Askofu Emmaus Mwamakula: Ujumbe maalumu kwa Tundu Lissu

Toosweet

JF-Expert Member
May 27, 2012
2,141
1,982
Kwenu,

Nilipata taarifa za kupigwa kwako risasi muda mfupi tu baada ya tukio kupitia kwa mmoja wa watu ninaowaamini sana! Ingawa ulikuwa ni mchana lakini mwili wangu ulitetemeka sana! Mungu anajua nilichokifanya muda ule. Baadaye niliandika katika ukurasa wangu kuomba Mungu akuponye. Mungu amejibu maombi ya wengi na sasa umepona jambo ambalo linafaa kuitwa muujiza wa Mungu. Jambo lililokutokea linatosha kabisa kwa mtu kama alikuwa hamjui Mungu basi huo ndio unakuwa mwanzo wa kuutafuta uso wa Mungu.

Usiku wa leo ninao ujumbe kwako. Unapoendelea na harakati zako za siasa, huna budi kusamehe na kumuomba Mungu akuondolee chuki na uchungu moyoni mwako dhidi ya mtu au kikundi cho chote unachoweza kufikiri au kuhisi kuwa kilikuwa nyuma ya tukio la kushambuliwa kwako. Jambo hili sio jepesi hata kidogo bali unahitaji kumuomba Mungu akupe neema hiyo na ujasiri huo. Uchungu ukiruhusiwa kukaa katika kifua chako inaweza kuwa ni vigumu kwa mbingu kukupa nafasi kubwa zaidi baadaye! Ndiyo, mbingu zitaruhusuje mtu mwenye uchungu au chuki kushika madaraka makubwa? Kwa sababu akiruhusiwa ataweza kuyatumia kulipa kisasi jambo ambalo Mungu hataki kwa sababu kisasi ni cha kwake yeye Mungu.

Nelson Mandela alipokuwa tayari kusamehe ndipo Mungu akaruhusu atawale. Kwa mtazamo wangu, ukuu wa Nelson Mandela haupo katika mateso aliyopata na muda aliokaa gerezani pamoja na harakati zake. Bali ukuu wa Mandela ulitokana na kitendo cha yeye kusamehe waliomtesa miaka mingi. Nelson Mandela wakati mwingine alifikia hata hatua ya kumpa nafasi aliyekuwa mtesi wake mkuu kukaimu Urais wakati yeye hayupo.

Ninasoma, ninasikia na wakati mwingine ninaona yanayoendelea. Siyo siri, baadhi ya watu wananena mambo magumu na mabaya dhidi ya watu wanaowadhania walikuwa nyuma ya tukio lako. Ninaogopa kuwa 'huruma' za watu wa aina hii ukizisikiliza sana zitaweza kuujaza moyo wako uchungu badala ya rehema. Ninakusihi katika Jina la Yesu usikubali moyo wako ujazwe au ujae chuki.

Ukuu wa Jenerali Obasanjo na hata heshima aliyokuja kuipata baadaye ulitokana na unyenyekevu alioupata akiwa gerezani. Katika mazingira ambayo hayakutegemewa, baada ya Jenerali Abacha kufariki ghafla, Mungu alimuondoa 'mrithi halali' Abiola ili kuhakikisha tu Obasanjo anatawala. Siandiki ujumbe huu kama mtabiri, hapana. Na wala siandiki ujumbe huu kwa lengo la kukuandaa au kutokukuandaa kwa nafasi za uongozi, la hasha. Ninaandika ujumbe huu ili kuiandaa roho yako na nafsi yako kumruhusu Mungu aliyekuokoa kutoka katika bonde la uvuli wa mauti ili akuelekeze vizuri yakupasayo kufanya.

Ni dhahiri kuwa nafsi iliyoumizwa na inayoruhusu uchungu kifuani haiwezi kusikia ipasavyo sauti ya Mungu.
Kwa kuwa wewe ni mwanasiasa, utakuwa pia umemsoma Mahtma Gandhi yule kiongozi mashuhuri wa India aliyeiruhusu Biblia iongoze harakati zake ingawa yeye mwenyewe hakuwa Mkristo.

