Makanisa makanjanja yadhibitiwe – Kilaini
Imeandikwa na Maulid Ahmed; Tarehe: 19th June 2009 @ 10:26 Imesomwa na watu: 230; Jumla ya maoni
Baada ya serikali kusitisha mpango wa kuyafutia misamaha ya kodi mashirika ya kidini na asasi zisizo za serikali, viongozi wa kidini wamepongeza hatua hiyo huku Kanisa Katoliki likiitaka kudhibiti makanisa yanayochipukia kama uyoga ambayo yanayotumia vibaya misamaha hiyo.
Sambamba na hilo, Baraza la Maaskofu wa Pentekoste (PCT) limekiri kuwapo tatizo la kuibuka kwa makanisa yanayojiita ya Pentekoste, yanayosadikiwa kutumia vibaya misamaha ya kodi na kueleza kuwa sasa hivi wanaorodhesha wanayoyatambua na kuyawasilisha serikalini ili kuyabana yanayoibuka kiholela.
Akizungumza na gazeti hili jana juu ya maoni ya kusitishwa kwa misamaha hiyo, Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini, alisema yapo makanisa mengi yanayoanzishwa yakiwa na lengo la kuitumia misamaha ya kodi kujitajirisha, hivyo serikali iache kuandikisha ovyo makanisa.
"Unakuta kanisa linaanzishwa likiwa na waumini 200, hilo kanisa gani, wanaanzisha ili wafaidike na misamaha ya kodi…miaka ya tisini, tatizo hilo lilionekana na serikali iliahidi kushughulikia makanisa hayo, lakini leo serikali inayaandikisha ovyo tu na katika muungano wa makanisa hayamo," alionya.
Kwangu mimi huu ni Ushauri wa hovyo na wa hatari kwa nchi iliyojiwekea misingi ya uhuru wa kuabudu kwenye katiba yake. Yaani watz 200 wakitaka kuabudu wasihalalishwe kuabudu! Idadi gani ni halali?
Kwangu mimi huu ni Ushauri wa hovyo na wa hatari kwa nchi iliyojiwekea misingi ya uhuru wa kuabudu kwenye katiba yake. Yaani watz 200 wakitaka kuabudu wasihalalishwe kuabudu! Idadi gani ni halali?
Ni wazi anachosema ni hiki: Wako watu wanadanganya wao ni Kanisa, na kwa hivyo wasamehewe kodi. Hao serikali isiwape msamaha wa kodi.
There are con men who couldn't care less about God, but want tax exemption. So, they start a "Church" for the specific purpose of cheating on taxes. Sasa Kama Baba Askofu anataka wathibitiwe kuna mbaya gani?
Hata RC si wanaweza kuwa makanjanja?
Hawa wanacheza game wasilolijua. Maana waagiza wa vitu vingi toka nje wao kama sikosei ndio namabri one. Na kama kuna wakwepaji kodi wazuri wao nadhani pia ndio nambari wani.
Lakini kwa kuwa si wote hatuwezi kuwahukumu wao wote.
Asianzishe mijadala ya dini ipi ni bora Tanzania na ipi siyo. Nadhani anataka kutupeleka huko.
Wote tuko sawa mbele za Mungu regardless of our purely human made religions.
Thanks Cynic.God bless you!
Nasema kuwa demokrasia ya kweli inaanzia kwenye imani zetu na tunayoyaamini.
Uwezo wa watu wengi kufikiri unaminywa na kuiga na kuabudu bila kufikiri.
Waache watu wafanye watakavyo, kwani kitu gani kinawafanya waondoke huko waliko?If you can satsify human's soul and mind; what makes them to run??
Huyo Gamanywa kawagawa wapentecost kwa misimamo yake juu ya ukimwi, kanisa katoliki ndio nisilisemee linatuhuma nyingi mno haziishi kila kukicha. Lets people dance as they wish, melody of faith is always on and tunes is so different!
Ni wazi anachosema ni hiki: Wako watu wanadanganya wao ni Kanisa, na kwa hivyo wasamehewe kodi. Hao serikali isiwape msamaha wa kodi.
There are con men who couldn't care less about God, but want tax exemption. So, they start a "Church" for the specific purpose of cheating on taxes. Sasa Kama Baba Askofu anataka wathibitiwe kuna mbaya gani?
Mazee mi nadhani wewe ndiye unayestahili kujitazama vizuri na wala si Kilaini. Tatizo lenu wengi wenu mnatangulizaga chuki badala ya judgement na objectivity mnaposikia tu neno kanisa katoliki. Ktk large picture hoja aliyoitoa ni sahihi...ingawa inaweza kuwa ngumu kiutekelezaji lakini way forward kutasaidia kudhibiti ukwepaji kodi na wajanja wanaotumia jina la Kristu kujinufaisha.
