nivoj.sued
JF-Expert Member
- Jul 14, 2009
- 221
- 190
Askofu Kilaini ametakiwa kumfunda JPM kuhusu matumizi ya kanuni ya siasa ya ujamaa na kujitegemea. Kwa maelezo zaidi soma hapa chini:
==============================================
Askofu Kilaini Atakiwa Kumfunda JPM Kuhusu Kanuni ya Sera Auni, kwa Maana ya,“The Principle Of Subsidiarity”
Akiwa mkoani Kagera, Rais John Pombe Magufuli, baada ya kuhudhuria ibada ya mwaka mpya, alianza ziara ya kukutana na wananchi waliothiriwa na tetemeko la ardhi la Septemba 10, 2015. Katika ziara hizo, Rais Magufuli alisikika akisema yafuatayo, kati ya mambo mengine:
"Nimekuja kuwapa ujumbe huu, na mwenye kusikia asikie: Panapotokea janga kama vile tetemeko, jukumu la serikali ni kurejesha miundombinu ya umma, siyo kujenga nyumba za wananchi. Asitokee mtu kuwadanganya kwamba serikali itagawa chakula, kwani hatuwezi kugawa chakula kwa watu wanaoishi katika mazingira ya kijani. Ndugu Mkuu wa Wilaya nataka nikueleze hapa, sitaleta chakula hapa Bukoba, kwani serikali haina shamba. Kwa hiyo kila mmoja katika upande wake abebe msalaba wake mwenyewe. Tuachane na mambo ya kwenda kwenye ‘kijiji cha katerero,’ ‘kuogelea kwenye mto ngono,’ na ‘kuzurura kwenye kijiji cha Luterangoma,’ na badala yake tuchape kazi” (Paraphrased).
Pia unaweza kusikiliza audio clip hapa:
Maneno haya yamelalamikiwa sana na watu wengi kwenye mitandao ya kijamii. Kila mmoja anatoa sababu yuke. Baadhi wanalaumu ukavu wa kauli. Wengine maudhui. Lakini, mimi siushangai ukavu wa maneno ya Rais Magufuli. Nina shida na maudhui yake kwa sehemu fulani. Nataka kuonyesha hilo.
Nimefanya kazi kama mhadhiri katika vyuo vya LearnIT na IIT, ambako nilikuwa na jukumu la kusimamia tasnifu za utafiiti wa wanafunzi wangu, kati ya majukumu mengine.
Mara zote nilipokuwa nasimamia dissertations za wanafunzi wangu, niligombana nao sana kuhusu sura ya tatu, inayohusu utaratibu wa utafiti (methodology). Nilikuwa nawauliza swali: What is your research philosophy? Wengi walikuwa hawajui jawabu.
Ilibidi kuwaongoza taratibu. Kwa kuanzia nilikuwa nawambia wakasome tena sura ya nne juu ya “Understanding research philosophies and approaches,” katika kitabu kifuatacho: Mark Saunders, Philip Lewis and Adrian Thornhill, RESEARCH METHODS FOR BUSINESS STUDENTS, 5th Edition(London: Pearson Professional Limited, 2009)
Kwa mujibu wa kitabu hiki, kuna kambi kuu mbili za research philosophies: kambi ya Realism / Postitivism dhidi ya kambi ya Phenomenology / Constructionism. Kambi ya kwanza wanasema koleo ni koleo, sio kijiko. Yaani, ukweli unagunduliwa, hauchongwi na msemaji. Na kambi ya pili wanasema koleo inaweza kuitwa kijiko bila tatizo kubwa. Yaani, ukweli unaweza kuchongwa, 2+2 ikawa tano, kwa sababu kura zilizopigwa zinasema hivyo!
Kwa ujumla, tangu tupate uhuru tulikuwa na marais wanafenomena. Sasa kwa mara ya kwanza tunaye rais mwanasayansi. Tuukubali ukweli huo. He is a positivist, fullstop. Hivyo, tunapojadili kauli zake tuzijadili tukiwa tumevaa miwani ya positivism. Ni kwa njia hii, tunaweza kumwelewa, japo sio lazima tukubaliani naye. Katika hili ninalolisema, hoja yangu ni hii:
Kwanza lazima tujiulize: “Ukweli ni kitu gani, na tunaweza kuupataje?”
Pili, yafaa tujue kuwa, “Ama ukweli uko mahali fulani nje ya vichwa vyetu na unasubiri kugunduliwa, au ukweli unachongwa kwa kutumia ndimi zetu.”
Tatu, tukumbuke kuwa, “Kama ukweli unagunduliwa, basi tunaweza kubishana kwa ufanisi, lakini kama ukweli unachongwa, basi mabishano yote juu ya kauli yoyote ni kupoteza juda.”
Hivyo, “kabla ya kuzihakiki kauli za JPM's lazima tkubaliane juu ya msimamo wa pamoja juu ya masuala haya ya kiepistemolojia na kiontolojia.”
Tunafahamu kuwa, “JPM mwanasayansi, yaani "positivist.” Na kwa hiyo, “yafaa kuhakiki kauli zake kwa kutumia miwani ya kisayansi.” Ni kwa njia hiyo, tutaepuka kuanguka katika mtaro wa upendeleo (subjectivism/bias).
Kwa kutumia mtazamo huu, hebu sasa tuchunguze baadhi ya kauli za JPM kwa mujibu wa hotuba yake ya Bukoba, wakati akiwahutubia waanchi katika viwanja vya shule ya Ihungo.