Ninajua kuwa ujumbe huu unaweza usipendwe na baadhi ya watu hasa wale waliojaa uchungu mioyoni mwao kwa kuwa unalenga kukutaka usamehe. Lakini ni wajibu wangu kama Askofu kukutaka hivyo. Watu hao watakaposoma ujumbe huu nao watasaidika. Ni dhahiri kuwa Mungu akitaka ufike sehemu utafika na akitaka usifike sehemu hautafika.

Kuna uhuru katika kusamehe! Kuna baraka katika kusamehe (Zaburi 32). Kuna ushawishi katika kusamehe! Kuna ulinzi na usalama katika kusamehe kwani mtu anayetangaza msamaha huwasababisha hata adui zake waweke silaha zao chini. Kinyume chake, mtu asiyesamehe anawafanya adui zake wajihami zaidi na hapo ndipo mapambano yanakuwa mazito kuliko ya awali.

Ninakutia moyo upate nafasi ya kuisoma Sala ya Bwana kwa tafakuri nzito. Mungu akikujalia neema na utayari kuchukua hatua ya kutangaza msamaha hadharani atakuongoza na atakuinulia watumishi wa Mungu watakaoandaa ibada kwa ajili hiyo au kukutia moyo kwa namna ambayo Mungu atakuongoza. Unaweza kutumia tukio lililokupata kwa ajili ya kumpa Mungu utukufu kwa njia ya kutangaza msamaha.

Utukufu uwe kwa Mungu awapae wakuu uwezo wa kutawala; awakwezaye wanyenyekevu na awashushaye wenye kiburi.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania (KMUT) & Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa ninaposoma pale wanafunzi (Mitume) walipomuomba Mwalimu wao (Yesu) awafundishe kusali kuna amazing verses.

"..utusamehe makosa yetu kama vile sisi tunavyowasamehe waliotukosea......."

Baadae anaongeza kwani msipowasamehe Watu makosa yao wala Baba yenu wa Mbinguni hatowasamehe ninyi makosa yetu.

Jamani kiukweli jamaa ameumizwa sana ila ili yeye ajipatanishe na nafsi yake inampasa asamehe ila aende na ile kauli "I survival to tell the tale"

Professorial rubbish ni shida aiseh
 
Kwenu,

Nilipata taarifa za kupigwa kwako risasi muda mfupi tu baada ya tukio kupitia kwa mmoja wa watu ninaowaamini sana! Ingawa ulikuwa ni mchana lakini mwili wangu ulitetemeka sana! Mungu anajua nilichokifanya muda ule. Baadaye niliandika katika ukurasa wangu kuomba Mungu akuponye. Mungu amejibu maombi ya wengi na sasa umepona jambo ambalo linafaa kuitwa muujiza wa Mungu. Jambo lililokutokea linatosha kabisa kwa mtu kama alikuwa hamjui Mungu basi huo ndio unakuwa mwanzo wa kuutafuta uso wa Mungu.

Usiku wa leo ninao ujumbe kwako. Unapoendelea na harakati zako za siasa, huna budi kusamehe na kumuomba Mungu akuondolee chuki na uchungu moyoni mwako dhidi ya mtu au kikundi cho chote unachoweza kufikiri au kuhisi kuwa kilikuwa nyuma ya tukio la kushambuliwa kwako. Jambo hili sio jepesi hata kidogo bali unahitaji kumuomba Mungu akupe neema hiyo na ujasiri huo. Uchungu ukiruhusiwa kukaa katika kifua chako inaweza kuwa ni vigumu kwa mbingu kukupa nafasi kubwa zaidi baadaye! Ndiyo, mbingu zitaruhusuje mtu mwenye uchungu au chuki kushika madaraka makubwa? Kwa sababu akiruhusiwa ataweza kuyatumia kulipa kisasi jambo ambalo Mungu hataki kwa sababu kisasi ni cha kwake yeye Mungu.

Nelson Mandela alipokuwa tayari kusamehe ndipo Mungu akaruhusu atawale. Kwa mtazamo wangu, ukuu wa Nelson Mandela haupo katika mateso aliyopata na muda aliokaa gerezani pamoja na harakati zake. Bali ukuu wa Mandela ulitokana na kitendo cha yeye kusamehe waliomtesa miaka mingi. Nelson Mandela wakati mwingine alifikia hata hatua ya kumpa nafasi aliyekuwa mtesi wake mkuu kukaimu Urais wakati yeye hayupo.

Ninasoma, ninasikia na wakati mwingine ninaona yanayoendelea. Siyo siri, baadhi ya watu wananena mambo magumu na mabaya dhidi ya watu wanaowadhania walikuwa nyuma ya tukio lako. Ninaogopa kuwa 'huruma' za watu wa aina hii ukizisikiliza sana zitaweza kuujaza moyo wako uchungu badala ya rehema. Ninakusihi katika Jina la Yesu usikubali moyo wako ujazwe au ujae chuki.

Ukuu wa Jenerali Obasanjo na hata heshima aliyokuja kuipata baadaye ulitokana na unyenyekevu alioupata akiwa gerezani. Katika mazingira ambayo hayakutegemewa, baada ya Jenerali Abacha kufariki ghafla, Mungu alimuondoa 'mrithi halali' Abiola ili kuhakikisha tu Obasanjo anatawala. Siandiki ujumbe huu kama mtabiri, hapana. Na wala siandiki ujumbe huu kwa lengo la kukuandaa au kutokukuandaa kwa nafasi za uongozi, la hasha. Ninaandika ujumbe huu ili kuiandaa roho yako na nafsi yako kumruhusu Mungu aliyekuokoa kutoka katika bonde la uvuli wa mauti ili akuelekeze vizuri yakupasayo kufanya.

Ni dhahiri kuwa nafsi iliyoumizwa na inayoruhusu uchungu kifuani haiwezi kusikia ipasavyo sauti ya Mungu.
Kwa kuwa wewe ni mwanasiasa, utakuwa pia umemsoma Mahtma Gandhi yule kiongozi mashuhuri wa India aliyeiruhusu Biblia iongoze harakati zake ingawa yeye mwenyewe hakuwa Mkristo.

Ninajua kuwa ujumbe huu unaweza usipendwe na baadhi ya watu hasa wale waliojaa uchungu mioyoni mwao kwa kuwa unalenga kukutaka usamehe. Lakini ni wajibu wangu kama Askofu kukutaka hivyo. Watu hao watakaposoma ujumbe huu nao watasaidika. Ni dhahiri kuwa Mungu akitaka ufike sehemu utafika na akitaka usifike sehemu hautafika.

Kuna uhuru katika kusamehe! Kuna baraka katika kusamehe (Zaburi 32). Kuna ushawishi katika kusamehe! Kuna ulinzi na usalama katika kusamehe kwani mtu anayetangaza msamaha huwasababisha hata adui zake waweke silaha zao chini. Kinyume chake, mtu asiyesamehe anawafanya adui zake wajihami zaidi na hapo ndipo mapambano yanakuwa mazito kuliko ya awali.

Ninakutia moyo upate nafasi ya kuisoma Sala ya Bwana kwa tafakuri nzito. Mungu akikujalia neema na utayari kuchukua hatua ya kutangaza msamaha hadharani atakuongoza na atakuinulia watumishi wa Mungu watakaoandaa ibada kwa ajili hiyo au kukutia moyo kwa namna ambayo Mungu atakuongoza. Unaweza kutumia tukio lililokupata kwa ajili ya kumpa Mungu utukufu kwa njia ya kutangaza msamaha.

Utukufu uwe kwa Mungu awapae wakuu uwezo wa kutawala; awakwezaye wanyenyekevu na awashushaye wenye kiburi.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania (KMUT) & Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umetumwa ila umebugi. Na waliommiminia risasi chuki zao wametubu?
 
