Athari za kiafya za vyakula vyenye wanga


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,975
Likes
5,344
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,975 5,344 280
athari-za-kiafya-za-vyakula-vyenye-wanga-jpg.361315


Imeandikwa na Dk. Boaz Mkumbo

MOJA ya vyakula ambavyo tumekuwa tukitumia kwa wingi hasa Watanzania wenye kipato cha kati na chini kabisa ni vyakula vya aina kuu tatu, Wanga, Protini na Mafuta (Fats).


Na kwa kiwango kidogo sana tunatumia vitamin na madini katika milo yetu. Moja ya masomo ya chakula tunayofundishwa ni kula mlo kamili.Watu wengi tumekuwa tukitumia elimu hiyo hadi hapa tulipofika.

Napenda kusema tu kwamba mlo kamili ni kwa ajili ya mtu mzima ambaye hana ugonjwa wowote na ni kwa yule tu ambaye hataki kula kiafya.

Napenda kusema haya kwa sababu tumekuwa tukila vyakula vya namna ile ile lakini tumekuwa tukiugua mno magonjwa mbalimbali yatokanayo na lishe mbovu. Hadi sasa ugonjwa wa kisukari hapa duniani unaua zaidi ya ugonjwa wa UKIMWI, swali la kujiuliza je, tumejitenga wapi mbali katika lishe?

Leo nataka nikueleze kidogo kuhusu sayansi ya chakula aina ya wanga. Maana kila mtu ninayemwelekeza njia sahihi ya kupunguza uzito anakwambia nitaishije bila chakula cha wanga? Mwili wako hutumia vyakula vikuu aina tatu ambavyo ni wanga, protini na mafuta.

Na unatakiwa ujue kuwa gramu moja ya wanga hutengeneza nishati ya mwili kalori nne, ambapo protini nayo hutengeneza kalori nne na Fats hutengeneza kalori tisa. Unaona ni zaidi ya mara mbili ya nishati zinazotengenezwa na chakula cha wanga.

Hii ina maana kuwa ninaposema kuwa tunaweza kupunguza wanga na ukaishi ukiwa na nguvu nyingi zaidi hata ya ulivyo kuwa katika lishe ya wanga nyingi.

KWA NINI NAKUSHAURI UPUNGUZE WANGA KIAFYA?
Unapokuwa umepunguza wanga au kuacha kabisa ulaji wa vyakula vyenye wanga nyingi, mfano mikate, ugali, wali na tambi. Hakikisha kitendo hicho kiendane na kuongeza kiwango cha mafuta na vyakula vya protini mwilini mwako katika lishe yako. Hii itaufanya mwili wako kuanza kutumia mafuta kama nishati ya mwili ya kwanza kujitengenezea nguvu.

Viungo vya binadamu kama ini na figo vinapokuwa vinatumia mafuta kuzalisha nishati ya mwili hutengeneza viini vya nishati viitwavyo Ketone Bodies, ambavyo hivi ndivyo hutumiwa na seli za mwili kujitengenezea nishati kwa wingi.

Hivyo basi, unapokuwa unajizuia kutumia vyakula vya wanga mwili wako utatumia karibia siku tano hadi wiki kuanza kutumia mafuta kama nishati ya mwili na hicho kitendo tunaita Keto Adaption.

Ningependa kusema kwamba Keto Adaption ni ile hali ya mwili wako kujenga mazoea ya kutumia mafuta kama chanzo cha nishati ya mwili na hapo ndipo utaanza kuona mabadiliko katika mwili wako makubwa.

Utakuwa unajisikia mwenye nguvu na unatashangaaa dalili mbalimbali zilizokuwa zinakusumbua zinapotea hii ni kwa sababu ya uwezo mkubwa wa ketone bodies katika mwili wako dhidi ya glucose.

Sote tunajua kwamba ulaji wa vyakula vya wanga kwa wingi na vyakula vyenye sukari nyingi vinaongeza kiwango cha sukari kwenye damu zaidi ya kiwango ambacho mwili wako unaweza kuhimili.

Mfano; kiwango cha kawaida cha sukari kinachohitajika mwilini mwako ni kijiko kimoja cha chai, hiki ni kiwango ambacho hakiwezi kukuletea matatizo. Basi kama binadamu anaishi kwa sukari inayokadiriwa kuwapo kwenye damu kama kijiko kimoja tu cha chai.

Unywaji wa soda moja unaweza kuongeza zaidi ya vijiko 10, hivyo basi mwili wako unakuwa unashindwa kuhimili sukari iliyozidi.

