hizi inadanganywa sana tu.
ila Uongo haufai...
 
Uongo ni kitu kibaya sana katika nyanja zote za maisha iwe katika mahusiano,Siasa,Kazini hata katika story za kawaida tu.Uongo unaleta sifa mbaya sana kwa mtu na unaweza ukadharaulika na kutokuaminika kabisa mbele za watu.Kuna uongo nilishawahi kuutengeneza hadi leo hii najuta.Ila uongo ni kitu kibaya sana ambacho kitakufanya ukose amani maisha yako yote.
 
Daah ile sasa hivi bhana uongo umeshamiri sio mtoto, kijana wala mzee.

Kuna mshikaji juzi kanishangaza sana, yaan namuona kabisa anaingia home kwake ilikua saa 4 asubuhi, saa 6 mchana ananicall eti "daah mwanangu tangu saa 3 tupo kwenye gari barabara mbovu kishenzi ndio sasa hivi naingia magetoni..." simdai wala sina ahadi nae sasa kwann anidanganye??? nikasema kweli zama za mwisho.
 
Karibuni wana wa Adam watamjua Mungu, kwa kweli wanamtafuta na kuzijua Kweli zake, maarifa yao yanaongezeka. Tuzidi kujifikirisha ktk kuzijua hizi KWELI tuwe huru kwa kujua tunachokiamini.

Pia, tutafakari ktk "baraka" za Mungu, neema na mengineyo mengi sana. Yote yana majibu mubashara. Hatutadanganywa na hawa wafia njaa eti watuombee tubarikiwe nknk.
 

barikiwa kwa kutia nyama ndani ya uzi huu, waefeso 4: 17 " msienende kama mataifa waenendavyo katika ubatili wa nia zao"
 
hiyo poligraph test yenyewe siku hizi inadanganywa sana tu.
ila Uongo haufai...

na ndiyo maana, polygraph procedure is called the Guilty Knowledge Test (GKT). kuna mabo mengi hapo yanahusishwa in order to confirm
 
When does telling the truth ever do you any good
 
Sema ukweli hata kama panga liko shingoni.(napenda kauli hii)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…