Kisu Cha Ngariba
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 22,135
- 48,821
Mida hii ya saa 12:29 nikiwa katika maandalizi ya mwisho kabisa kuelekea kanisa la Ufufuko na Uzima chini ya askofu baba Josephat Gwajima kwa ibada pia nitakuwa nawamegea mambo kadhaa ambayo askofu Gwajima atataka Tanzania isikie na huku ikumbukwe kabisa akiwa hajasema lolote tokea aachiwe huru.
Stay tuned: JF siku zote unakuwa wa kwanza kupata habari.
....UPDATES....
Kwaya wamemaliza kuimba mzee wa kanisa anawapongeza na kusema "kama Gwajima angeendelea kuwa ndani na wauza madawa kuendelea kutanua mtaani basi hii kwaya leo ingekuwa inamalizia kurekodi album yake pale central"
===========
Askofu Josephat Gwajima amesema akimpeleka Makonda mahakamani, atakuwa amepeleka serikali mahakamani. Hivyo atamshtaki Makonda kwa Rais ili achukue hatua zinazostahili na hatokubali akiendelea kuwa mkuu wa mkoa.
Gwajima amedai watu wasiwalaumu jeshi la polisi kwani na wenyewe wanateswa kama wanavyoteswa wao. Amesema alipoenda polisi amekuta nao wameswekwa ndani kwa amri ya Makonda. Amedai matatizo yote yamesababishwa na 'kiumbe mmoja'.
Amempongeza Rais kwa kumchagua mkurugenzi husika na amemshauri asiache kuamini vijana kwa kuwa kijana mmoja ameharibu.
....Mengineyo....
Gwajima: Lengo la Paul Makonda ni kuchafua majina ya watu kwa sababu anazozijua mwenyewe.
Askofu Gwajima: Askari walipekuwa nyumba yangu chumba hadi chumba lakini hawakukuta kitu chochote.
Askofu Gwajima: Mimi nitawaambia kitu, msilaumu Polisi wala Ofisi ya Rais. Wao hawahusiki na hili ila ni kiumbe mmoja tu ameibuka katikati.
Askofu Gwajima: Waliniambia wakanipime kwa Mkemia na walinipima kwa uwazi kabisa. Niliwaambia hata wakikuta pombe wasema ni dawa za kulevya.
Askofu Gwajima: Polisi nao wanateswa kama tunavyoteswa sisi. Wanaambiwa wakapekuwe nyumba yangu japo wanajua hamna kitu ila inabidi waende.
Askofu Gwajima: Baada ya kukosa walichokuwa wanatafuta nyumbani kwangu tukarudi polisi usiku ule ule kuendelee na mahojiano.
Askofu Gwajima: Kamanda Sirro akaniuliza kwa nini nimewekwa kwenye orodha hiyo, nikamwambia ni chuki tu za mtu aliyekaa kwenye kiti chake.
Askofu Gwajima: Sijawahi kuvuta sigari, kunywa pombe wala kwenda disko tangu nimezaliwa mimi.
Gwajima: Chumba nilichowekwa polisi nilikuwa mimi na manji. Nikasema 'kumbe na mimi nina pesa kiasi hiki hadi nawekwa na huyu?'
Askofu Gwajima: Kwanini kina Manji wao hadi leo hawajafanyiwa kama nilivyofanyiwa mimi ili nao watoke mule ndani?
Askofu Gwajima: Manji ana kampuni 23, na ameajiri watu zaidi ya 5000. Unashindwaje kumpelekea hati ya kumuita umhoji kabla ya kumtangaza?
Askofu Gwajima: Baada ya kukosa madawa, utalisafishaje jina langu nililolijenga kwa jasho kubwa kwa miaka 29?
========
Kilichojiri Kanisani kwa Gwajima ibadani
Mahubiri ya Gwajima
==========
“RAMANI YA UBAYA IMEKOMESHWA”
Unapoona mtu anataka kujenga nyumba lazima wazo la kujenga linaze, anampa wazo mchora ramani kwamba nataka nyumba yangu iwe na jiko, stoo, sehemu ya kufulia, shemu ya ebule iwe hivi n.k, halafu mchora ramani atakwenda sehemu ya itakapojengwa nyumba atapaangalia jua linachomozaje na linazamaze, baadaye anachoa ramani na baada ya ile ramani kupitishwa inapelekwa kwa mhandisi anatoa mawazo ake kwamba sehemu hii iwekwe nondo za cm kadhaa , halafu inapelekwa kwa mjenzi ambaye anaanza kujenga sawasawa na ramani aliyochorewa akiwa pamoja na consultant anayesimamia ujenzi ili vipimo na vyifaa vilivyopangwa kutumika vinatumika kama ilivyokusudiwa na baadaye nyumba inatimia.
RAMANI YA UBAYA
Kwenye ramani ya Ubaya inaanza kwa mfano huu huu, bahati nzuri huwa nafundisha maisha niliyofundisha, kwahiyo ubaya unapochorwa baadaye ubaya huu unazaa matunda.
Kwenye Biblia zamani alikuwepo Mfalme anaitwa Ahabu ambaye alioa mke wake aitwaye Yezabeli ambaye hakuwa mtu mzuri, wakati ule siku moja mfalme alipita kwenye njia karibu na nyumbani kwake akaona shamba zuri limestawi linapaliliwa vizuri na lina mbolea ambalo ni la mtumishi wa Mungu aitwaye Naboth, Ahabu alikuwa karibu na hilo shamba na watu walilisifia sana.
Mfalme huyu alikuwa na wivu juu ya lile shamba akitaka liwe lake, akaamua kumwendea Naboth ili amuuzie shamba hilo lakini Naboth akataa akisema mali aliyopewa ya urithi Mungu aepushe mbali jambo hili haliwezekani akakataa kabisa, hata kabla Mfalme hajasema bei atakayo mpatia Naboth aligoma kuliuza. Mfalme alipokataliwa alienda nyumbani kwake kwa huzuni nyingi na mke wake Yezabeli akamwona na kumwambia atalishughulikia jambo hilo yeye atulie alale.
Yezabeli huyo aliamua kuandika waraka akawaambia watu watafute mashahidi watatu waongo waende wakamsingizie Naboth amemtukana Mfalme na Mungu (kwa kawaida kwenye sheria za Israel wakipatikana mashahidi watatu kwenye jambo unapigwa mpaka unakufa) ule mchoro wa Yezabeli mke wa Mfalme ukatimia wale mashahidi wakaenda kutoa ushahidi wa uongo kwa Mtumishi wa Mungu Naboth naye akapigwa kwa mawe akafa.Baadaye mke wa Mfalme akaenda kumwambia Mumewe tayari shamba lipo mkononi mwake ainuke akalitazame.
Mfalme Ahabu akaenda kwenye lile shamba akawa analitembelea na ghafla akatokea mtu mmoja aliyeitwa Eliya mtishibi akaibuka akamwambia Mfalme umemuua mtu ili umiliki shamba, kwasababu hiyo na wewe utakufa kama yeye na damu yako itachuruzika ikilambwa na mbwa kama mtu huyu wa Mungu.
Baadaye ikatoke vita ya kawaida ambayo lengo lake lilikuwa Mfalme afe. Lakini Mfalme kwa vile alijua alishatamkiwa maneno na Nabii Eliya, aliaamua kuwaita manabii nyumbani kwake ili awaulize aende Ramoth gileadi kupigana vita au asiende?, manabii wote walimwambia kwea ee mfalme lakini kulikuwa mmoja alitwaye Sedekia alimwambia Mfalme nenda ukapigane ee mfalme (hata waovu nao huwa wanajifanya wanamtumikia Mungu).
Ila ndani ya moyo wa Mfalme Ahabu, moyo wake ulikua unawasiwasi, akamua kuwaita manabii wengine 400 na wote wakasema kwea ee mfalme, bado mfalme hakuridhika akaamua kuulizia kama kuna nabii mwingine ndipo akaambiwa yupo aitwaye Mikaya lakini hana maneno mazuri sana, mfalme akaamuru aitwe.
Nabii Mikaya akaenda kuongea na Mfalme Ahabu akamwabia na wewe sema neon kwamba niende au nisiende, kwasababu Mikaya aliona manabii wengine wamesema nenda mfalme, yeye naye akasema Mfalme kwea Ramoth Gileadi ukapigane, lakini Mfalme hakuamini Mikaya amemtamkia maneno mazuri, akamwambia nakuapisha kwa jina la Bwana wa Majeshi sema tena, ndipo Nabii Mikaya akasema ukweli wenyewe, akasema tazama niliwaona wana wa Israeli wamekwea Ramoth Gileadi lakini wamepigwa wakatawanyika kama kondoo asiye na mchungaji, baada ya maneno hayo Mfalme akaamuru nabii Mikaya akamatwe akaenda kupigana Ramoth Gileadi kupigana akawaambia wamfunge na kummpa chakula kibaya mpaka atakaporudi, wakati akiyasema hayo Nabii Mikaya na yeye akasema kama utarudi salama basi Mungu hakunituma ila mfalme akaendelea kwenda. (kama lipo jambo Duniani la kuepuka ni kushindana na watu waliotumwa).
“Wale wanaoshindana na bishara yako uliyopewa na Mungu, wanaoshindana na ndoa yako uliyopewa na Mungu, wanaoshindana na familia yako hawatakushinda kwa jina la Yesu” Nabii Mikaya akamwambia Mfalme kama unakwenda kupigana utakufa, Mfalme akaamua kuvaa nguo za chuma badala ya za kifalme. Zamani mtu alikuwa anachaguliwa kuwa mfalme kwa uhodari wake wa kupigana vita na kwenye vita ilikuwa ukiona mtu amevaa mavazi ya dhambarau unakaa mbali kwasababu alikuwa ni Mfalme, ilikua Mfalme na Mfalme walikua wanapigana.
