Askofu Methodius Kilaini: Rais chaguo la Mungu huyu hapa

Askofu Methodius Kilaini: Rais chaguo la Mungu huyu hapa

Mpalakugenda

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2015
Posts
4,649
Reaction score
5,083
Askofu Kilaini ametaja sifa za rais anayetakiwa, moja ya hizo ni kumcha Mungu.

Najiuliza kati ya hawa wawili Lowassa na Magufuli nani anayo?

==============================

Kilaini : Rais chaguo la Mungu huyu hapa.

Rais ajaye baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, anapaswa kuwa na sifa nane muhimu ili akidhi kigezo cha kuliongoza taifa hili vizuri na kwa mafanikio

Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba.

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, hatimaye Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba ameibuka na kutoa sifa za rais chaguo la Mungu kutoka katika orodha ya wagombea nane wa nafasi hiyo wakiwamo Dk. John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Edward Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akizungumza katika mahojiano maalum na Nipashe mwishoni mwa wiki, Askofu Kilaini anayekumbukwa zaidi kwa madai kuwa ndiye aliyemtabiria Rais Jakaya Kikwete, kuwa Rais baada ya kumtaja ndiye chaguo la Mungu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, alisema rais ajaye baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, anapaswa kuwa na walau sifa nane muhimu ili akidhi kigezo cha kuliongoza taifa hili vizuri na kwa mafanikio.

Mosi, Askofu Kilaini aliitaja sifa ya uadilifu, akisema ni muhimu kwa kila mgombea anayepaswa kuliongoza taifa hili baada ya uchaguzi mkuu mwezi ujao.
Askofu Kilaini aliitaja sifa ya pili kuwa ni 'kuchapa kazi kwa vitendo'. Alisema sifa hii pia ni muhimu kwa Rais ajaye kwani atalazimika kuonyesha kwa vitendo katika kuchapa kazi na siyo kinyume chake.

Sifa ya tatu kwa rais chaguo la Mungu, kwa mujibu wa Askofu Kilaini, ni kwa mgombea atakayekuwa akitekeleza majukumu yake ipasavyo huku sifa ya nne ikiwa ni hali ya kuwa na uzalendo wa kweli, kwa kufanya kila jambo kwa maslahi ya taifa.

Sifa ya tano kwa rais anayepaswa kuongoza taifa hili ni kuwa mchamungu, sifa ya sita kuwa ni mpenda watu huku ya saba, kwa mujibu wa Kilaini, ni kuwa mtu asiye bosi kwa wananchi bali mtumishi wao (wananchi).

"Sifa nyingine (ya nane) ni ujasiri wa kuweza kuwakemea wale wote wasio waadilifu (katika serikali yake)," alisema Askofu Kilaini.

Alipotakiwa amtaje kwa jina mgombea anayetimiza vigezo hivyo vya kuwa "Chaguo la Mungu", Askofu Kilaini alisema hawezi kufanya hivyo sasa na badala yake anasubiri uchaguzi ukishafanyika kwani anaamini kuwa nguvu ya Mwenyezi Mungu ni kubwa na kwa vyovyote vile, kiongozi ajaye (rais) atapatikana kwa nguvu yake (Mungu).

Mbali na Magufuli na Lowassa anayewakilisha pia vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya Chadema, NLD, NCCR-Mageuzi na Chama cha Wananchi (CUF), wagombea wengine wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Chifu Lutasola Yemba wa ADC, Janken Kasambala wa NRA, Fahmy Dovutwa wa UPDP, Anna Mghwira wa ACT-Wazalendo, Hashim Rungwe wa Chaumma na Maximilian Lymo wa TLP.

ATOA MAZITO
Katika hatua nyingine, Askofu Kilaini amewataka Dk. Magufuli, Lowassa na wagombea wengine wa urais kuwakumbusha watu wao kuwa wazingatie kuiweka mbele amani ya nchi kwani uchaguzi ukimalizika maisha yataendelea kama kawaida.

"Ninalowaasa Watanzania wasipoteze fursa hii ya kuwasikiliza wagombea. Watu wafurahi, uchaguzi si vita si, watu kuchukiana, uwe wakati wa kufurahi licha ya kuwapo mapungufu madogo... lazima tulinde amani yetu kwani mara baada ya uchaguzi maisha yataendelea," alisema Askofu Kilaini.

