Askofu Gwajima apekuliwa na Polisi nyumbani kwake, bado anashikiliwa kituoni

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,536
Hapo Jana Askofu Mkuu wa makanisa ya Ufufuo na Uzima Duniani, Dr Josephat Gwajima aliitikia wito wa polisi, baada ya mahojiano polisi waliamua kwenda kukagua nyumbani kwake, Salasala Dar es Salaam.

Upekuzi ulianza na kumalizika kukiwa na police wa upelelezi zaidi ya sita na ushahidi wa majirani wawili. Mara baada ya upekuzi walisainiana ripoti ya ukaguzi Mbele ya mashahidi hao kukiwa hakuna kitu chochote kilichopatikana kinachohusishwa na dawa za kulevya au bangi.

Baada ya ukaguzi huo polisi waliondoka na Askofu Mkuu Dr Josephat Gwajima na kurudi naye central police majira ya saa nne usiku kwa mahojiano zaidi ambapo hadi muda huu bado wamemshikilia.

Nitawaletea Updates zaidi.
 
kwa Manji walikwenda?
 
Hapo sasa! Unapiga kelele kwamba anahusika na dawa za kulevya ndipo saa kibao baadae unaenda kumpekua!!

Watu tukihoji ikiwa kuna nia thabiti tunaambiwa tunatetea wauza ngada!!! Hivi hata kama kweli huyo Gwajima anauza ngada, bado wanatarajia kukuta japo kakijiko kamoja ka ngada?!

Nasubiri yule aliyetangazwa hadharani kwamba yeye ndo ana bandari kabisa ya kushushia mzigo!!! But as usual, maafande wataenda pale "kupekuwa" saa kadhaa baada ya kuwa ameshatonywa kiaina kwamba "tunakujua wewe ni drug dealer na unatumia private boat dock kushusha mzigo kwahiyo tunakuja kukupekua!"

Sijui lini Watanzania tutaamka na kusema no to political drama!
 
Back
Top Bottom