Askofu Kilaini achemsha kwa ushauri huu!

hapo juu tuko ukurasa mmoja Mkuu...............

Ukiwa na system inayofanaya kazi yake inavyotakiwa.......haya maneno ya huyu Ndugu Kilaini wala yasingekuwa na maana........

....sidhani kama Kilaini kakurupuka tu........he has seen and experienced....who knows.......the ball is with the Government now.........let them take a note!

Hiyo ''experience'' ameipata baada ya Waziri Mkulo kutangaza kuwatoza kodi? Kilichomsukuma kutoa tamko sasa hivi na siyo kabla kiko wazi tu.
 
Tutajuaje kama kanisa flani ni la ukweli na kanisa flani ni la uongo? Kwa idadi ya waumini?

Hapa hoja kubwa kwa upande wa serikali si kujua kanisa lipi ni la kweli na lipi ni uwongo.....! Kama zilivyo taasisi nyigine inachotakiwa kujua ni je, hayo yanayojiita makanisa yanafuata sheria za nchi? Kama ndiyo hakuna shida...shida zinaanza pale ambapo makanisa hayo yanaanza kukiuka taratibu zilizopo na kuvunja sheria!
 
Mwanaluguma, hebu nipe link kati ya ''ukibwetere'' na ''idadi ya waumini + kusamehewa kodi". Sioni.

Hajasema habari ya idadi ya waumini. Anachozungumzia hapa na ndicho haswa moyo wa mada ni kuratibu shughuli za haya makanisa yetu ili kujua mwenendo wake unaendana na madhumuni ya kuundwa kwake...(ikiwemo kuhakikisha misamaha ya kodi haitumiki vibaya) Sasa kwa sababu mnazozijua wenyewe mmeamua hii mada kuichukua na kuipeleka 'kusikojulikana' na kuingiza hoja ambazo hazipo.
 
Hiyo ''experience'' ameipata baada ya Waziri Mkulo kutangaza kuwatoza kodi? Kilichomsukuma kutoa tamko sasa hivi na siyo kabla kiko wazi tu.

Ndg unaonekana husomi hata unacholeta hapa jamvini. Hebu soma hii sehemu:

..miaka ya tisini, tatizo hilo lilionekana na serikali iliahidi kushughulikia makanisa hayo, lakini leo serikali inayaandikisha ovyo tu na katika muungano wa makanisa hayamo

Ina maana hili suala limekuwa likifuatiliwa kitambo, na sasa serikali inakumbushwa wajibu wake baada ya kukurupuka na kukimbia wajibu wake wa kuratibu shughuli za makanisa yote na hivo kubaini yapi yanaendeshwa ndivyo sivyo, na kutaka kuya-penalize wote bila ya sababu ya msingi.
 
No. Ni wewe mwenyewe ulibaki square one. Mimi nipo square two. Nasema kwamba matamshi ya Askofu Kilaini kwamba taasisi za kidinii zichujwe wakati wa kuandikishwa yanakinzana na uhuru wa kuabudu unaotolewa na katiba.

Taasisi za dini zinachujwa mazee..hiyo sio option. Sheria inataka hivyo na ndio maana huwezi kuunda kikundi chako kiholela bila kujulikana kwenye mamlaka husika. Ukienda kujiandikisha lazima ukidhi vigezo na huko kama ndiko unakokuita kuchujwa basi hiyo ndo maanake. Sielewi unachopinga hapa maana kila kitu kiko wazi, ndoa huandikishwa kuwa halali, bendi za muziki zinaandikishwa BASATA, makampuni BRELA and the list goes on and on. Hili halikwepeki.
 
By the way kudhibiti au tuseme ku-monitor taasisi zote ikiwemo dini zote ni kazi ya serikali. Hivi mnakumbuka kilichotokea Uganda mwaka 2000 wakati Kibwetere alivyoteketeza watu na kutoweka. Serikali ya Uganda ilijuta sana kwa hili maana haiku-monitor mwenendo wa makanisa. Mnakumbuka sakata la Gayana miaka ya 1970? Hakuna Demokrasia isiyo na kikomo.

Mwaka jana huko USA wachungaji wa makanisa ya kilokole wamewekwa kiti moto na Congress kwa kufuja pesa za waumini wao kwa kuishi kifahari kupindukia na huku wakipewa misamaha ya kodi na serikali? Congress inataka makanisa ya namna hiyo yadhibitiwe vilivyo. Hivyo Kilaini hayuko mbali na hili.
 
Ushauri wa Kilaini ni mbovu haukuzingatia ukomavu wa kiuongozi kwa kiongozi mkuu kama yeye
1.Kwa kiongozi aliyekomaa kiungozi ukidai kitu ukapata inabidi unyamaze usiendelee na kidomodomo.Aliomba kodi iondolewe imeondolewa na serikali ilibidi baada ya kutimiziwa alichotaka anyamaze asiendelee na kidomodomo kwa mtu mkomavu kiuongozi.
Totally disagree with you. Yaani Kilaini atulie eti kwa sababu kapewa alichokuwa anaomba? so unataka kuniambia Serikali iliwa blackmail viongozi wa dini wasipanue midomo yao?
Mkuu hizi ni fikra ni za kibinafsi sana...eti ukipewa unachoomba hutakiwi upanue mdomo wako tena? Kwa nini basi unawalaumu viongozi wanapokea rushwa na kuwasaliti wananchi kwa kukaa kimya badala ya kuendelea kuikemea serikali?

2.Utafiti nilioufanya kwa makanisa madogo nchi mbalimbali duniani hukataa kusajiliwa na serikali kwa sababu huamini kuwa Mungu na kaisari (Mtawala) ni vitu viwili tofauti.
Acha kutudanganya hapa mkuu......umefanya utafiti nchi zipi, na makanisa madogo yepi mkuu....tupe hiyo repoti ya utafiti sio blabla mkuu! Eti makanisa hukataa kusajiliwa na serikali......hii itakuwa true endapo nchi hizo zinaendeshwa kwa misingi ya kidini na si nchi kama Tz ambayo serikali yake haiendeshwi kwa misingi ya dini and so kila taasisi inayofanya shughuli yoyote lazima itambuliwa na serikali ili kuweza kuwalinda raia wake!
Na kwa misingi Hiyo ya utofauti wao hulipa kodi zote serikalini kama Yesu alivyowaagiza kuwa mpeni kaisari kilicho chake kaisari (kodi} na mpeni Mungu kilicho chake Mungu (sadaka).Wao hawaigusi serikali na serikali haiwagusi kila mmoja huheshimu mipaka yake.
Hili mbona liko wazi mkuu....nani anabishia hapo?

Sasa serikali ilikuwa inalia ipewe chake wakatoliki hawataki kulipa cha kaisari (kodi) na wanaona fahari kutomlipa kaisari chake (kodi).
Khaam mkuu sasa unazidi hata kama una chuki binafsi na RC this is too much! Mkuu ni ukweli kwamba hili sakata linawahusu wakatoliki tu...na unaongezea ...wanaona fahari kutomlipa kaisari chake....is this true? ndo RC walivyokwambia?

Makanisa mengi madogo kwa taarifa yake Kilaini hayo anayosema yana watu wachache mengi hayana mpango wa kukwepa VAT. hujenga majengo yao bila kuomba misamaha ya kodi kwenye vifaa vya ujenzi na wala hawana mpango wa kuomba VAT iondolewe.

Makanisa mengi yapi si uyataje ili tuyachambue vizuri.......eti hayana mpango wa kuomba VAT iondolewa......iondolewe mara ngapi wakati sheria ilishaondoa na wakiuziwa bidhaa bei huwa VAT exclusive?......eti hawana mpango wa kuomba VAT iondolewe ....iondolewe kutoka wapi tena wakati sheria ilishaiondoa?
Iwe simenti,nondo,baisikeli,magari,vinanda,magitaa n.k huvinunua na VAT zake hivyo hivyo na hawataki kuomba msamaha wa kodi kutokana na imani yao ya kidini kuwa lazima kodi ilipwe kama Yesu ALIVYOAGIZA.

Wewe unaijua vizuri jinsi sheria ya VAT 1997 inavyofanya kazi? Anybody supplying goods or services to the VAT relieved person is not supposed to charge VAT.......religious organisations ni relieved from paying VAT so they are enjoying this benefit kimyakimya.....need we say more on this!

Labda yeye Kilaini na usomi wake atueleze ni kwa mamlaka gani aliyonayo aweza kataa kulipa kodi wakati Yesu mwanzilishi wa kanisa alilipa kodi.

Ebu nionyeshe wapi na lini Kilaini amekataa kulipa kodi na pia niambie mamlaka husika kwa nini hazijamchukulia hatua kwa kufanya hivyo?

Huo unafuu wa kusamehewa kodi kautoa kitabu gani cha biblia au kaupata wapi?

Mkuu nchi hii haiendeshwi kwa vifungu vya biblia inaendeshwa na sheria za nchi mkuu. Mbona hujiulizi wa kati huo huo, kifungu gani kinasema hawa kina Kilaini kutoa huduma za kijamii chini ya Caritas, mahospitali, mashule, orphanage centres, miradi ya maji kwa wananchi wote.....and they have been very successiful on this side. Kutoa huduma za kijamii ni jukumuu la na Kanisa? wanatekeleza hayo majukumu kwa niaba ya serikali kwa ujira upi sasa......please try to think out of the box...sio bible bible tu mkuu!

.......yeye kilaini na papa benedicto ni akina nani wasilipe kodi?
Eeeh mkuu...kweli umedata....nilifikiri utaishia kwa Kilaini.....sasa Benedict anatuhusu nini kny mjadala huu hapa....kama sio chuki binafsi na RC? Yaani umeshidwa japo uwataje, KKKT,Anglican, Mashekhe waliokutana na PM pale Dodoma na kukubaliana kudatilisha uamuzi wa kuondoa misamaha, ukamtaje Pope.....kweli RC inakuudhi mchungaji!