Niwazi kwamba, ujumbe wa JPM una ukakasi kwa kuwa ni mkavu. Lakini, ni maoni yangu kuwa, kwa vile JPM ni Rais Mwanasayansi, ukavu wa maneno yake halipaswi kuwa tatizo. Badala yake, tatizo linapaswa kutafutwa katika udhati (objectivity) wa kauli zenyewe.
Na udhati huo unatafutwa kwa kuzingatia kuwa, anayeongea ni Mkuu wa nchi, anayeongoza nchi kwa mujibu wa katiba na sheria. Hivyo, kauli zake zinapimwa kwa kutumia mizania hiyo. Nitaonyesha mfano wa namna ya kuhakiki maneno ya JPM, na hivyo kuyakosoa kwa kuzingatia kiwango cha udhati wake.
JPM, kama mkuu wa nchi, anapaswa kusimamia utekelezaji wa shughuli za serikali kwa kuzingatia “kanuni ya siasa ya ujamaa na kujitegemea.” Hivyo ndivyo ibara ya 9 ya katiba ya Tanzania(1977) aliyoahidi kulinda inavyosema.
Yaani, “Lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya Muungano… kutokana na kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ambayo inasisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano (ib.9)”
Katika mtazamo wa kifalsafa, kuongelea “kanuni ya siasa ya ujamaa na kujitegemea,” ni kuongelea “PRINCIPLE OF SUBSIDIARITY.” Siku moja, Mwalimu Nyerere, alikuwa na haya ya kusema kuhusu kanuni hii, ya Ujamaa na Kujitegemea:
“The first and the most important distinction should be drawn between the negative concept of socialism and self-reliance and the positive concept of it."
"Basically the negative concept of socialism and self-reliance refers to the limitation of competences of the 'higher' organization in relation to the 'lower' entity, whilst its positive concept represents the possibility or even the obligation of interventions from the higher organization. We can clarify this distinction in the following way."
“The negative concept of socialism and self-reliance states that: (1) the higher entity cannot intervene if the lower entity can satisfactorily accomplish its aims, or (2) the higher entity should not intervene if the lower entity alone can accomplish its aims, or (3) the higher entity must not intervene if it is not assigned to do so."
“The positive concept of socialism and self-reliance states that: (1) the higher entity can intervene if the lower entity cannot satisfactorily accomplish its aims, or (2) the higher entity should intervene if the lower entity alone cannot accomplish its aims, or 3) the higher entity must intervene if it is assigned to do so.”
Kwa sababu hii, kanuni ya siasa ya ujamaa na kujitegemea ni kanuni inayoongelea mfumo wa mkamilishano uliopo kati ya serikali kuu, serikali ya mkoa, serikali ya wilaya, serikali ya kata, serikali ya kijiji, serikali ya kitongoji mpaka kaya. Zote nizi ni “entities” zinazoongelewa.
Kwa hiyo, kauli ya JPM kwamba, “kila mmoja katika upande wake abebe msalaba wake mwenyewe,” inaeleweka na kukubalika.
Lakini, tatizo liko katika kujua "upande" wa serikali kuu ni upi na "upande" wa serikali ya mkoa/wilaya/kata/kijiji/kaya ni upi. Kanuni ya siasa ya ujamaa na kujitegemea inatoa mwongozo katika hili.
Hata hivyo, ni maoni yangu kwamba, JPM haonekani kuizingatia kanuni hii. Kwa mfano, JPM anaharibu umantiki wa kanuni hii, pale anapoongea maneno haya:
"Panapotokea janga kama vile tetemeko, jukumu la serikali siyo kujenga nyumba za wananchi. Asitokee mtu kuwadanganya kwamba serikali itagawa chakula, kwani serikali haina shamba.”
Kupitia maneno haya, na kadiri kanuni ya siasa ya ujamaa na kujitegemea inavyohusika, napendekeza kwamba, Rais ameonyesha dhamira ya kuvunja Katiba aliyoapa kuilinda.
Kwa ujumla, katika eneo hili la kisiasa, bado JPM anapwaya sana. Hivyo, Namshauri JPM afanye hima kutafuta mshauri wa kisiasa.
Najua fika kuwa, Askofu Dk. Methodius Kilaini ni mtaalam sana katika eneo hilo. Juzi nilimwona JPM akibusu pete yake ya Kiaskofu.
Hivyo, hapa pia namwomba Askofu Kilaini kumnong'oneza JPM juu ya umuhimu wa kuheshimu kanuni ya siasa ya ujamaa na kujitegema, kwa maana ya “the principle of subsidiarity.”
Mwaka 1931, Papa Pius XI, kupiti waraka uitwao “Quadragesimo Anno,” aliongela “Kanuni ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea” kama ifuatavyo:
“It is a fundamental principle of social philosophy, fixed and unchangeable, that one should not withdraw from individuals and commit to the community what they can accomplish by their own enterprise and industry. So, too, it is an injustice and at the same time a grave evil and a disturbance to right order to transfer to the larger and higher collectivity functions which can be performed and provided for by lesser and subordinate bodies. Inasmuch as every social activity should, by its very nature, prove a help to members of the body social, it should never destroy or absorb them.”
Namtakia utendaji mwema JPM.
Deusdedith Jovin Kahangwa
January 04, 2017.
===========================
Chanzo: www.facebook.com/deus.jovin