2. Kuhusu kwingine ambako unatakiwa uandae CV inayojitegemea bila ya kujaza taarifa zako kwenye mfumo, uwe na amani sana. Ma Hr, huwa wanatudanganya kupita maelezo, kwa kutuambia mbwe mbwe nyingi kuhusu uandishi wa Cv, mpaka inafika hatua watu wanakuwa na wasiwasi juu ya namna ipi ni sahihi kuandika Cv.
Ukweli ni kwamba andaa Cv yako kwa standard inayoeleweka na isiyochanganya, punguza manjonjo na urembo, kikubwa kinachoangaliwa sio namna ulivyoiremba au kupanga, suala ni, “Je unavyo wanavyovitaka?”
Kama unavyo vinavyohitajika, viweke vionekane kwa urahisi, kisha jiandae kuvitetea kupitia kuandika na kuongea.