ATCL haitapewa fedha nyingine

Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,358
4,304
NAIBU Waziri wa Uchukuzi, Dk. Athman Mfutakamba amesema kuwa serikali haina mpango wa kutoa fedha nyingine kwa ajili ya kuifufua Kampuni ya Ndege (ATCL).
Akiongea katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV, Mfutakamba alisema kwa sasa serikali inajitaidi kutafuta wawekezaji wa ndani na nje ili kuhakikisha wanairudisha kampuni hiyo katika hadhi yake.
Alisema serikali ilishatoa fedha nyingi kwa ATCL ambapo wameitaka kampuni hiyo katika kipindi hiki kuhakikisha wanafunga mkanda ili waweze kujiendesha kibiashara.
Dk. Mfutakamba alisema serikali inawakaribisha wawekezaji walio na uwezo kwa ajili ya kuingia ubia na ATCL, hatua itakayosaidia watu wengi kuweza kutumia usafiri huo.
Alisema mbali na hilo serikali inafanya jitihada kwa ajili ya kuboresha viwanja vya ndege pamoja na kuhamasisha watu wengine kuanzisha mashirika yao ya ndege kutokana na usafiri wa anga kuwa wa gharama kubwa. “Katika hili la ATCL serikali imeshatoa fedha nyingi na matatizo hayajaisha na bado yanajadiliwa kuona jinsi ya kuyamaliza lakini tunawataka ATCL wao nao wafunge mikanda wajiendeshe kibiashara,” alisema.
Dk. Mfutakamba: ATCL haitapewa fedha nyingine

Kuna siku, member alileta thread ya tetesi kuwa Rostam amekamatwa Malaysia..lakini aliporudi katika kuwajibu wanahabari alisema alikwenda huko kutafuta wawekezaji katika usafiri wa anga.....sasa connect the dots...

Ua Tanesco ,kampuni binafsi zizalishe umeme wa dharura..

Ua shirika la ndege ili uimarishe sekta ya utalii nchini kwa kutegemea mashirika ya ndege ya nchi nyengine au makampuni binafsi...

Agiza matrekata kwa kilimo kwanza ila sahau innovation centers za ndani katika kuzalisha vifaa vya kilimo.

Orodha ni ndefu.....
 
Back
Top Bottom