Askofu KKKT atuhumiwa kuibua uasi

Apr 18, 2012
95
213
pic+kkt.jpg

Dar es Salaam. Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Dk Owdenburg Mdegela amepewa onyo na mkuu wa kanisa hilo nchini, Dk Frederick Shoo kuacha mipango aliyodai ya kuratibu uasi.
Dk Shoo amefikia hatua hiyo baada ya kudai kuwa Dk Mdegela ametangaza dayosisi teule ya Mufindi iliyopo ndani ya Dayosisi ya Kusini yenye makao makuu yake mkoani Njombe kuanzia Januari Mosi, 2019.
Onyo la Dk Shoo, ambaye pia ni askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini amelitoa kupitia barua aliyoiandika Desemba 3 kwenda kwa Mkuu wa Jimbo la Mufindi, Dk Anthony Kipangula na kuagiza isomwe juzi Jumapili kwenye sharika zote za jimbo hilo.
Katika barua hiyo yenye kurasa mbili, Dk Shoo amemtaka Askofu Mdegela kutunza ahadi na heshima yake kwa kutojihusisha na uasi huo, la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
“Washarika wote wa KKKT, Jimbo la Mufindi wanaonywa kutojiunga kabisa na uasi huu,” anasema Dk Shoo.
Hata hivyo, Askofu Mdegela akizungumza na Mwananchi jana juu ya tuhuma za uasi na onyo alilopewa, alisema yeye amestaafu na anachofanya ni kuchunga kondoo wa Bwana.
“Mufindi hakuna uasi na kuandikiana barua ni utoto, kwa nini tusikae tukazungumza. (Rais mstaafu Benjamin) Mkapa alisema watu wazima wanakaa wanazungumza, watoto ndiyo wanaandikiana barua,” alisema kiongozi huyo wa kiroho aliyestaafu mwaka jana.
“Mgogoro huu unachangiwa na vitendo vya kibabe na kihuni vinavyofanywa na Askofu (wa Dayosisi ya Kusini-Isaya) Mengele ambaye hafai kuwa askofu,” alisema Mdegela.
Akizungumzia tuhuma hizo, Askofu Mengele alisema, “Mgogoro unachangiwa sehemu kubwa na askofu mwenzetu mstaafu Mdegela na anachokifanya anaingilia eneo jingine la utawala, ni sawa na Idi Amin alivyojitangazia Kagera kuwa Uganda.”
“Ningekuwa Serikali, ina maana ningekuwa na majeshi, ningeingiza jeshi vitani, lakini kwa kuwa ni dini kuna timu ya maaskaofu kumi inayoongozwa na Askofu Benson Bagonza italishughulikia hili,” alisema Askofu Mengele.
Kuhusu barua hiyo kutokusomwa juzi, Askofu Mengele alisema itakuwa wahusika waliowaaminisha washirika wa Mufindi kuwa ni dayosisi na msimamo wa kanisa ni kinyume chake waliona inaweza kuwaondolea imani kwa waumini.
Barua ya Dk Shoo ina kichwa cha habari, ‘Jimbo la Mufindi kujitangaza kuwa Dayosisi ya maandalizi Mufindi.’
Inasema, “Nimesikitishwa sana na kitendo cha uasi. KKKT lina utaratibu wake wa kikatiba kuhusu kuzaliwa kwa dayosisi mpya. Uamuzi wenu wa kujitangaza kuwa eneo la KKKT Dayosisi ya Maandalio ni batili na inakiuka utaratibu wa kanisa letu.”
“Kwa kitendo hicho mmeonyesha wazi kuwa mmetetereka, kudharau na kukataa ushauri mliopewa wa kuleta suluhu kwa mgogoro kati ya Jimbo la Mufindi na Dayosisi ya Kusini.”
Dk Shoo anasema hadi sasa Jimbo la Mufindi ni sehemu ya KKKT Dayosisi ya Kusini kikatiba na kisheria. Anasema, “kitendo cha kujiengua na kujitangaza kama mlivyofanya kamwe hakiwezi kupata baraka za kanisa kwa kuwa ni uasi.”
“Dayosisi ya Kusini iliyo moja ya Dayosisi 26 za KKKT inayo mamlaka kamili kikatiba na kisheria ya kuwachukulia hatua stahiki dhidi ya uamuzi huo na kuwawajibisha wote wanaohusika kwenye uasi huu,” inasema barua hiyo.
Tayari Askofu wa Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza ameteuliwa kuongoza kamati maalumu ya halmashauri kuu ya wajumbe kumi kushughulikia mgogoro huo na Dk Shoo ameitaka kufanya wajibu wake mapema iwezekanavyo.
Mwananchi limezungumza na Askofu Bagonza kuhusu kamati hiyo iliyoteuliwa Septemba jinsi itakavyofanya kazi na amesema wanatarajia kwenda huko baada ya sikukuu ya Krismasi.
“Baada ya kuteuliwa, nilishindwa kwenda kwa sababu kipindi hicho nilikuwa namuuguza mke wangu ambaye baadaye alifariki dunia, lakini kwa sasa najipanga pamoja na wajumbe wengine 10 ambao ni maaskofu kuangalia ratiba zao ili twende,” alisema.
Alisema watakachokwenda kufanya ni kuzungumza na washarika wa Mufindi utaratibu unaopaswa kufuatwa ili kupata dayosisi kwa mujibu wa katiba ya KKKT na si vinginevyo.
Aligusia njia zinazotumika kupata dayosisi kuwa, mosi ni kwa dayosisi ya eneo husika mfano Kusini ambayo Mufindi iko ndani yake kwenda KKKT makao makuu kueleza kuwa eneo lao limekuwa kubwa, hivyo wanaiomba Mufindi kuwa dayosisi.
Pili, alisema ni kwa KKKT makao makuu kuona eneo la dayosisi fulani limekuwa kubwa hivyo kutangaza dayosisi mpya. “Kinachofanyika Mufindi ni kinyume cha utaratibu na katiba ya KKKT,” alisema Askofu Bagonza.
 
Kuwa kiongozi wa kiroho ni wito lakini ikiwa ni kazi basi inakuwa kazi kweli kweli
 
Mgogoro huu unahitaji kutumia busara kubwa saana kuumaliza
 
Back
Top Bottom