Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,317
- 38,456
Askofu Zakaria Kakobe ni mmojwapo wa viongozi wa dini ambao mara kwa mara hujihusisha na siasa za nchi yetu. Mwanzoni kabisa alitumia taarifa mbalimbali za mashirika ya Kimataifa kuonesha jinsi mabilioni ya fedha za wananchi yanavyoliwa kupitia mikataba ya Kandarasi mbalimbali.
Lakini Mwaka 2000 Kakobe kwa uwazi aliamua kusimama upande wa aliyekuwa Mgombea Urais kupitia chama cha TLP Augustine Mrema. Kakobe alizunguka sehemu kubwa ya nchi kumkampenia Mrema na ninakumbuka kwamba alikuwa na vyombo vya kisasa kabisa vya kufanyia mikutano.
Kwenye chaguzi zilizofuatia Kakobe alikuwa mpiga kampeni mwenye uelekeo wa kuunga mkono vyama vingine dhidi ya CCM. Nakumbuka ni Askofu pekee aliyeelekeza waumini wa dhehebu lake kusali siku ya Jumamosi ili wapate fursa ya kupiga kura siku ya Jumapili badala ya kwenda Kanisani.
Mara ya Mwisho Kakobe kuwa kwenye habari za kisiasa ni pale alipotoa tamko lake kulalamika kitendo cha viongozi dini toka Madhehebu ya Wapentekoste kututeuliwa kuingia kwenye Bunge la katiba. Tangu aliposema kwamba CCM itapata laana na chama hicho kukutwa na dhahama ya kutokuelewana baina yao. Baada ya hapo Kakobe kakaa kimya. Je ameacha kujihusisha na mambo ya siasa?