Kanisa linalokiuka hata maagizo ya Bwana wao la kutaka walipe kodi na halitaki ni hatari.
Wewe kama sio RC unamjua bwana wao alisema nini, unaijua misingi ya RC wewe kama sio muumini wake? Acha kupayuka ndugu yangu huijui RC hata kidogo.....wivu tu.

BWT: Unakaribushwa kuwa muumini wa RC if you like mkuu.

Napendekeza kanisa katoliki lifutiwe usajili au likubali kulipa kodi kama Yesu alivyoagiza ili liendelee kutambuliwa kama kanisa na si genge la maharamia wakwepa kodi ya VAT waliojificha nyuma chini ya altare ya kanisa ya kugawia sakramenti.

Acha mnkari mkuu, usajili wa RC Tanzania utafutwa si kwa shinikizo lako bali tu kama itagundulika kuwa linakiuka sheria na taratibu za nchi. Lakini ni kuhakikishie kama kilio chako ni kuua ukatoliki...ha!ha!ha! ukatoliki ni imani ya watu ambayo imekuwepo miaka nenda rudi.....so sisi tutapita ukatoliki will be there to stand kama zilivyo imani nyingine!

Unaita RC ni genge la maharamia....is this true kweli mkuu?

Kushambulia makanisa madogo kayaonea na mimi kama mpiganaji wa porini AMBAYE NI SAUTI KWA WASIO NA SAUTI nasema hapana.
Narudia tena...ukirejea tundiko la Cynic Kilaini alitoa tu mfano ....na hakusema eti makanisa yote madogo yasisajiliwe ndugu yangu
Hongereni.Nyie mtaenda huko mnakoita mbinguni na Kilaini na wenzie wataenda gizani jehanamu kwenye kona yenye moto mkali siku ya kiyama kwa kukataa kumpa kilicho chake kaisari(VAT) kama Yesu alivyoagiza.
Heee..! Netanyahu kesha kuwa Hakimu mwandamizi wa sir GOD....? yaani tayari unauwezo wa kujua nani na nani wataenda heaven .....please if you don't mind advise mi taenda upande upi?.....i guess kule uliko mpeleka Kilaini sio?

Kilaini alipaswa ajue kuwa Kutolipa VAT siyo kitu cha kuchekelea kwa makanisa yote kama ilivyo kwa Lutheran,Angilikana,katoliki na hicho kinachoitwa Baraza la makanisa ya wapentekoste cha akina Askofu Mwasota

Heh...kumbe na wengine wapo?

Kwa makanisa mengi madogo kukataa kukataa kulipa kodi kama VAT ni upotofu wa kiimani.Na ndio maana waliamua KUJITENGA NA kuanzisha yao yenye waumini wachache lakini wenye nidhamu ya hali ya juu ya kulipa kodi zikiwemo za VAT wakipinga mfumo wa kishetani ndani ya makanisa makubwa yaendayo kinyume na Yesu alivyoagiza.
Taja hayo makanisa matakatifu mkuu.....mbona unauza chai tu?
 
Totally disagree with you. Yaani Kilaini atulie eti kwa sababu kapewa alichokuwa anaomba? so unataka kuniambia Serikali iliwa blackmail viongozi wa dini wasipanue midomo yao?
Mkuu hizi ni fikra ni za kibinafsi sana...eti ukipewa unachoomba hutakiwi upanue mdomo wako tena? Kwa nini basi unawalaumu viongozi wanapokea rushwa na kuwasaliti wananchi kwa kukaa kimya badala ya kuendelea kuikemea serikali?

Acha kutudanganya hapa mkuu......umefanya utafiti nchi zipi, na makanisa madogo yepi mkuu....tupe hiyo repoti ya utafiti sio blabla mkuu! Eti makanisa hukataa kusajiliwa na serikali......hii itakuwa true endapo nchi hizo zinaendeshwa kwa misingi ya kidini na si nchi kama Tz ambayo serikali yake haiendeshwi kwa misingi ya dini and so kila taasisi inayofanya shughuli yoyote lazima itambuliwa na serikali ili kuweza kuwalinda raia wake!

Hili mbona liko wazi mkuu....nani anabishia hapo?

Khaam mkuu sasa unazidi hata kama una chuki binafsi na RC this is too much! Mkuu ni ukweli kwamba hili sakata linawahusu wakatoliki tu...na unaongezea ...wanaona fahari kutomlipa kaisari chake....is this true? ndo RC walivyokwambia?

Makanisa mengi yapi si uyataje ili tuyachambue vizuri.......eti hayana mpango wa kuomba VAT iondolewa......iondolewe mara ngapi wakati sheria ilishaondoa na wakiuziwa bidhaa bei huwa VAT exclusive?......eti hawana mpango wa kuomba VAT iondolewe ....iondolewe kutoka wapi tena wakati sheria ilishaiondoa?

Wewe unaijua vizuri jinsi sheria ya VAT 1997 inavyofanya kazi? Anybody supplying goods or services to the VAT relieved person is not supposed to charge VAT.......religious organisations ni relieved from paying VAT so they are enjoying this benefit kimyakimya.....need we say more on this!

Ebu nionyeshe wapi na lini Kilaini amekataa kulipa kodi na pia niambie mamlaka husika kwa nini hazijamchukulia hatua kwa kufanya hivyo?

Mkuu nchi hii haiendeshwi kwa vifungu vya biblia inaendeshwa na sheria za nchi mkuu. Mbona hujiulizi wa kati huo huo, kifungu gani kinasema hawa kina Kilaini kutoa huduma za kijamii chini ya Caritas, mahospitali, mashule, orphanage centres, miradi ya maji kwa wananchi wote.....and they have been very successiful on this side. Kutoa huduma za kijamii ni jukumuu la na Kanisa? wanatekeleza hayo majukumu kwa niaba ya serikali kwa ujira upi sasa......please try to think out of the box...sio bible bible tu mkuu!

Eeeh mkuu...kweli umedata....nilifikiri utaishia kwa Kilaini.....sasa Benedict anatuhusu nini kny mjadala huu hapa....kama sio chuki binafsi na RC? Yaani umeshidwa japo uwataje, KKKT,Anglican, Mashekhe waliokutana na PM pale Dodoma na kukubaliana kudatilisha uamuzi wa kuondoa misamaha, ukamtaje Pope.....kweli RC inakuudhi mchungaji!

Wewe kama sio RC unamjua bwana wao alisema nini, unaijua misingi ya RC wewe kama sio muumini wake? Acha kupayuka ndugu yangu huijui RC hata kidogo.....wivu tu.

BWT: Unakaribushwa kuwa muumini wa RC if you like mkuu.

Acha mnkari mkuu, usajili wa RC Tanzania utafutwa si kwa shinikizo lako bali tu kama itagundulika kuwa linakiuka sheria na taratibu za nchi. Lakini ni kuhakikishie kama kilio chako ni kuua ukatoliki...ha!ha!ha! ukatoliki ni imani ya watu ambayo imekuwepo miaka nenda rudi.....so sisi tutapita ukatoliki will be there to stand kama zilivyo imani nyingine!

Unaita RC ni genge la maharamia....is this true kweli mkuu?

Narudia tena...ukirejea tundiko la Cynic Kilaini alitoa tu mfano ....na hakusema eti makanisa yote madogo yasisajiliwe ndugu yangu

Heee..! Netanyahu kesha kuwa Hakimu mwandamizi wa sir GOD....? yaani tayari unauwezo wa kujua nani na nani wataenda heaven .....please if you don't mind advise mi taenda upande upi?.....i guess kule uliko mpeleka Kilaini sio?

Heh...kumbe na wengine wapo?

Taja hayo makanisa matakatifu mkuu.....mbona unauza chai tu?
Mheshimiwa Next Level wacha nikujibu kwa ufupi maeneo machache.

Mpiganaji yeyote duniani kama mimi ukimuuliza kuhusu conflict origin atakuambia source ni ulevi wa ukubwa na kutokujali serious concerns za minority kwa wale walioko kwenye position kubwa wawe serikalini,bungeni,kanisani.vyama vya siasa,machifu,katika familia,maofisini n.k.

Kanisa katoliki ni moja ya institutions ambazo ni walevi wa ukubwa sana na hawajali concerns za minority believers wa faith nyingine.Kutokana na ulevi huo wa ukubwa walisahau na kudharau concerns za minority kama za akina Martin luther na reformers wengine na kuwaona kama wahuni na vikundi vidogo vya watu wachache ambavyo havifai hata kuitwa kanisa vya vichochoroni visivyo na wafuasi wa maana bali wahuni wa vichochoroni na malofa na wemye akili finyu zisizojua mambo.Matokeo yake ukatoliki uliporomoshwa na hao minority hadi ukatoliki ukapoteza ufalme wake kwenye baadhi ya mataifa ikiwemo uingereza,ujerumani,n.k Na sasa hivi hao waliowaona kama minority ni tishio kwa ukatoliki kila kona duniani.

Naona Kilaini anaendeleza kosa lile lile la wajenzi wa ukatoliki wa mwanzo ndio maana na mimi nikiwa msomi niliona nimparamie nimwambie kakosea.Hao anaowaona WATU mia mbili kama sio kitu akae chonjo mapinduzi yote makubwa duniani na vita zote kubwa huanzishwa na minority wahuni wa vichochoroni na sio majority waliolewa ukubwa na dharau kwa minority waishio kwenye majumba ya kifahari.Martin Luther na reformers wengine walianza peke yao baadaye wakaungwa mkono na minority baadaye majority wakawaona minority wana hoja wakawaunga mkono wakauvurumisha ukatoliki nje ya nchi zao kama wanavyovurumisha kibaka. wakatoliki wakawa minority na wao minority wakawa majority.Kilaini Asidharau minority na kuwaona si kitu.Statement yake ya mia mbili tu ni ya dharau mno kwa kiongozi wa kidini kama yeye.Hivi parokia yake kule kijini kwake ina waumini wangapi? je inastahili kuitwa kanisa kama ina watu mia mbili au haistahili?

Pili kuhusu kuwa makanisa yote hufaidika na VAT si kweli Next level umedanganya.Sheria ya VAT sio automatic.Mfano ukiagiza mali au chochote cha kanisa nje ya nchi unatakiwa kulipa ushuru na kodi mbali mbali na ukinunua ndani ya nchi unatakiwa ulipe VAT. sasa ili mfanyabiashara akuuzie bila VAT inabidi uonyeshe makaratasi ya usajili na vibali vinavyokuruhusu wewe usilipe VAT ambavyo hutolewa na serikali baada ya wewe mwenye kadini kako mtumba toka ulaya kwenda serikalini kujikomba wakupe hayo makaratasi ya usajili na ya kusamehewa kodi za nguo mitumba,dawa mitumba,magari mitumba na nguo Za kusalishia mitumba ikiwemo majoho mitumba ya maaskofu toka ulaya visamehewe kodi zote.ukiwa huna hayo makaratasi husamehewi uwe unaagiza vitu nje ya nchi au unanunua ndani ya nchi.Kwa yale makanisa ambayo hayataki kusajiliwa na serikali kwa kuwa huamini kuwa kuabudu ni suala la mtu binafsi na si serikali na huamini kuwa mungu huwezi kumsajili serikalini hao ndio usiseme hununua vitu vyote na VAT na hufurahi sana kununua na VAT.

Sasa makanisa mengi madogo kwa kujua kuwa kulipa kodi ni wajibu WAO KIBIBLIA hununua bila kuonyesha hiyo mikaratasi ya misamaha na usajili hata kama wanayo hivyo kununua bidhaa zenye VAT.

Kwa kawaida Huuziwi bidhaa bila VAT kwa kutamka tu kuwa wewe ni dini au kanisa vinginevyo kila mtu angeenda dukani kusema anaenda kununua kitu cha kanisa.

Kuna swali umeuliza kuwa makanisa yanapotoa huduma za jamii kama hospitali,shule n.k huwa nani anawalipa.Nikujibu hivi sadaka wanazopata kanisani huwa wanazitumia kwa kazi gani kama hawawezi kulipia hao wanaohudumu kanisani,hospitalini na kwenye mashule yao? Kazi ya hizo sadaka za mabilioni wanazokusanya ni nini? Pia huduma hizo huwa sio bure ni za kulipia kama hizo shule usiseme ada zao mtoto wa mkulima haziwezi kabisa ni za kusomesha watoto wa matajiri wa mijini kaulize ada ya shule za ST FRANCIS,KIFUNGILO,ST MARIAN,ST.MARIA GOLETTI,KANDOTO,NA SHULE ZOTE ZA MISHENI ZILIZOBEBA MAJINA YA WATAKATIFU WAKATI SI TAKATIFU KWA KUTOZA ADA KUBWA zilizozagaa kila kona ya nchi UONE ADA ZAKE uone kama ada hizo zatosha kulipa hao wanaoendesha shule au la.Ada za hizo shule za saint wha what ni kubwa kuliko shule za wafanyabiashara binafsi na ni kuliko za serikali.Wangekuwa wanalipisha ada inayolingana na ya shule za serikali ungesema wasamehewe kodi walau ya VAT na hata mimi ningeomba hata ruzuku wapewe lakini hawana huruma shule za watakatifu za wakatoliki ada ni kubwa inatisha kuliko ada inayotozwa na shule binafsi za waabudu mashetani na wanga.Shule za watakatifu za wakatoliki hazijali kabisa mtoto wa mkulima maskini wa tanzania bali zinajali watoto wa matajiri wa mijini ambao ndio waweza mudu hizo gharama za ada na usafiri wa mabasi maalumu ya kupeleka na kurudisha wanafunzi waendapo na kurudi shule.Faida zinazopatikana kwenye hizo ada hutumika kwa kitu gani kama haziwezi kulipia mishahara ya mapadri,wahudumu wa shule na hospitali na huduma zingine za jamii? Vyuo vyao ndio usiseme ada ni za juu kuliko vyuo vya serikali huduma gani hiyo kama siyo bishara tu kama zingine?

Nchi huendeshwa na katiba ni kweli lakini dini huendeshwa na kitabu cha dini.Kuhusu kusema Wakatoliki wanakiuka misingi ya dini yao na maagizo ya mwanzilishi wa ukatoliki hili nasimamia na siombi msamaha.Kila dini ina mwazilishi na ndiye huwa nguzo ya hiyo dini.Na dini ili isione imekuja kutapeli mtu duniani lazima ifuate maagizo ya mwanzilishi wake.Dini ya kikatoliki mwanzilishi wake Ni yesu na mitume wake kumi na mbili.Yesu mwanzilishi wa katoliki alilipa kodi na aliagiza wafuasi wake walipe kodi.Sasa Kanisa katoliki kama halilipi kodi je ni wafuasi wa mwanzilishi yesu au ni matapeli waliokuja tanzania kwa jina la yesu ili wakwepe kodi ya VAT? Dini isiyofuata maagizo ya mwazilishi wake ni matapeli.Wanatumia dini kuibia watu au kuwanyima watu kilicho haki yao.Kanisa katoliki Tanzania kukataa kulipa VAT na kuivalia njuga serikali ni kuitapeli na kuionea serikali kutumia ujanja na vitisho ili wakwepe VAT kwa jina la YESU wakati Yesu hataki watu wakwepe kulipa VAT kwa jina lake.Mwanzilishi wao aliagiza walipe kodi ilibidi walipe.kanisa au dini yoyote huendeshwa na maagizo ya mwanzilishi hili la kikatoliki Tanzania halina utii kwa kaisari wala kwa mwanzilishi ndio maana nikapendekeza lifutwe maana halifai duniani anakoishi kaisari kwani halimlipi VAT na wala halifai mbinguni aliko mwanzilishi wake aliyeagiza lilipe kodi kwa Kaisari Kikwete maana halimtii hivyo hata likifutwa hakuna laana yoyote toka duniani wala mbinguni, kaisari atafurahi na Yesu atafurahi kuwa kanisa jeuri lisilotii mafundisho yake haliko tena duniani kuendelea kumuudhi kwa kukwepa kodi alizoagiza zilipwe
 
