Askofu- Ushoga unaipeleka dunia pabaya

mdau wetu

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
548
57
KUTOKANA na kukua kwa kasi kwa tamaduni za nchi mbalimbali hasa za Magharibi nchini, Serikali imetakiwa kuwa makini na baadhi ya tamaduni hizo kwani zimeonekana kuharibu kwa kiasi kikubwa maadili na sifa ya nchi hasa kwa vijana walio wengi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Jimbo la Kilimanjaro, Glorius Shoo, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu mmomonyoko wa maadili hasa vitendo vya ushoga ulioshika kasi hivi sasa.

Askofu Shoo amesema, ni jambo la aibu na ni dhambi kubwa kwa watu wanaojiita mashoga na kutaka kutambuliwa na Serikali tena kupewa haki na heshima huku wakijua mapenzi ya jinsi moja ni chukizo kwa Mungu kwani huo haukuwa mpango wake tangu alipoumba dunia.

“Jambo hili ni la kusikitisha, tena la aibu kubwa tumekuwa tunasikia mara nyingi watu wanaibuka na tena bila aibu wanajitangaza kuwa wanashiriki mapenzi ya jinsi moja ila cha ajabu hawachukuliwi hatua zozote,” amesema Askofu Shoo.

Amesema, ushoga (mapenzi ya jinsi moja) ni kinyume cha utaratibu ila cha ajabu anashangazwa na mashoga hao kudai kutambuliwa katika Katiba mpya, jambo alilosema linaipeleka dunia pabaya.

Askofu amesema, baadhi ya nchi masikini zimekuwa zikiingia mikataba ambayo pengine athari zake ni pamoja na kuwepo kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsi moja katika jamii ambao bila hofu ya Mungu, sasa imefikia mahali wanadai kutambuliwa kikatiba.

Askofu Shoo amesema ,Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kutokana na watu wake kuwa waadilifu pamoja na kumtii Mungu ila kundi la watu wachache wanaitia doa kwa kujiita mashoga, hivyo kutaka Serikali kutoa tamko juu ya jambo hilo kwani kwa kunyamaza, mashoga hao watajipa moyo kuwa Serikali inawathamini na kuwatambua.

sosi " Habari Leo"

“Sheria zimekuwepo kuhusiana na mapenzi ya jinsi moja ila sasa zinaonekana kukosa nguvu au kukiukwa wazi wazi kwani sheria ya kujamiana watu wa jinsi moja hapo awali ilikuwa ni kifo japokuwa sheria hiyo inaonekana kutokufanya kazi hivi sasa,” alisema.
 

Mkasika

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
391
154
The fact that the West are saying so will not change the Word of God. Our God hates sin and homosexuality is sin and abormination in the eyes of God. Gaysim is perversion of the highest order even animals never practice it yet they dont have power of reasoning. There4 dont try to console yourself or even to show that its ok. This is a disease and its treatable. And its the devil's perfect gift to any willing person.
 

Pota

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
2,018
706
askofu ameongea vizuri, but MAANDIKO yanasema ondoa kwanza kibanzi katika jicho lako kisha uondoe boriti katika
jicho la mwenzako. mi nadhani angekemea kwanza makanisani kwani kuna makanisa na maaskofu wanaoshogoka nk then ndo
aje upande wa serikali
 

Bornvilla

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
924
267
Kutokupenda kutumia vipaji vyetu na akili zetu ndio kunakotuangamiza watanzania na waafrika,kwani kutokana na tamaa zetu za kijinga tunaingia mikataba ya kipumbavu tu na ambayo ina masharti ya kipumbavu kama lazima ushoga utambuliwe! Mfano tumeona kwa majirani zetu na sasa kwetu laja.Walaaniwe wote wanaohamasisha,wanaofanya na wanaofanyiwa! Laana za milele ziwashukie!
 

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,782
4,040
Maaskofu wana akili sana. That is the way to go. Pigeni vita hii uchafu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom