Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 894
- 994
๐จ๐๐ฐ๐๐ฃ๐ข๐ฆ๐ ๐ง๐ ๐ฌ๐ข๐๐ฌ๐ ๐ณ๐ ๐๐ค๐๐๐ข๐ฅ๐, ๐๐ง๐๐๐ข๐ค๐ข, ๐๐ณ๐๐ง๐๐ข๐ค๐ข ๐ง๐ ๐๐ข๐ญ๐ข๐ก๐๐๐ ๐ณ๐ ๐๐ฎ๐ฅ๐ข๐ ๐๐ฐ๐ ๐๐๐ข๐๐ ๐ค๐ฐ๐ ๐๐ฐ๐๐ฆ๐ฏ๐ฎ๐ฅ๐ข ๐ฐ๐ ๐๐ข๐ง๐ข.
๐Hivi punde, Kupita ukurasa wake katika mtandao ya YouTube, Mchungaji Josephat Gwajima, kama ilivyo ada yake, amezungumza tena na umma wa Watanzania, hotuba ambayo kwangu binafsi, haileti mwanga kwa Taifa mbeleni, bali kiza kinene kilichojaa udini, ukabila, unafiki na hatari ya kuligawa Taifa.
๐Gwajima amejaribu kuonesha taswira kuwa Taifa lipo njia panda na kwamba CCM itaanguka endapo haitamsikiliza yeye kuelekea Uchaguzi Mkuu. Ameitaja serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa shutuma mbalimbali, ikiwemo madai ya mauaji, utekaji, kufungiwa makanisa na hata kumtaja Tundu Lissu kama mhanga wa dhuluma.
๐Hata hivyo, hoja zake si ngeni kwa masikio ya Watanzania, na kama zilivyo mara nyingi, zimejaa upotoshaji, unafiki wa kisiasa na ajenda binafsi hatarishi kwa mshikamano wa taifa.
๐ด๐๐๐ก๐๐๐๐ง๐ ๐๐ข๐๐๐๐ง๐ โ๐๐๐ ๐๐ค๐๐๐๐๐ ๐บ๐ค๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐. ๐น๐ข๐๐ก๐๐๐ ๐๐๐๐..๐๐๐
Leo hii Gwajima anajitokeza hadharani akilalamikia kufungwa kwa makanisa kana kwamba hili limeanza chini ya Rais Samia.??
Ukweli ni kuwa makanisa yalifungwa hata wakati wa Rais John Pombe Magufuli, kipindi ambacho Gwajima alikuwa Mbunge wa CCM kupitia Jimbo la Kawe;
โช๏ธKanisa la EAGT Arusha Road Dodoma lilifungwa. โช๏ธAssemblies of God Morogoro ilisitisha ibada kwa maelekezo ya serikali, na makanisa kadhaa Dar es Salaam yalifungwa kwa sababu za kisheria na kiutawala.
๐Gwajima hakusema chochote wakati huo, hakuandaa hotuba ya YouTube, hakuandamana na hakuwa msemaji wa ukristo kama anavyojionyesha leo. Ukimya huo unathibitisha kuwa msimamo wake wa sasa si wa kweli bali ni silaha ya kisiasa dhidi ya Rais Samia.
๐Kuhusu Tundu Lissu, Gwajima anataka umma uamini kuwa Lissu anaonewa leo.
๐Lakini tukio la kupigwa risasi kwa Lissu lilitokea mwaka 2017, wakati wa utawala wa Magufuli, na Gwajima akiwa ndani ya Bunge. Hakuinua sauti wala kuonyesha mshikamano wa kibinadamu.
๐Leo anajifanya mtetezi wa Lissu si kwa sababu ana uchungu wa dhati, bali kwa sababu jina hilo ni rahisi kulitumia kama nyenzo ya kumshambulia Rais Samia.
๐Isitoshe, kauli yake kwamba wakristo nchi nzima wasimpigie kura Rais Samia ni sumu ya mbaya kwa mshikamano wa Taifa. Misingi ya nchi yetu imejengwa juu ya mshikamano wa umoja, na historia ya dunia imejaa mifano ya mataifa yaliyoporomoka kutokana na siasa za udini, kama vile Sudan na Nigeria, ambako uchaguzi unageuka kuwa uwanja wa kugombania imani badala ya sera na maendeleo.
๐Hoja ya Gwajima inaibua hofu kwamba chuki zake zinachochewa na ukweli kuwa Rais Samia ni Muislamu, jambo linaloonyesha wazi nia ya kuingiza mgawanyiko wa kidini kwenye siasa za Tanzania. Hili si jambo la mzaha; ni hatari inayoweza kuharibu amani na mshikamano tulioujenga kwa miongo mingi.
๐Gwajima pia ametumia hoja za marekebisho ya sheria za uchaguzi, akitaka CCM ifanye kile anachokiita โminimal reformsโ ambayo mengi yanabebwa na madai ya CHADEMA ya "No Reform No Election".
๐Ukweli ni kwamba madai haya yalianza zamani, kabla ya Rais Samia kuingia madarakani. Kipindi cha Magufuli, madai haya yalikuwepo lakini Gwajima hakuwahi kuyaunga mkono. Kauli yake ya leo haina uhalisia wa kiitikadi bali inalenga kudhoofisha CCM chini ya uongozi wa Samia.
๐Kwa upande mwingine, hoja yake kwamba CCM iko hatarini kuanguka inapingwa na takwimu na uhalisia wa kisiasa. CCM ina wanachama zaidi ya milioni 13 na mashina zaidi ya laki mbili kote nchini. Ni chama kilichojijenga kwa sera imara, mtandao mpana na historia ya ushindi wa kudumu. Kwa nguvu hii, ushindi wa CCM si swali la kama, bali ni suala la lini.
๐Kama haitoshi, kwanini nimediriki kusema Gwajima ni Mnafiki na muongo, Gwajima mwenyewe amewahi kutamka hadharani kwamba kazi yake ya uchungaji ni kubwa kuliko urais au ubunge, na kwamba hawezi kugombea nafasi hizo.
๐Lakini haikupita muda akajitosa kugombea ubunge na kushinda, akisaidiwa na ukaribu wake wa kikabila na Rais Magufuli. Tukio hili linaonyesha tabia ya kutokuwa na msimamo na mtu anayefuta mkumbo wa kisiasa.
๐Gwajima sio mtu wa kuaminika, historia yake binafsi imejaa tuhuma za kimaadili, ikiwemo madai ya kushiriki ngono na mfuasi wake wa kanisani. Hii ni doa kubwa kwa mtu anayejionyesha kama kiongozi wa kiroho na maadili. Ni unafiki mkubwa kuhubiri uadilifu hadharani huku mwenyewe ukipuuza misingi yake.
๐Hotuba ya Gwajima haijengi taifa. Ni jaribio la kupandikiza chuki za kidini. Tanzania haiwezi kurudi nyuma katika mshikamano na amani yake kwa sababu ya kauli za mtu mmoja anayetanguliza maslahi binafsi mbele ya maslahi ya taifa.
๐Rais Samia Suluhu Hassan na CCM wamesimama imara kwa mshikamano na maridhiano, na kauli za kijinga kama za Gwajima ni kelele za kisiasa zisizo na msingi mbele ya historia na mustakabali wa nchi yetu.