Kwa wale wanaopenda kula baga, inakadiliwa kuwa baga moja ya kati inaweza kutoa sukari zaidi ya vijiko 16 kwenye damu.

Swali la kujiuliza mwili unapeleka wapi sukari iliyozidi wakati miili yetu inahitaji sukari kiwango kidogo kama kijiko kimoja tu kuishi?
Mwili hutengeneza maji kutoka kwenye seli za kongosho ziitwazo beta seli, maji haya ni homon iitwayo Insulin, kazi kubwa ya insulin ni kutunza glucose hii katika damu kwa matumizi ya baadae, na inatunza katika kiasi maalumu katika mfumo wa Glycogen na kiasi kikubwa katika mafuta.

Hivyo basi, mafuta haya huhifadhiwa katika sehemu mbalimbali kama tumboni, shingoni, mikononi, kifuani na kiunoni. Mafuta haya huhifadhiwa katika mfumo wa Tryglycerides ambayo haya ni miongoni ya mafuta mabaya mwilini mwako.

Sasa mtu anayekwambia wanga nyingi katika chakula chako ni salama anakudanganya kwa kiasi kikubwa kwani tunaona jinsi gani ulaji wa kiwango kingi cha vyakula vya wanga na sukari vinavyosababisha sukari kupanda kupita kiasi na insulin kuanza kuhifadhi katika mafuta.

Kila siku nasema, tumekaririshwa adui mkuu ni fats na kujisahau ulaji mbovu wa vyakula vya wanga huku tukiishia kulea vitambi na magonjwa sugu, hii yote ni kutokuwa na ufuatiliaji wa lishe nzuri na salama kwako.

MADHARA MENGINE YA SUKARI
Napenda kuwarudisha nyuma kidogo katika somo la bailojia. Tulijifunza kuwa miili yetu imejengwa kwa kiini kidogo sana kiitwacho seli ambapo shughuli zote za mwili zinafanyika humo.

Nilijifunza kuwa ndani ya seli kuna viungo vidogo vidogo navifananisha na (Apartments kwenye nyumba kubwa) moja wapo ni Mitochondria, hiki ni kiungo kidogo katika seli ambacho kinahusika na kuzalisha nishati ya mwili tu. Pia nikikumbuka watu wote tulijifunza kwamba mwili wetu hujitenegenezea nishati ya mwili au nguvu kupitia kuifanyia kazi sukari iliyo ndani ya damu baada ya kuingia ndani ya seli.

Hivyo basi insulin ni kama ufunguo ambao unafungua milango ili sukari iweze kuingia ndani ya seli hadi kwenye mitochondria. Mwili wako unapokuwa unatumia hewa ya oxygen kuna uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa athari iitwayo Oxdative stress.

Hii ndiyo inayofanya chuma kipate kutu, hii ndiyo inayofanya mafuta ukiyaweka kwenye jua kwa muda mrefu yanaharibika. Basi mwili wako unakuwa unatengeneza vihatarishi viitwavyo Reactive Oxygen Species kwa kifupi huitwa Free Radicals.

Hizi ni sumu ambazo hupatikana wakati mwili unajitenegenezea nishati yake kwa kutumia oxygen na hizi zinapokuwa kiwango kikubwa huweza kuharibu kabisa seli na kuziua na pia zinaweza kupelekea kupata magonjwa sugu kama saratani.

Hivyo, tafiti zinaonesha kwamba vyakula vya wanga na sukari vina matokeo makubwa ya kutenegeneza Free Radicals nyingi kupita kiasi.

Miili yetu ina kiwango fulani cha viondoa sumu ambavyo vinaipunguza sumu ya free radicals kuepusha kusababisha magonjwa kwa kuziua seli.

Lakini panapokuwa na kiwango kikubwa cha uzalishaji wa free radicals mwili unashindwa kuhimili na hatimaye free radicals zinaanza kuleta madhara mwilini mwako. Kadri mitochondria zinavyodhoofika ndivyo magonjwa nyemelezi ya lishe yanavyotukabili kila kukicha.
chanzo.ATHARI ZA KIAFYA ZA VYAKULA VYENYE WANGA ~ Jiko Langu
 
Mr Q

Mr Q

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Messages
7,502
Likes
9,732
Points
280
Mr Q

Mr Q

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2012
7,502 9,732 280
yees huyo ndio mziziMkavu tuliye mzoea karibu tena mkuu
 
Life.co.tz

Life.co.tz

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2012
Messages
630
Likes
286
Points
80
Life.co.tz

Life.co.tz

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2012
630 286 80
Yap Somo zuri sana Hili.
Sasa Naomba utupe walau mfano wa Tuleje sasa ili kuepukana na Madhara hayo.
Mimi mwanachi wa Kawaida ninaezungukwa na vyakula vya wanga. soda na juisi kibao nk.
 