Hata hivyo, Kilaini alisema kuwa anachofarijika ni kuona kuwa hadi sasa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu zinaendelea kufanyika kwa amani na kwamba, hadi sasa hakuna tukio kubwa la kuogofya kiasi cha kutishia amani ya taifa.

"Angalau kwa wagombea wakubwa (wa nafasi za urais), bado hatujapata kitu kibaya kama kuhamasisha watu wachaguane kwa dini, ukabila na ukanda. Hilo linakatazwa kwenye katiba yetu na sisi viongozi (wa dini) hatuwezi kuacha kulikemea hilo kila wakati linapojitokeza... daima tunapaswa kuwakumbusha watu kuwa siasa si mahala pa udini, ukanda na wala si mahala pa ukabila," alisema Askofu Kilaini.

Aidha, aliongeza kuwa ni wajibu pia kwa viongozi wa dini wakiwamo wa kanisa lake (Katoliki) kuhakikisha kuwa wanawahamasisha watu kujitokeza kwenye kampeni, kusikiliza ahadi za wagombea na vyama vyao na mwishowe kujitokeza siku ya kupiga kura ili kuwachagua watu wanaoamini kuwa wanafaa kuongoza.

"Ninalowaasa Watanzania ni kwamba wasipoteze fursa hii (ya mikutano ya kampeni). Wajitokeze kuwasikiliza wagombea na kuchambua ilani na ahadi wanazotoa kabla ya kufanya uamuzi siku ya kupiga kura," alisema.

DINI NA SIASA
Kilaini alisema miongoni mwa kasoro chache zilizojitokeza hadi sasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi ni kuwapo kwa baadhi ya viongozi wa dini wanaoonekana kuchanganya siasa na dini, ingawa hilo halijaleta athari kubwa hadi kufikia sasa.

Alisema yeye na viongozi wengine wa dini hawaachi kukumbushana juu ya wajibu wao katika kipindi hiki ambao ni pamoja na kutoonyesha ukereketwa kwa chama au kwa mgombea yeyote na pia kuwatayarisha watu ili wapige kura kwa haki, amani na uhuru.

Alisema hivi karibuni, viongozi wa dini nchini walikutana na maafisa wa serikali wakiwamo Mkuu wa Jeshi la Polisi, Msajili wa Vyama vya Siasa na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kujadili mambo mbalimbali kuhusiana na uchaguzi na mwishowe walikubaliana kuwa wao (viongozi wa dini) wasionyeshe ukereketwa wa vyama wala wagombea binafsi na kamwe sehemu za ibada zisitumike kwa kampeini za siasa.

Alisema nafasi ya kanisa lao (Katoliki) kwa uchaguzi wowote ule ukiwamo wa Tanzania ni kuhamasisha watu wawe na uhuru wa kuchagua mtu wamtakaye, kuhamasisha haki itendeke ili kila mmoja aridhike na matokeo na pia, kuhamasisha amani ambayo ni tunu muhimu kwa taifa.
 
Aliyemwekea dk.mwakyembe su.... anatakiwa kutubu kwanza
 
Familia ya lowasa ni familia onayofuata sana misingi ya imani yao

Imani ya familia ya lowasa hii hapa

LOWASA.jpg
 
Hii sifa sio ya lazima... infact kuleta maswala ya dini kwenye serikali ni kitu hua napingana nacho kila siku, dini ina limits nyingi sana sio waislamu, wakristo, buddhist,.... Mtu ambaye atakaa anafata kanuni za dini anaziapply kwenye kuendesha nchi tutegemee shida tu huko mbele.
 
Mkuu Naomba Uweke Sifa Zote Alizozisema Askofu Kilaini Mimi Nimesoma Heading Tu Kwenye Gazeti,
 
Ni muhimu kuwa na kiongozi mwenye hofu ya Mungu ili aongoze kwa hofu ya Mungu,magufuli anatosha katika hili
 
Hii sifa sio ya lazima... infact kuleta maswala ya dini kwenye serikali ni kitu hua napingana nacho kila siku, dini ina limits nyingi sana sio waislamu, wakristo, buddhist,.... Mtu ambaye atakaa anafata kanuni za dini anaziapply kwenye kuendesha nchi tutegemee shida tu huko mbele.

