Askofu Malasusa: Ni makosa kuziita Hospital na Shule za Kanisa kuwa ni za Binafsi ziitwe za Kiroho ndio sababu hazina gharama kubwa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
89,458
154,684
Askofu wa KKKT DMP Dr Malasusa amesema Shule na Hospital za Kanisa siyo za Binafsi kama zinavyoitwa na Wengi bali Hizi ni Huduma za Kiroho

Askofu Malasusa amesema Shule za Binafsi kuna zinazochaji hadi Ada ya sh milioni 9 kwa Primary lakini huwezi kukuta ada kama hiyo kwenye Shule za Kanisa

Askofu Malasusa amesema hayo kwenye Sherehe za miaka 30 za Shule ya Kisarawe zilizofanyika Mkuza Kibaha

Source: Upendo TV
 
Ni aidha Public or Private huo ukiroho unaingiaje wakati shule zinafundisha elimu dunia? Au mtu akianzisha shule yake ada akaweka kama ya seminari inakuwa ya kiroho nayo?
 
Malasusa hizo nishule za taasisi za dini sio mtu binafsi baaasi!
iwe taasisi ya kiroho au ya kimwili ilo simuhimu kulitanabaisha ... lipeni kodi mnahela nyingi mnapewaga tena hazipigwi kodi samaanyi lkn
 
Matibabu ni ya kiroho pia? 🤣🤣🤣
Askofu aache mbwembwe.

Nadhani madai sahihi ni zisajikiwe kama 'non-profit organizations' na zipewe misamaha ya kodi kwa ahadi ya kutoa huduma kwa gharama nafuu.

Uendeshaji wake unajikita kwenye kutoa huduma kwa maana hawatafuti faida.
 
Hiyo nonprofit huekewi maana

Nonprofit maana yake ni kuwa faida inayopatikana hawagawani wamiliki inatumika kuendeleza kazi za taasisi!!

Sio kwamba inaendeshwa bila faida yaweza kuwa yapata faida kuliko kampuya Azam kwenye shughuli zake ila hawagawani kila mtu akale kwao

Ndio maana makanisa yana miradi kibao ,mashule ya bei nk lengo yajiendeshe na padri au sista mwendeshaji asije kosa nguo kwa kutembea uchi kisa waumini wamegoma kutoa sadaka kanisani

Faida ya mradi inafidia
 
Ni aidha Public or Private huo ukiroho unaingiaje wakati shule zinafundisha elimu dunia? Au mtu akianzisha shule yake ada akaweka kama ya seminari inakuwa ya kiroho nayo?
Amechoka kimwili na kiroho.
Hakuna unafuu wowote
 
Matibabu ni ya kiroho pia? 🤣🤣🤣
Askofu aache mbwembwe.

Nadhani madai sahihi ni zisajikiwe kama 'non-profit organizations' na zipewe misamaha ya kodi kwa ahadi ya kutoa huduma kwa gharama nafuu.

Uendeshaji wake unajikita kwenye kutoa huduma kwa maana hawatafuti faida.
Kwani sasa zimesajiliwa kama nini?
 
Askofu wa KKKT DMP Dr Malasusa amesema Shule na Hospital za Kanisa siyo za Binafsi kama zinavyoitwa na Wengi bali Hizi ni Huduma za Kiroho

Askofu Malasusa amesema Shule za Binafsi kuna zinazochaji hadi Ada ya sh milioni 9 kwa Primary lakini huwezi kukuta ada kama hiyo kwenye Shule za Kanisa

Askofu Malasusa amesema hayo kwenye Sherehe za miaka 30 za Shule ya Kisarawe zilizofanyika Mkuza Kibaha

Source: Upendo TV
Mwizi kama mwizi tu

USSR
 
Mmnh za Kiroho?!

Labda tupendekeze jina lingine lakini kwenye u-kiroho sizani!

Watu wenyewe wako mwilini muda mwingi kama si wote!
 
Malasusa hizo nishule za taasisi binafsi sio mtu binafsi baaasi!
iwe taasisi ya kiroho au ya kimwili ilo simuhimu kulitanabaisha ... lipeni kodi mnahela nyingi mnapewaga tena hazipigwi kodi samaanyi lkn
unajua neno binafsi lina tafsiri yake.je binafsi ni nafsi ya ngapi labda tuanzie hapo kupata tafsiri sahihi.(personal property).kiswahili wakati mwingine kinachanganya watu.
 
Hiyo Ada ndogo ni Tsh. Ngapi anamaanisha huyu Mzee?

Au milioni mbili siku hizi imeshakuwa bei ndogo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom