MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
VIDEO:
Askofu Charles Salala wa Kanisa la Africa Inland Dayosisi ya Pwani Pastoreti ya Magomeni amemwambia Rais Magufuli anachokifanya ni kutumbua majipu madogo madogo kwa sababu jipu kubwa ambalo ni shetani lilishatumbuliwa na Mwenyezi Mungu.
Askofu aliyasema hayo wakati wa Ibada ya kuazimisha Pasaka iliyohudhuriwa na Rais Magufuli na Mkewe, Mama Janeth Magufuli.
Askofu alienda mbali zaidi na kusema, Tanzania inahangaika na jipu mama ambalo ni dhambi. Dhambi hii inazalisha matatizo tunayoyapata leo nchini.
Askofu alisema, ‘’watumishi hewa ni matunda ya majipu madogo madogo yaliyotoka kwa jibu mama ambalo ni dhambi’’
‘’Mheshimiwa Rais kazi ipo kwa ajili ya majipu madogo madogo yanayoleta watumishi hewa, wanafunzi hewa, mikopo hewa, kila kitu hewa. Tunaomba Mwenyezi Mungu akupe neema ya kuweza kuyatumbua. Sisi tunakuunga mkono’’ Alisema.
Rais Magufuli alishukuru sana kupata mafundisho/mahubiri kutoka kwa Askofu ambayo yamemfundisha na kumfungua kuhusu dhana ya jipu Mama, majipu na dhambi.
Rais alimaliza kwa kuwaomba waumini waendelee kuliombea taifa amani na utulivu ili matarajio ya maendeleo zaidi kwa wananchi wapenda amani yatimie.