Hapa umepiga ikulu, ila subira sasa wenyewe waje!
 
Ndugu unasema kweli juu ya mambo ya ulipaji kodi, lakini kuna jambo moja unalojisahau: na wakati bajeti zinasomwa jamani tuwe makini kuangalia comments zinazotolewa na wataalam wa mambo ya fedha na washauri wa serikali juu ya mambo yanayohusu bajeti na kodi za kila aina.
Baada ya bajeti kusomwa, kuna tax manager mmoja wa PriceWatehouse Coopers Tanzania aliandika swala juu ya mada hii. Iko hivi:
Sababu ya Serikali kukusanya kodi kwa namna yoyote na katika vyombo vyovyote ni ili iweze kutumia fedha hizo kuleta huduma katika jamii. Kila Mtanzania anafahamu namna ambavyo madehebu ya kidini yalivyosaidia serikali kuleta huduma, na pia huduma nyingi bado zinatolewa na madhehebu ya kidini karibu asilimia 45 ya huduma za kimaendeleo, waweza kuzitaja tu hapa, mashule, mahospital, vituo vya mayatima, vituo vya ufundi stadi na mengine labda unayafahamu zaidi. Wakati madhehebu mbalimbali ya kidini yanapata msamaha wa kodi, ni kwa sababu vifaa vinavyoingizwa vinaenda moja kwa moja kutumika katika mambo hayo yaliyotajwa.
Tunaposema kwamba madhehebu ya kidini yalipe kodi, (na hii sio kwa Kanisa Katoliki tu ndugu yangu kwa sababu, baada ya muda kidogo, mashehe wataongea, wachungaji wataongea pia kuhusu swala hili, ni kwa vile tu Kilaini ameanza kuongea, lakini wote walikuwa wanapata msamaha wa kodi). Serikali inaposema walipe Kodi, ina maana kwamba serikali sasa itachukua mzigo wa kutoa huduma zote hizo ambazo madhehebu ya kidini yalikuwa yakizitoa, kwa sababu wamelipa kodi, na fedha hiyo sasa inapaswa kufanya kazi yake kama jinsi inavyofanya kupitia makanisa na madhehebu mbalimbali.
Kwa bahati mbaya, nafasi hii serikali iliyotoa kwa madhehebu mbalimbali kupata msamaha wa kodi imechezewa na baadhi ya madhehebu, kwa kupitia msamaha huu, wengi wamejiingizia mali za kila aina kwa kupitia makanisa yao kwa faida zao na familia zao, and I guess this is what upsets the government, na hata viongozi wa dini ambao wanafanya juu chini kuona huduma zinawafikia wananchi. Hii ndio sababu iliyomfanya Kilaini akaongea.
Pili: Ningependa mjadala huu uelekezwe zaidi kwenye swala la kodi, kwa sababu ndilo swala linalojadiliwa hapa wala sio ni dini ipi ya kweli au kanisa lipi la kweli au linafuata maandiko, kumbukeni tupo kwenye jamii forum, na inaitwa Home of Great Thinkers! Kama mnataka tujadili swala la maandiko, toeni topic hiyo ili great thinkers waanze kazi ya kuandika..
 
Amepiga ikulu ya wapi? Mambo mengi ni off-topic na pumba zisizohusiana na mada. Ila tulia keti kitako na usipagawe tutakapoanza kujibu hoja kwa hoja, na pumba kwa pumba..
 
You said it all baddy!
 
Amepiga ikulu ya wapi? Mambo mengi ni off-topic na pumba zisizohusiana na mada. Ila tulia keti kitako na usipagawe tutakapoanza kujibu hoja kwa hoja, na pumba kwa pumba..
Kwani na wewe ni miongoni mwao... Au kimbele mbele kimekushika!?
 
Haya misamaha ndo hiyo imesharudishwa ya nini kuendelea kurumbana? Nafikiri kila mtu aamini anavyoamini, pia kutoka kanisa moja kwenda jingine ni uamuzi wa mtu mwenyewe wala mtu mwingine hana mamlaka ya kumuingilia. Achana na waumini 200 kuna makanisa yana waumini kuanzia 3 lakini wanaendelea kukua siku hadi siku hata watafika maelfu.

I think you are missing the point. Swala si kurudisha misamaha ya kodi. Swala ni nini kilipelekea mpaka serikali ikatoa misamaha hii kwa dini . nk. Kama hakuna ufumbuzi wa tatizo hili huko mbeleni serikali itaja toa tena. Ndio maana Askofu Kilaini anaitaka Serkali iwe makini na hao makajanja katika kuangalia "who is genuine and honest and who is not" Nazi moja au mbili mbovu zisiharibu uzuri wa nazi zilizo nzima. Kukua au kutokuwa sio issue, swala ni kufuata utaratibu. Mnakumbuka yaliyotokea Uganda 2000? Jina la Kibwetere bado mnalikumbuka? Ndio makajanja anayosema Askofu Kilaini.
 
Ushauri wa Kilaini ni mbovu haukuzingatia ukomavu wa kiuongozi kwa kiongozi mkuu kama yeye kwa sababu zifuatazo:

1.Kwa kiongozi aliyekomaa kiungozi ukidai kitu ukapata inabidi unyamaze usiendelee na kidomodomo.Aliomba kodi iondolewe imeondolewa na serikali ilibidi baada ya kutimiziwa alichotaka anyamaze asiendelee na kidomodomo kwa mtu mkomavu kiuongozi.

Salale! This is a fallacy. Inaonekana huelewi tatizo ktk dimension zake. Tukumbushane tu kuwa hii ishu inahusu ukwepaji kodi kwa jina la Mungu. Hii si tu inaleta madhara kwa mapato ya serikali bali pia inaleta picha mbaya kwa makanisa yote na kulitweza jina la Mungu kwa namna moja au nyingine. Baada ya serikali kurudisha misamaha ya kodi bila kusema itachukua hatua gani , ni haki kwa mtu aliyeliona tatizo kuzungumza kama alivyofanya Kilaini. Sielewi unawezaje kushindwa kuliona hili. Sielewi ukomavu unaouongelea ni ukomavu gani huenda labda unayo definition yako ya neno ukomavu na kidomodomo..zile zetu standard tunaona hazi-apply hapa
 
Netanyahu said:
2.Utafiti nilioufanya kwa makanisa madogo nchi mbalimbali duniani hukataa kusajiliwa na serikali kwa sababu huamini kuwa Mungu na kaisari (Mtawala) ni vitu viwili tofauti.Na kwa misingi Hiyo ya utofauti wao hulipa kodi zote serikalini kama Yesu alivyowaagiza kuwa mpeni kaisari kilicho chake kaisari (kodi} na mpeni Mungu kilicho chake Mungu (sadaka).Wao hawaigusi serikali na serikali haiwagusi kila mmoja huheshimu mipaka yake.

Mazee ingependeza ungeleta huo utafiti na huko ulikofanyika ili tuujue na tuufanyie kazi kitaalamu. Suala la kulipa kodi au kutolipa ni makubalino na masikilizano kama taifa na kuona nini kifanyike kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa taifa husika. Kama Tanzania tumeona utaratibu wa kusamehe kodi ni mzuri na unaifaa jamii yetu hakuna ubaya na wala si dhambi kuendelea kutumika. Hivyo hoja kuwa kwa kuwa nchi X makanisa hulipa kodi zote haimaanishi utaratibu huo utaleta matunda hapa Tanzania. Ni vyema tukajua kila nchi ina mazingira tofauti, huduma za kijamii tofauti, na vipato vinatofautiana..kuna mambo mengi ya kuzingatia..

Mwisho, kwa kumalizia hii hoja, ule mfano wa Bible haumaanishi kumpa Kaisari yaliyo ya Kaisari na Mungu yaliyo ya Mungu haulengi kwenye mambo ya pesa kama unavyo-suggest. Ule msemo ni wa kiroho zaidi na kama wewe sio mmojawapo wa walioamini ukaacha kupotosha maana inayokutikana mle.
 
Netanyahu said:
Sasa serikali ilikuwa inalia ipewe chake wakatoliki hawataki kulipa cha kaisari (kodi) na wanaona fahari kutomlipa kaisari chake (kodi). Makanisa mengi madogo kwa taarifa yake Kilaini hayo anayosema yana watu wachache mengi hayana mpango wa kukwepa VAT. hujenga majengo yao bila kuomba misamaha ya kodi kwenye vifaa vya ujenzi na wala hawana mpango wa kuomba VAT iondolewe.Iwe simenti,nondo,baisikeli,magari,vinanda,magitaa n.k huvinunua na VAT zake hivyo hivyo na hawataki kuomba msamaha wa kodi kutokana na imani yao ya kidini kuwa lazima kodi ilipwe kama Yesu ALIVYOAGIZA.

Ok, Kilaini amesema kuna makanisa yameandikishwa na serikali na wala hayajajiunga na 'muungano wa makanisa' na serikali pia inalalamika kuwa makanisa yanatumia vibaya misamaha ya kodi, hii ina maana kuwa serikali haiyajui hayo makanisa 'madogo' ambayo mimi nayaita ya 'mfukoni', ila wewe sijui uliyapata wapi na wakakueleza kuwa hawana mpango wa kukwepa VAT...!

