Asubuhi inapofika mpaka jioni – usiku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Asubuhi inapofika mpaka jioni – usiku

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Apr 18, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Apr 18, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ASUBUHI INAPOFIKA MPAKA JIONI – USIKU

  Maandiko hapo chini yamekuwa inspired na nyimbo iliyoimbwa na kijana Immanuel katika mjumuiko wa wanazuoni pale soma book café

  ………………………………………..

  Kama kawaida zangu asubuhi imefika napita Chai bora kuelekea Ubungo , hapo chai bora mkono wangu wa kushoto kuna kanisa moja hivi kubwa siku hizi kanisa hilo linazidi kujaa watu sana pembeni mwa kanisa hilo kuna mnara wa simu upande wa kulia kuna nyaya za umeme zimekatiza zinazopeleka umeme visiwani umeme unaopita pale ni mkubwa sana

  Pale kanisani kuna vijana wengi tu wengine walilala mule ndani unajua kwanini ? wengine ni waimba kwaya wengine huwa wanafunga wengine ni wale vijana ambao hawana makazi maalumu kwahiyo inabidi watumie kanisa kama makazi yao kujifanya waimba kwaya au wanasaidia kitu Fulani Fulani ndani ya kanisa

  Mchungaji wa kanisa hilo namjua miaka kadhaa iliyopita wakati namaliza sekondari alikuwa anakawaida sana ya kutembelea mgahawa mmoja wa Mtandao kwa ajili ya kuchukuwa picha na video za ngono wakati kanisa halijaanza kushamiri sana

  Alipotea kidogo kwenda naigeria alivyorudi ndio nikaja kusikia hadidhi zingine kwamba huwa anafufua watu anatenda sana maajabu vijana wanajaa sana kwake kwa ajili ya maajabu hayo jumapili ikifika ndio usiseme magari kibao pale watu kibao mpaka kanisa halitoshi

  Kanisa liko kileleni kwa kilima hapo hapo kuna mnara wa simu sijui watu hawaoni afya zao zinaweza kudhurika kukaa pale pembeni kidogo kuna nyaya za umeme zimepita na tanesco wamepiga marufuku watu kujenga makazi yao karibu na nyaya hizo hapo hapo kuna mabomba ya songas na kuna alama kabisa lakini waumini hawaelewi hiyo

  ………………………………………………………………………….

  Safari yangu inaendelea mbele ya chai bora kuna sehemu moja wanatengeneza matofali huwa naona vijana mbali mbali pale haswa usiku wengi wamebabe mabegi kwa nyuma , basi mimi siku zote nilikuwa nafikiri wale vijana labda ametoka shule wanapiga story pale kumbe yale mabegi yana bidhaa yaani bangi , mirungi na madawa ya kulevya

  Askari huwa wanafanya misako pale na vijana wamezoea kwahiyo wakikamatwa wanakuwa na pesa wakifika kituoni mbezi au rombo wakati mwingine urafiki basi pochi ndio laongea pochi lako likiongea huyooo hakuna mtu wa kukuuliza tena unakuja kuendelea na biashara zako mpaka wakija kufanya doria tena mchezo unakuwa ule ule kupeana pesa .

  Wakati naelekea karibu na jengo la makao makuu ya tanesco naona kuna ubao upande wangu wa kulia umeandikwa ( USIKOJOE HAPA WALA KUTUPA TAKA ) huwa naambiwa mule ndani kuna usalama wa taifa wanaishi mbona taka zimejaa sana pale kwenye bango na kwa kweli wanaotupa taka hizo ni wale wanaochoma mahindi pamoja na wauza miwa .

  ……………………………………………………………………………..

  Ndio kwanza nimefika zangu kituo kikuu cha mabasi ubungo naona vijana wengi sana pale wengine wanaita watu wakapande magari wengine wanataka tiketi nje ili mradi kila mtu na shuguli yake anayoona inamwingizia kipato , halafu nikashikwa na bumbuwazi kuona kijana wa kichina anaita watu wakapande basi lake linaloenda mikoani ( NIKAJISEMA HUYU MCHINA AMEOMBA KIBALI CHA KUFANYA KAZI HII HAPA BONGO AU ?? )

  Sikuwa naenda mikoani nikapanda zangu daladala ndani ya dala dala vijana 2 wakapanda na mimi , nikaenda kukaa kabla ya hapo walikuwa wakinisukuma sukuma lakini sikusema chochote kile nikakaa zangu hawa vijana huwa nawaona pale kituo karibu kila siku sijui kazi yao ni nini haswa

  Kumbe walikuwa wanamtafuta mtu mbele ya safari wakashuka pale manzese kufika magomeni kizee cha watu kinalia kimeibiwa laki 8 kinasema kilikuwa kinataka kwenda kununua bidhaa kariakoo ( KIZEE KINA PESA NYINGI KAMA ZILE HAKINA ACCOUNT BENKI YAKU HIFADHI AKIFIKA KARIAKOO NDIO AWEZE KUDROO AFANYE MANUNUZI YAKE AU ATEMBEE NA KADI YA ATM ?) Wale jamaa sijui walimjuaje yule mzee hata hivyo nilishtuka tu wanavyosukumizana ili mtu upoteze balance .

