Aslay ataka tuzo ya heshima

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512

Msanii wa Bongo fleva Aslay amesema hajaridhika na mafanikio ambayo ameyapata kupitia mziki wake anaoufanya mpaka atakapo pata tuzo ya heshima hapa Bongo.

Akiongea kupitia eNEWZ Aslay amesema kwamba pamoja na kufanya nyimbo nyingi hali inayopelekea wasanii wengine pamoja na mashabiki kuhisi kwamba amepata mafanikio makubwa, lakini yeye ataridhika pale atakapopata tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya heshima.

Hata hivyo Aslay amesema ataendelea na staili yake ya kutoa nyimbo mfululizo huku akieleza jinsi ambavyo anajisikia furaha baada ya kuona wasanii wengine wa Bongo wanaiga staili yake hiyo.

Aidha Aslay ameweka wazi kuwa hapendi kuweka wazi mambo familia yake ndio sababu kubwa inayomfanya 'asimpost' mtoto wake wa pili na sio kwamba anazuiliwa kufanya hivyo na mpenzi wake wa sasa (Tessychocolate) kama inavyoelezwa mitandaoni.

Kwa undani zaidi usikose kutazama ENEWZ kupitia East Africa Television saa 12:00 Jioni.


Muungwana
 
Yap yap,
Kazi kazi,chapi kazi bwana Aslay.

Kazi yako "Natamba" hakika ilinimbamba vilivyo.

Mafanikio mema kwako!!
 
heshima kwa kipi hasa ? hizi nyimbo alizotoa mwaka jana na mwaka huu ndio anataka tuzo ya heshima.... ?

haka katoto kanakoelekea kanalewa sifa, na ndio utakuwa mwisho wake kimziki kwani atakuja kuwaringia mapromota atakosa shows...

anawajua malejendari wa muziki wa dance, rumba wa miaka hiyo, mpaka bongo flavour wa miaka ya 2000s ? ni yupi anahisi anampita ?
kwanza ana album ngapi ? mtu ambaye anazidiwa umaarufu na vanesa mdee ? anajulikana kenya na bongo tu....

ukweli usiopingika.... at the moment the kid is doing fantanstic kwenye hii tasnia ya muziki wa kizazi kipya, ushauri wangu aendelee kupiga kazi ajipambanue kimataifa kwanza, aache pombe maana nasikia analewa sana now days.
 
Ilinisisimua but haikuwa na maslahi kwa Aslay
Bali iliwafaidisha Ruge na Nandy na wasikilizaji
Ruge ni mzee wa fursa,anakamata fursa apendavyo kwa wasanii.

Ruge ni kama simba hivyo wasanii lazima wawe makini (learning to play with a lions testicles).
 
Hahaha
Halaf ana baht mbaya kweli, alifanya vzuri fella akampeleka kwa yamoto band

Now kawika Ruge ana mtumia vilivo kumpa promo Nandi.
Kama hastuki shauri yake
Ndio mziki wetu huu wa wadau muache utamsikia nae baadae anadai haki za wasanii
 
Back
Top Bottom