Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,289
- 2,472
Wasalaam wote humu. Bila kupoteza muda moja kwa moja kwenye simulizi.
Ilikiwa ni mwishoni mwa miaka ya 1990, sekondari moja hukoo... Nikiwa A level boarding. Sasa akawepo dada mmoja binti mrembo aliyekuwa O level. Hata sasa ni mrembo bila ya shaka. Tena alikiwa dada mkuu msaidizi. Nikawa nampenda moyoni na nikawa najiambia siku moja nitamtolea dukuduku langu. Kiukweli kilichokuwa kinanichelewesha kutoa dukuduku ni woga wangu, hasa ukichanganya na uzuri wake. Ikawa kila nikimwona moyo wangu hupiga pah !
Siku moja asubuhi nikasema lazima nimweleze. Mara wakati wa harakati za asubuhi wakati wa usafi na pilika za hapa na pale mara nikamwona. Nikasema leo liwalo na liwe. Huku moyo ukidundadunda nikafika hadi alipo na kumsalimu. Wala sikuwa na mazoea nae kwa kweli. Salamu akaitikia ila kwa kushangaa shangaa. Sikumkawiza, nikamweleza nilihitaji awe wangu (hahahaaa....). Dah ! Nikikumbuka huwa nacheka halafu najisikia vibaya. Basi kwa kuwa ilikuwa ni asubuhi, wala sikuwa na mazoea nae, pia akili za watu muda huo ziliwaza assembly kisha madarasani, kwa kweli majibu niliyopewa ni sawa na kama nilipigwa KO moja safi.
Sikumbuki moja kwa moja au neno kwa neno ila nakumbuka alinitoa nishai. Bahati nzuri sana ni mimi nae tu tulikuwa eneo hilo japo around palikuwa na wanafunzi wengine. Napenda kujipa moyo kuwa hakuna aliyesikia. Basi sikuwa na nguvu tena ya kujadili chochote nikajiondokea hapo na kuelekea bwenini. Bwenini nikajilaza kitandani. Kitanda changu cha juu kwenye deka ila nilijilaza cha chini yake.
Tangu hapo sikusikia tena chochote wala kumuona mtu yoyote, wala sikujua nawaza nini. Nilikuja kushituka wanafunzi wanatoka assembly na wanaingia bwenini chap kama kuna kitu walisahau ili wawahi madarasani. Assembly huchukua zaidi ya nusu saa, kwa maana nyingine ni kama nilizimika kwa zaidi ya nusu saa.
Nikajiinua nami kuelekea darasani. Siku hiyo ilikiwa nzito sana kwangu. Basi nikakubali matokeo na nikajiambia sitathubutu tena. Ikawa hata nikimwona nampitia mbali ili kujiepusha tu.
Ajabu ni kwamba siku zilivyokuwa zinasogea kila tukipishana alikuwa akionyeshaa hali ya kutaka maridhiano. Pengine alitambua kuwa ile nishai aliyonitoa haikuwa saizi yangu. Nilikuwa naona hali ile lakini sikuwa na uthubutu tena !
Siku moja tukiwa assembly nikaitwa na kiranja wa zamu kwenda mbele kuongoza gwaride na sala. Nikapanda pale nikawapigisha mikono juu chini, kando kunja kadhaa kisha nikaanzisha sala. Wakiwa wanaendelea na sala nami nikawa natembeza macho kwa wanafunzi wote. Mara macho yangu yakagingana na mrembo yule aliyekuwa akinitazama kwa kina na utulivu kama ananisoma. Pale pale nikashusha macho chini, sala ikaisha nami nakawalegeza kisha nikashuka pale kuungana na wenzangu
Tangu wakati huo ni kama nikawa niliyemsoma ni mtu aliyetafuta namna ya kufanya maongezi nami, ila kwa bahati mbaya sikuwa tayari tena. Nikalibeba hilo hadi nikamaliza shule na kuondoka zangu, wao wakiwa kidato cha nne wakati huo.
Miaka miwili mbele nikiwa chuo fulani nafanya kazi (temporary), ikawa ni msimu wa chuo kupokea wanachuo wapya. Hamad ! Yule pale... Nimamuona akaniona na kila mmoja akatabasamu. Taratibu kila mmoja akajongea kumsogelea mwenzie kwa lengo la kisalimiana. Kila mmoja alikuwa na tabasamu usoni.
Tulipeana mikono na kusalimiana kwa bashasha na kushangaa tumekutana tena. Alikuwa si yule mrembo aliyenitoa nishai tena, alionekana kupevuka zaidi kifikra. Alionekana kufurahi kuniona tena.
Je, bado nilikiwa yule yule wa KO au nami nilibadilika ? ITAENDELEA...
Sent using Jamii Forums mobile app