Askofu Mlawi alaani vikali Matukio ya Utekaji: Asema ni dalili ya kukosekana kwa Amani

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,514
Reaction score
6,070
Askofu Mkuu wa Makanisa ya SPCT na Rais wa Umoja wa Maaskofu, Wachungaji, Mitume, Manabii na Madhehebu ya Kikristo Tanzania, Askofu Musa Mlawi, ameibuka na kulaani vikali vitendo vya utekaji vinavyoendelea kushuhudiwa nchini, akivitaja kuwa dalili ya kukosekana kwa amani.

Ametoa wito huo jijini Dodoma, wakati akizungumza na Jambo Tv akieleza kuwa Vitendo vya watu kutekwa, kuvamiwa, kupigwa na kuteswa ni jambo linalotia hofu.

"Ingawa bado hatujajua ni nani wanaofanya haya, wala wanatoka wapi, sisi kama viongozi wa dini tunabaki kushangaa," amesema Askofu Mlawi.

Amesema anaamini kuwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na serikali havihusiki moja kwa moja na matukio hayo, bali kuna uwezekano wa kuwapo kwa kikundi kisichojulikana kinachofanya vitendo hivyo kwa nia ovu.

Askofu Mlawi amemwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuliangalia kwa uzito suala hili linalotishia usalama wa raia na kuchafua taswira ya taifa.

"Ni jambo la kushangaza kuona matukio haya yakitokea ilhali vyombo vya ulinzi vipo, lakini hakuna hata mmoja aliyekamatwa na kufikishwa mahakamani. Tunajiuliza, ni nani wanaofanya haya? Kwa nini hakuna hatua zinazochukuliwa?" alihoji kwa msisitizo.

Amesisitiza kuwa Watanzania wanahitaji majibu ya wazi kutoka kwa vyombo husika ili kurejesha imani ya wananchi kwa taasisi za ulinzi na usalama, pamoja na uthibitisho kuwa hakuna watu walio juu ya sheria.
Source: Jambo TV
 
View attachment 3358988
Wahusika wanataka mpaka mawe yaimbe ndio waone kuwa this issue is serious
 
Ni muda sasa wa kumtoa mkoloni mweusi
 
Vilio vimekmvuka mipaka saaa

Haleluyaaa
 
Amesema anaamini kuwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na serikali havihusiki moja kwa moja na matukio hayo, bali kuna uwezekano wa kuwapo kwa kikundi kisichojulikana kinachofanya vitendo hivyo kwa nia ovu.
Kikundi kisichojulikana tena?
Huyu yupo nyuma ya muda
 
Hadi mawe yataongea na bado.
Hatutaki ufirauni kwenye taifa letu
 
Kama hajatumwa ku nuetralize sakata la gwajima poa ila asipate misukosuko naye akaambiwa anaingiza chuki kwa wananchi waichukie serikali. Na kama naye kaamu kujilipua basi ajiandae vema kufutiwa usajili kanisa lake
 
Mwamposa akijitokeza kupinga kama wenzake atashukiwa kwa kasi ya ajabu kama mwewe achukuapo kifaranga cha kuku. Kwanza watamuambia anauza maji na mafuta feki ya upako, yule ndio hawakosi sababu za kumsulubu, bora akae kimya tu na awe chawa pro max
 
Back
Top Bottom