Hili suala la kuhusisha idadi ya waumini na kanisa tuliomba hapahapa jamvini tuwekane sana..je sheria za kuandikisha makanisa zinataja idadi ya chini ya waumini ni wangapi ili kuandikishwa ..hili suala halijajibiwa na matokeo yake watu mnarejesha pumba zilezile na kulichosha jamvi kwa maneno mareeeeefu yasiyo na ushahidi..

Pia naona unashupalia sana kuwa eti Yesu alisema tulipe KODI! Lakini kadr unavyozidi kuishupalia hii ishu ndivyo hivyohivyo unavyozidi kuonesha hukuelewa kadhia nzima. Hivi labda nikuulize ni kanisa lipi ambalo Yesu aliagiza lilipe kodi kipindi kile? Maana nijuavyo kanisa limeanza kitambo baada ya Yesu kutoweshwa duniani.

Bible niliyonayo inasema watu wa walimuendea Yesu kumtega akiwa karibu sehemu ya kuabudia na kumuuliza je tulipe kodi kwa serikali ya kikoloni ya Kirumi? Walimuuliza hivo wakitegemea kuwa awajibu msilipe bali lipeni hekaluni ili wampikia jungu kwa mamlaka..From religious point of view tunasoma kila mamlaka imetoka kwa Mungu, na Yesu hapo aliwaambia mlipeni Kaisari kodi kwa kutumia hii premises. Pia aliwaambia mlipeni Mungu yaliyo yake ikiwa na maana yaliyo yake ni vile matakwa ya Kimungu, sio tu kuhusu kulipa zaka na sadaka. Kumpa Mungu yaliyo ya Mungu ni kuishi matakwa yake, na kumpa Kaisari yaliyo yake ni kutii mamlaka zilizopo. Mambo ya pesa ni subset tu. Sasa kwa misingi hii basi suala kuwa Yesu aliagiza tulipe kodi ni wewe umetafsiri na wala sio uhalisia wa mambo.
 
Netanyahu said:
Labda yeye Kilaini na usomi wake atueleze ni kwa mamlaka gani aliyonayo aweza kataa kulipa kodi wakati Yesu mwanzilishi wa kanisa alilipa kodi.Huo unafuu wa kusamehewa kodi kautoa kitabu gani cha biblia au kaupata wapi? Kama Yesu Alilipa kodi na mitume wake walilipa kodi hadi akafanya muujiza wa samaki ili ipatikane pesa ya kulipa kodi yeye kilaini na papa benedicto ni akina nani wasilipe kodi? Kanisa linalokiuka hata maagizo ya Bwana wao la kutaka walipe kodi na halitaki ni hatari.Napendekeza kanisa katoliki lifutiwe usajili au likubali kulipa kodi kama Yesu alivyoagiza ili liendelee kutambuliwa kama kanisa na si genge la maharamia wakwepa kodi ya VAT waliojificha nyuma chini ya altare ya kanisa ya kugawia sakramenti.

Nafikiri kama nilivyoonesha hapo juu, hoja yako kuhusu Yesu aliagiza tulipe kodi is VERY MISPLACED. Ni vyema kama hujui watu wengine wanaamini nini vyema ukaketi kitako ukabakia mtazamaji badala ya kuleta vioja. Yesu alilipa kodi kama Yesu na sio kama kanisa, wafuasi pia walilipa kodi kama wafuasi na sio kama kanisa. Na wakatoliki wote popote walipo kama individuals wanapaswa kulipa kodi zote zilizoamriwa na mamlaka halali, na sijasikia popote ambapo Kanisa Katoliki limewazuia watu kulipa kodi...Sasa mazee kabla hujarukia kitu tanguliza busara mbele.
 
Netanyahu said:
Kushambulia makanisa madogo kayaonea na mimi kama mpiganaji wa porini AMBAYE NI SAUTI KWA WASIO NA SAUTI nasema hapana.Hongereni makanisa madogo ambao huwa mnalipa VAT kwenye bidhaa mnazonunua na ambao hamjawahi kukanyaga serikalini hata kwa mjumbe wa nyumba kumi kujikomba msamehewe kodi ya VAT.Hongereni.Nyie mtaenda huko mnakoita mbinguni na Kilaini na wenzie wataenda gizani jehanamu kwenye kona yenye moto mkali siku ya kiyama kwa kukataa kumpa kilicho chake kaisari(VAT) kama Yesu alivyoagiza.

Mazee umesema kweli wewe ni mpiganaji wa porini. Ukiwa porini sometimes unashindwa kupata enlightment inayopaswa kurutubisha akili ili kuji-update na ulimwenguni huu uendao kwa kasi.

Point yako kuhusu makanisa madogo ni void, kama nilivyokwisha kuonesha hapo juu.

Point yako kuhusu Yesu kuagiza kulipa kodi pia ni void kama nilivyokwisha hap juu.

Natarajia utatoka huko porini ulipo upagane vita ya kujikomboa kifikra.
 
Back
Top Bottom