SI KWELI PreGE2025 Askofu Gwajima ajiuzulu ubunge Kawe

SI KWELI PreGE2025 Askofu Gwajima ajiuzulu ubunge Kawe

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Wakuu nimeona hii taarifa kuwa Gwajima amejiuzulu ubunge kawe niya kweli?
1748967595925.jpeg
 
Tunachokijua
Madai

Mtumiaji mmoja wa mtandao wa X alichapisha taarifa iliyoambatana na grafiki yenye mfanano na nembo ya Wasafi media, grafiki hiyo ina barua yenye kichwa “Taarifa kwa Umma” na ‘caption’ inayosomeka GWAJIMA AJIUZULU NAFASI YA UBUNGE KAWE.

Uhalisia wa taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa taarifa hiyo na kujiridhisha kuwa si ya kweli. Ufuatiliaji umebaini kuwa hakuna chanzo cha kuaminika kilichochapisha wala kutoa taarifa hiyo.

Josephat Gwajima katika mitandao yake ya kijamii hajachapisha taarifa yenye kuashiria yeye kujiuzulu ubunge wake katika jimbo la Kawe, wakati ripoti hii inaandikwa taarifa ya mwisho iliyokuwa ikionekana katika ukurasa wake ilihusu kuhamasisha mfungo na maombi kuanzia tarehe 02 Juni 2025 hadi Juni 8, 2025.

Wasifu wake katika mtandao wa instagram bado unasomeka kuwa bado ni mbunge wa jimbo la Kawe, inasomeka; Member of parliament for Kawe constituency

Wasafi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii pia hawajachapisha taarifa wala grafiki yenye maudhui hayo kama inavyoonekana. Aidha grafiki hiyo pia ina makosa kadhaa ikiwemo kutumia mwandiko ‘font’ tofauti na inayotumiwa na Wasafi TV na FM.

Aidha Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima, leo Jumatatu Juni 2, 2025, aliitwa na Mwenyekiti wa Bunge kuuliza swali kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo
Free tundu Lissu.
No reform No election.
No reform No election.
No reform No election.
 
Back
Top Bottom