Mamlaka zote zinatoka juu na ndo maana hata kabla ya binge kuanza ni lazima kuwepo na dua kwanza kwa watu kumcha mwenyezi, ni lazima rais alielewe hilo, aliishi na aliheshimu ..sasa huwezi kumpata wa kufanya hayo kama hana uchaji wa Mungu kwanza
 
Familia ya lowasa ni familia onayofuata sana misingi ya imani yao

Nakushangaa wewe unayejiita "boyfriendy" unajiwekea unaandika vilivyo nje ya uzi ulioulizwa. Kihere here cha nini? Kwa kuwa umeliazisha mwenyewe, Dk. Magufuli ndiye mcha Mungu maana kuanzia utoto wake Kanisa ndiyo msingi wa maisha yake. Dk. Magufuli mcha Mungu hoyeeeeeeee
 
Sijawahi kuona picha ya magufuli akiwa kanisani,halafu hiyo picha low as a alikuwa anasimikwa uchifu wa unyamwezini
 
Imani ya familia ya lowasa hii hapa

LOWASA.jpg

Hapo lowasa alikuwa anasimikwa kuwa chifu wa wanyamwezi,wanyamwezi akiwemo sitta,said nkumba...walitambua uwezo wa lowasa mapema,hebu angalia MTU kama sitta anaongozwa NA chifu lowasa NA hana matatizo,huyu lowasa ni jembe,masheikh,wachungaji wotr walitoa unabii
 
Nakushangaa wewe unayejiita "boyfriendy" unajiwekea unaandika vilivyo nje ya uzi ulioulizwa. Kihere here cha nini? Kwa kuwa umeliazisha mwenyewe, Dk. Magufuli ndiye mcha Mungu maana kuanzia utoto wake Kanisa ndiyo msingi wa maisha yake. Dk. Magufuli mcha Mungu hoyeeeeeeee

Utakua umedata si bure, ebu soma alichoandika mtoa mada alafu ujiulize kipi kipi nilichoandika kipo nje ya mada? Na sidhani kama unamfahamu vizuri uyo magufuli vinginevyo utakua upo hewani hewani usiyejua yaliyomo
 
Askofu Kilaini ametaja sifa za rais anayetakiwa, moja ya hizo ni kumcha Mungu.

Najiuliza kati ya hawa wawili Lowassa na Magufuli nani anayo?

Lowassa.....
 

Attachments

  • Lowassa.2.jpeg
    Lowassa.2.jpeg
    2.5 KB · Views: 884
  • Lowassa.jpeg
    Lowassa.jpeg
    5.5 KB · Views: 881
  • Lowassa.3.jpg
    Lowassa.3.jpg
    25.9 KB · Views: 250
Yanaongelewa mengi sana juu ya hili lakini ukweli ulio dhahiri ni kwamba tunahitaji RAISI mwenye hofu ya Mungu ndani yake, bila hivyo Nchi itaangamia na wizi, ubadhirifu na maovu mengi kuaongezeka, lakini RAISI mwenye hofu ya Mungu atayanyoosha haya.......je ninani kati ya wagombea hawa ana hofu ya Mungu, mifano iko hai fatana nami.... kwani huyo ndio RAISI ajae kwani chaguo la watu ni chaguo la Mungu......
 
Yanaongelewa mengi sana juu ya hili lakini ukweli ulio dhahiri ni kwamba tunahitaji RAISI mwenye hofu ya Mungu ndani yake, bila hivyo Nchi itaangamia na wizi, ubadhirifu na maovu mengi kuaongezeka, lakini RAISI mwenye hofu ya Mungu atayanyoosha haya.......je ninani kati ya wagombea hawa ana hofu ya Mungu, mifano iko hai fatana nami.... kwani huyo ndio RAISI ajae kwani chaguo la watu ni chaguo la Mungu......
Mkuu, hofu ya Mungu unaipimaje ? Kwa kuhudhuria Msikitini, Kanisani au Dini asili ya Babu yake kila siku ?
 
Kweli mkuu tena Huyo pamoja na hofu ya MUNGU ana hofu na watanzania na ana hofu na nguvu ya uma ndiyo maana amejiunga na ukawa kuleta mabadiliko
 
Katika hili Lowassa ndiye mwenye hofu ya Mungu.
Tazama anavyoishi na familia yake na yule mwingine ni tofauti.
Ukitaka kujua baba mwema kwa familia angalia tabasamu la mke wake.....hapa sina haja ya kufafanua maana liko wazi.
 
Back
Top Bottom