Nina wasiwasi kuwa huyo askofu huenda atapigwa mawe. Sisemi hivyo kwa sababu JK atashinda, ninasema hivyo kwa sababu JK lazima ashinde kwa nji ayoyte ile, au niseme lazima atangazwe mshindi!!!.
Jk ni mtu hatari sana, na sijui kwa nini Mkapa hakuliona hilo, but duru zinasema kuwa Mkapa alitishwa sana. JK alitaka kuingia madarakani kwa njia yoyote ile, alianza kufyeka vikwazo toka mwanzo, marehemu Dr Omari, ambaye ukweli he was the best candidate kuwa mrithi wa Mkapa kuliko JK. Omari akakatika kama mua wa kondeni. Watu kama kina SAS, Sumaye, Malecela, Mwandosya walivunjwa vunjwa isivyo kawaida, na SAS aliyeonekana dhahiri kuwa tishio akazushiwa kashfa mbaya. JK aliutaka uraisi kama sijui nini-- lazima tujiulize kwa nini aliutaka na hata sasa baada ya kufail for the last 5 years, bado anautaka kwa udi na uvumba? Haogopi kutumia hata ushirikina kuhakikisha kuwa anautaka. Huyu ni mtu hatari sana kwa mstakabali wa taifa letu!!
So atatumia nguvu zile zile alizotumia kuwanyamazisha wapinzani wake 2005, kuchakachua kura. This time atatumia jeshi la wananchi wa tanzania, kwa kuwa polisi na usalama wa taifa inaelekea wameshasoma mazingira na wanajua kuna hofu. In all these years, sikuwahi kusikia kutoka nchi yoyote jeshi likiingilia mambo ya uchaguzi na kuwataka wagombea wakubali matokeo. Kazi ya jeshi ni kulinda nchi nje ya mipaka yetu, mambo ya ndani na fujo baada ya uchaguzi ni kazi ya jeshi la polisi.
So huyo askofu atapigwa mawe kwa kuwa mgombea atakayeshindwa ambaye ni JK ndiye atakayetangazwa kuwa ameshinda! Pole sana askofu wetu, lakini moyoni umeshinda kabisa