kalagabaho

kalagabaho

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
4,724
Likes
2,745
Points
280
kalagabaho

kalagabaho

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
4,724 2,745 280
Yap Somo zuri sana Hili.
Sasa Naomba utupe walau mfano wa Tuleje sasa ili kuepukana na Madhara hayo.
Mimi mwanachi wa Kawaida ninaezungukwa na vyakula vya wanga. soda na juisi kibao nk.
Umezunguukwa na soda na sio maji wala madafu??
 
dre4691

dre4691

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2016
Messages
486
Likes
306
Points
80
Age
28
dre4691

dre4691

JF-Expert Member
Joined Feb 22, 2016
486 306 80
Yap Somo zuri sana Hili.
Sasa Naomba utupe walau mfano wa Tuleje sasa ili kuepukana na Madhara hayo.
Mimi mwanachi wa Kawaida ninaezungukwa na vyakula vya wanga. soda na juisi kibao nk.
Kunywa subir matokeo yake
 
Mtoto halali na hela

Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2012
Messages
22,110
Likes
5,331
Points
280
Mtoto halali na hela

Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2012
22,110 5,331 280
Mzizi mkavu tuleje maana mabachelor wengi ni Ugali tambi na wali
 
Bejajunior

Bejajunior

Senior Member
Joined
Sep 19, 2011
Messages
194
Likes
7
Points
35
Bejajunior

Bejajunior

Senior Member
Joined Sep 19, 2011
194 7 35
Ni vyema ukaweka mfano wa mpangilio wa hivyo vyakula bora toka asubuhi hadi usiku badala ya kukosoa tu hivyo vyakula vyenye wanga kwani wengine tumezoea asubuhi chai chapati,maandazi au vitumbua mchana sembe jioni wali.
Vyema sana.. ulichotaja ni kama mlo mtukuka kwa Tanzania yetu.
 
ChaterMaster

ChaterMaster

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2009
Messages
1,433
Likes
475
Points
180
ChaterMaster

ChaterMaster

JF-Expert Member
Joined Aug 17, 2009
1,433 475 180
Mzizi Mkavu tafadhali nijibu hili..
Hvyo vyakula vya mafuta ni vip.. Maana upande mwingne tunaambiwa mafuta hasa ya wanyama ni hatari kwa miili yetu.. Yanaleta colestro kwa kasi
 
TZ ME

TZ ME

Member
Joined
Dec 22, 2014
Messages
78
Likes
56
Points
25
TZ ME

TZ ME

Member
Joined Dec 22, 2014
78 56 25
Ndg mzizi mkavu, somo lako nimelipenda leta suluhu sasa.. Vyakula mbadala ya wanga ni vipi??
 
divisiblebyzero

divisiblebyzero

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2015
Messages
668
Likes
254
Points
80
divisiblebyzero

divisiblebyzero

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2015
668 254 80
Ukifuata mashart sana ya wataalamu wa afya utajikuta mtu wa mawazo na hofu kubwa. Cha msingi nikumwomba Mungu tu amna option. Mtoa mada katoa list ya vyakula vya kuepuka ila hajatoa option watu wale nini. Huu si ushauri ila nikuleteana hofu ya maisha.
 
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Messages
11,497
Likes
24,044
Points
280
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2016
11,497 24,044 280
Mzizi Mkavu mpaka Leo hajaleta majibu ya nn kifanyike(mbadala wa vyakula vya wanga)...tuendelee kusubiri!??
 
kisu cha ngariba

kisu cha ngariba

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Messages
22,195
Likes
47,977
Points
280
kisu cha ngariba

kisu cha ngariba

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2016
22,195 47,977 280
Mzizi Mkavu mpaka Leo hajaleta majibu ya nn kifanyike(mbadala wa vyakula vya wanga)...tuendelee kusubiri!??
Kula vyakula vyenye protein.
 
S

sawabho

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2011
Messages
5,107
Likes
1,654
Points
280
S

sawabho

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2011
5,107 1,654 280
Acheni kutia watu hofu, tangu mwaka 1961 tunakaula hivyo vyakaula; mbona bado tunaishi ??.
 
Prince Mhando

Prince Mhando

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Messages
4,885
Likes
3,999
Points
280
Prince Mhando

Prince Mhando

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2014
4,885 3,999 280
Mada inamyumbisha msomaji...mbona haujavitaja hivyo vyakula vya wanga...¿
 

Forum statistics

Threads 1,235,506
Members 474,615
Posts 29,225,101