  Ndani ya basi kila abiria anamshangaa mzee hakuna wa kumsaidia wengine wanacheka , sasa tulipofika kituo cha jirani mtu mwingine alishuka hakutoa nauli konda akamkaba shati atoe nauli ( SI UNAJUA MBONGO USIPOMKUMBUSHA HATOI ) kituo kilichofuatia abiria katoa nauli yake akawa anadai chenji konda kasema hana chenji kama anataka waende mpaka mwisho wa safari ndio ampe chenji yake konda kamwamuru dereva aondoke jamaa wa watu akabaki hajui la kufanya .

  ……………………………………………………………………………

  Nimefika zangu katika kazi zangu za kila siku mara rafiki yangu mmoja mwanasheria akanipigia simu --- ahh bwana maro njoo oficini mara moja kuna kitu nataka utazame , kufika huko kumbe kuna laptop kama mpya hivi imetumika kidogo akaniambia niiangalie halafu niseme bei yake ni ngapi ili anunue

  Nikamuuliza nani anayeuza laptop hiyo naweza kumwona ,kumpigia mwenye laptop kaulizwa jina la mtu anayetaka kuongea nae akatajiwa jina langu ( AHH NIPO MBALI ) hakuweza kuja nilipoongea zaidi na huyo mwanasheria kaniambia yule kijana anazo laptop 5 kwenye buti ya gari yake zimetoka south afrika .

  Sikupenda mjadala nae sana nikaamua kuiangalia nilipowasha nikaona aliiformat ikabidi niweke programu moja hivi ya kuweza kurecover nione ndani ilikuwaje ( niligundua hiyo laptop ilikuwa inatumika marekani na mtu huko Washington na siku 15 kabla alitumia yahoo messenger kuchat mwenyewe ni muhindi )

  Ndio hivyo imekuja kuuzwa kwa mwanasheria – Huyu kijana anaweza kuja kuwa Mwanasheria wetu mkuu huko mbeleni tunapoenda – lakini ameshanunua kitu hicho

  Tulivyoendelea na hadithi zaidi nikamwomba adaptor ya hiyo laptop kumpigia yule jamaa kasema hazikuja na adaptor ila anaweza kununua tu

  NDUGU MSOMAJI ISHARA MOJA YA KUJUA KAMA LAPTOP NI YA WIZI MARA NYINGI HAZINA ADAPTOR AU KUNA NAMBA FULANI HIVI ZINAPISHANA INGAWA KUNA WENGINE HUWA WANANUNUA ADAPTOR ZINGINE .

  ………………………………………………………………………..

  Kazi zangu nyingi nimemaliza kati kati ya jiji naamua kurudi zangu nyumbani jioni nikapanda gari mpaka ubungo ili nikifika hapo nitembee mpaka nyumbani kuchangamsha mwili
  Kuna watu wengi sana ubungo wamachinga kibao wanauza vitu unajua jiji lilikataza wamachinga maeneo yake lakini wako jioni hiyo wanauza vitu kwa mamia na jioni ile vitu bandia vingi sana vinauzwa kuanzia sabuni , simu mpaka nguo na vitu vingine vya ndani .

  Kijana mmoja akaja akanimulika na simu akaniambia ile simu anaiuza alfu 30 nikamwomba aizime na kuwasha tena akaizima na kuiwasha mara mwenzake akafuatia ameshika mfuko nae kanionyesha ingine inafanana nay a mwenzake ila ile ilikuwa inaonyesha mpya zaidi ila bei sawa

  Huyu mmoja akaniambia anataka kunipa ile yake kwa bei pungufu nikamwomba aizime na kuiwasha akaniambia tukajifiche manake pale maaskari kibao nilipokataa wakaniita mwanga kwanini sitaki kwenda

  Ukirogwa kwenda huko kuonyeshwa maana yake wanabadilisha na unapewa simu ingine sio ile uliyoonyeshwa pale , na vijana wengi wanaibiwa pesa zao pale kwa njia zile

  Kabla sijavuka bara bara jioni ile kulikuwa na land cruiser ya polisi imekuja kasi askari akashuka akamkamata kijana mwingine aliyekuwa na simu pale wakamwingiza kwenye gari – wakaondoka na gari lile kufika mbele kunaitwa Ubungo maji kijana yule akashushwa askari wale wamechukuwa simu

  Na siku yangu imeishia hapo – nikaendelea zangu na safari kurudi nyumbani , hata hivyo kwenye simu kulikuwa na pesa kidogo nikaamua kumpigia mbogela kumsalimia aaah ananiambia mambo mazito mtikisoko wa uchumi duniani

  Wakati napiga nilikuwa Kona hapo kuna bar zaidi ya 3 zimefuatana zote watu wamejaa muziki mzito watu wanakunywa na kula na kucheza pool hakuna anayejali tena nje mvua ikija isije wanaendeleza FUJO ndivyo wanavyosema wenyewe

  WEEKEND NJEMA
   
 2. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2009
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Made interesting reading. Keep it up!!
   
Loading...