Siku moja Ilitokea mbinguni Mungu aliuliza ninani nimtume aende duniani kumdanganya Ahabu, mbingu nzima ikanyamaza hakuna aliyejitokeza lakini ikasikika sauti kutokea kuzimu shetani akasema nitume mimi nitaenda kumdanganya, Mungu akamuuliza utaenda kumdanganyaje yule pepo akasema nitaenda nitaingia mdomoni mwa wasaidizi wake ili wamdanganye kwa ushauri mbaya. Mungu akasema nenda ukafanye hivyo na ikawa. (kuwa makini unapopewa ushauri unaweza kupokea ushauri sio).
VITA YA AHABU
Mfalme Yehoshafati alikuwa amevaa mavazi ya Kifalme ahabu (kwenye vita usivae mavazi yasiyo yako utakufa) alipoonekana kwenye vita ile kumbe ilipangwa Mfalme akimbizwe apigwe mpaka afe, wakamfuata wakamzingira ili wamuue lakini Yehoshafati akapiga kelele akasema si yeye wasimuue nao wakamwachia. Askari mmoja katikati yao akasema anajisikia katikati ya watu hawa yupo mfalme Ahabu. Mtu mmoja akaamua kurusha mshale wa nasibu juu ili umtafute Mfalme Ahabu katikati ya watu wale, mshale ukamwona Ahabu ukashuka mpaka alipo ukatafuta mahali penye maongeo ya chuma kwenye mavazi yake maana alikuwa amevaa mavazi ya chuma ukamchoma mpaka kwenye moyo.
Kule Mikaya aliyefungwa hakusema namwachia Bwana haya yote yaliyotokea bali alisema apewe haki yake. Mfalme Ahabu alipopigwa na mshale ule alikimbizwa mpaka akaenda kuanguka na damu zikachuruzika mbwa wakaja wakaanza kumla kama Neno la mtu wa Mungu Eliya lilivyonena juu yake likatimia.
Baada ya hayo Wakaenda kumtoa Mikaya kwa heshima zote wakasema Nabii Mikaya wewe ni Mtumishi wa Bwana achana na wengine na mikaya akatoka na nchi nzima ikafurahi ikasema Hakika Mikaya ni nabii wa Mungu.
Ukiri:
“Kwa jina la Yesu nafuta ramani ya mikosi namabaya iliyopandwa kwenye kazi yangu na kwa jina la Yesu, nafuta maumivu na mikosi iliyochorwa juu ya bishara yangu, ninaharibu michoro ya giza juu yangu kwa jina la Yesu, kwa jina la Yesu wale waliotengeneza ramani za ubaya kwenye maisha yangu na familia yangu iwarudie wao kwa jina la Yesu. Nakusanya kundi la malaika waletao mabaya nawatuma waende kwale waliopanga mabaya juu yangu kwa jina la Yesu.” Amen
Naamuru kila ramani ya ubaya iliyochorwa juu yako iharibike na impate Yule aliyeichora juu yako kwa jina la Yesu. Amen.
Bishop Dr Josephat Gwajima
Jumapili ya Tarehe 12.02.2017

Gwajima: Ni afadhali kuishi siku moja kama simba kuliko siku mia moja kama Kondoo.
Gwajima: Sasa nataka tuanze kuomba maumbi ya kurusha Makombora. Makombora ya leo yatatua sehemu husika. Shauri yako, umechagua sehemu mbaya. Mwambie mwenzako ulitakiwa uwaze mara mbili.
Gwajima: Majeshi majeshi..majeshi ya bwana, yanaua majeshi..yanapiga kabisa..
Gwajima: Kizazi korofi Mungu anakitafutia Mtumishi Mkorofi. Nlikuwa nmelala lala hivi, sijamsaidia rais kwa inavyotakiwa sasa naamsaidia. Naahidi mbele za bwana ntamsaidia rais. Mimi ndo risasi yake ya mwisho ndani ya bunduki yake, ntamsaidia kunyosha wasaidizi wake waliopindapinda. Katika maombi ya leo asiwepo mtu wa kumshambulia Rais, polisi au TISS. Maombi ya leo ya alenga mtu mmoja.
Gwajima: Kesho narudi polisi kuwatetea nliyowaacha sero bila kujali ni Muislam au nani. Kesho naenda Polisi tena kumtete Manji, wakitaka wanikamate tena. Tunaye rais.
Gwajima: Nawashauri waumini wangu msifanye fujo sehemu yoyote, wale mtakaonifuate muwe watulivu.