Ushauri kama huo angeutoa mtu yeyote .. Kiongozi ya AIC, KKKT, Shehe, Mkulo, Lipumba, wewe, etc. bado ningekuwa na opinion kwamba ni wa ovyo na wa hatari. Nashangaa haya mambo ya chuki dhidi ya Kanisa Katoliki yanakujaje hapa. Angalia nilipoanzisha thread sikutaja Kanisa wala jina la Askofu! Tuangalie haya mambo kwa mapana mkubwa.
In one hand tunatetea uhuru wa kutoa maoni. In another hand tunakuwa watu wa kwanza kuyanyonga maoni ya watu wengine; mi nadhani hii si sahihi! Hayo yalikuwa maoni ya kilaini. Tuheshimu maoni yake hata kama hatukubaliani nayo. Ikiwa lazima tuyajadili kwa nia ya kupata muafaka, si kuonyesha jinsi mtoa maoni alivyokosea.
Hayo ni maoni tu. Method kilaini hana uwezo wa kutunga sheria. Na hii haijawa sheria. Tumwachie Kilaini maoni yake na siye tutoe maoni mbadala badala ya kushambulia mtoa maoni kuwa ametoa maoni ya hatari na hovyo. Kwanza hii authority ya kujudge maoni ya hatari na hovyo tumeitoa wapi?
Maoni ni maoni tu. Kukiwa na haja ya kuyajadili, tuyajadili kwa kuzingatia kuwa ni maoni ya mtu au taasisi moja tu. Ikiwa lengo letu ni kujenga jamii pana inayojari uhuru wa kutoa maoni basi tuwe wa kwanza kuheshimu uwezo wa wengine kutoa maoni. Wakitoa maoni tuyaone ni maoni tuu ikiwa ni lazima tutoe maoni mbadala kwa lengo la kuboresha.
Nadhani tuna ugonjwa wa kutovumilia maoni. Na kama hili ndo tatizo letu, basi hata tusijiulize kwa nini mara nyingi serikali zetu zinaonekana kukosa uvumilivu. Waliomo serikalini ndio hawa hawa tunaoweza kujua maoni ya hovyo na hatari! Ni wazi tutafanya juhudi kuhakikisha maoni ya hovyo na hatari hayaonekani wala kusomwa au kusikika.
Let's be fair. Let's be true to ourselves.
Ni wazi anachosema ni hiki: Wako watu wanadanganya wao ni Kanisa, na kwa hivyo wasamehewe kodi. Hao serikali isiwape msamaha wa kodi.
There are con men who couldn't care less about God, but want tax exemption. So, they start a "Church" for the specific purpose of cheating on taxes. Sasa Kama Baba Askofu anataka wathibitiwe kuna mbaya gani?
Mazee kuongoza kuagiza vifaa nje hailifanyi kanisa katoliki kuwa mkosaji mazee, hizo chuki zenu sizielewi zinakoanzia. Askofu Kilaini ametoa tu wito kwa serikali iangalie kama inaweza kufanya kitu kudhibiti ukwepaji kodi. Hajazungumzia dini ipi ni bora na ipi si bora, msipotoshe habari kwa makusudi.
Ushauri kama huo angeutoa mtu yeyote .. Kiongozi ya AIC, KKKT, Shehe, Mkulo, Lipumba, wewe, etc. bado ningekuwa na opinion kwamba ni wa ovyo na wa hatari. Nashangaa haya mambo ya chuki dhidi ya Kanisa Katoliki yanakujaje hapa. Angalia nilipoanzisha thread sikutaja Kanisa wala jina la Askofu! Tuangalie haya mambo kwa mapana mkubwa.
Basi ataje zipi ni dini kanjanja kama anazijua! nimesema tena na narudia tena kuwa hata RC wanaweza kuwa kanjanja.
Sikiliza mkuu, hili la kukwepa kodi si la dhehebu fulani tu, linahusisha madhehebu mengi katika mapana yake na hata serikali inaelewa kila kitu wala si siri. Hata Mkullo hana haja ya kutajiwa maana anajua kila kitu. Hii aliyosema TBC ilikuwa ni utetezi tu ili tumuonee huruma kwa kuwaondolea hiyo exemption.
Hivyo tusitoane macho mkuu. Hata sisi tumetoa comment juu ya comments za Kilaini simply kama yeye alivyotoa comments zake kwa makanjanja wengine.
More? ninafahamu mapadre, wachungaji na wafanyakazi wa missions mbalimbali ambao magari yao yako registered kanisani lakini yanatumika privately. Need say more?