Upande wa pili wa waliomfanyia hivyo mheshimiwa lissu vipi wenyewe hawana Ujumbe wowote wa kuwapa , maana baada ya Lissu bado wanaendeleza mateso kwa wengine kwa njia tofauti ikiwemo sumu ,vifungo ,mateso ya kila aina , na wenyewe Ujumbe wao ukowapi baba askofu ? .
 
Sauti itokayo nyikani, hakuna uhuru ndani ya moyo wa mtu bila kusamehe, ukisamehe, utakuwa umeutua mzigo mzito unaotembea nao kifuani na moyoni mwako na waliokuzunguka. Amina, TAL, samehe kila kitu na kwako hii itkuwa shule kubwa kuliko ya darasani. Tanzania ni yetu, neno AMANI, upendo na subira viendelee kuwa dira yetu. Sote, kwa namna moja au nyingine, tuna makosa na ndiyo ubinadamu.
 
Sala ya Bwana ipo karibu miaka 2000 iliyopita. Sijawahi kukutana na maandiko yoyote yanayoeleza kuwa Wayahudi wamewahi kuwatangazia msamaha Manazi ya Kijerumani. Lissu anaweza kusamehe lakini siku moja tusiyoijua sheria lazima ichukue mkondo wake, hata kama ni kuwahukumu marehemu walitenda uovu huo.
 
Utukufu juu mbinguni na amani duniani kwa watu aliowaridhia. Amina.
 
Sala ya Bwana ipo karibu miaka 2000 iliyopita. Sijawahi kukutana na maandiko yoyote yanayoeleza kuwa Wayahudi wamewahi kuwatangazia msamaha Manazi ya Kijerumani. Lissu anaweza kusamehe lakini siku moja tusiyoijua sheria lazima ichukue mkondo wake, hata kama ni kuwahukumu marehemu walitenda uovu huo.
Inahitaji neema ya Mungu kulielewa hili. Funguka masikio ya rohoni utaelewa.
 
Lissu alishasamehe muda mrefu saana na anashukuru Mwenyezi Mungu kumponya - sasa najiuliza unataka asamehe namna gani? asihoji waliompiga risasi kwa nini hawajakamatwa?
asihoji namna mazingira alivyopigwa risasi pale nyumba za vigogo ni kitendo cha kutosamehe? nk

Kama Lissu atakaa kimya basi atakuwa hajatimiza wajibu wake sababu same scenario inaweza kutokea kwa wengine ikawa mbaya zaidi - Mungu kamponya ili alifanyie kazi jambo hili kwa faida ya wengine wengi.
 
Lissu alishasame muda mrefu saana na anashukuru Mwenyezi Mungu kumponya - sasa najiuliza unataka asamehe namna gani? asihoji waliompiga risasi kwa nini hawajakamatwa?
asihoji namna mazingira alivyopigwa risasi pale nyumba za vigogo ni kitendo cha kutosamehe? nk

Kama Lissu atakaa kimya basi atakuwa hajatimiza wajibu wake sababu same scenario inaweza kutokea kwa wengine ikawa mbaya zaidi - Mungu kamponya ili alifanyie kazi jambo hili kwa faida ya wengine wengi.
huyo lissu anakisasi sana hawezi kusamehe ndiyo maana hatakiwi kuwa kiongozi
 
Askofu yuko sahihi sana!
Anko hapa alipofikia kuna siku anaweza kutoka mbio kwa miguu pale kwenye nyumba nyeupe mpaka burundi zinakoishi chuki!

Swali ni kuwa yeye akilalanayo bashite atabaki kwenye hali gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaweza kumjibu lolote huyu Askofu lakini ujumbe wake upo sambamba na maandiko.

Mimi nimwombacho Mungu wetu na Tundu mwenyewe ni kutenda yoye kwa dhamira moja tu - kuwasiaidia wengine walio wanyonge ambao sauti zao hazina uwezo wa kusikika, na siyo kwa dhamira ya kulipa kisasi.

Kwa vyovyote Mungu alitenda muujiza wa Lisu kwa lengo maalum. Asali na kuomba ili kulitambua lengo la Mungu.
 
Back
Top Bottom