Mbona hakuna aliposema kuna baa la njaa? Kasema kuna ukame na upungufu wa chakula jambo ambalo serikali inalitambua na kulichukulia hatua kwa mfano baada ya TMA kutangaza dalili za ukame serikali nzima kuanzia vitongojini mpaka mikoani wanahamasisha mazao yanayohimili ukame hizo hatua zimeanza kuchukuliwa siku nyingi. Lkn bado nchi haina baa la njaa bali kuna upungufu wa chakula especially mahindi lkn nchi bado ina mtama mwingi uwele mwingi mchele mwingi mihogo mingi viazi vingi mazao ya jamii ya kunde pia yako mengi. Jana nimeona mahindi ya kuchoma Tangi bovu vitumbua vimejaa kwa bei ya kawaida mitaani ( Dsm) hiyo ni njaa kweli? Be serious! Huko vijijini pia kuna maeneo machache yamekumbwa na ukame kwa kuchelewa mvua lkn maeneo hayo hayo mvua imeanza kunyesha japo kwa kiwango kidogo. Huyo kiongozi wa dini ni wajibu wake kuwataka waumini waliombee taifa mvua kwani mvua hainunuliwi dukani bali ni m/mungu na hakuna njia nyingine ya kumfikia zaidi ya maombi.