Uchaguzi 2020 Askofu Benson Bagonza: Wote Hawaamini

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,485
99,200
WOTE HAWAAMINI...

Na Askofu Benson Bagonza, KKKT Dayosisi ya Karagwe

Waliopiga kura hawaamini,
Waliogoma kupiga kura hawaamini,
"Walioshinda" hawaamini,
"Walioshindwa" hawaamini,
Walioshuhudia hawaamini,
Waliohesabu kura hawaamini,
Wasimamizi hawaamini,
Waangalizi wa ndani na nje hawaamini,
Walinzi wa amani hawaamini,

Kwa nini lakini?

KWA sababu mwaka 2019 baada ya Uchaguzi wa serikali za mitaa,

"Walioshinda" hawakuwa na furaha,
"Walioshindwa" hawakuwa na furaha,
Waliopiga kura, ambao hawakupiga kura, waliohesabu, waliotangaza na waliosikia, WOTE hawakuwa na furaha. FURAHA alipotea, hajarudi. Sasa na IMANI ametoweka.

Usinibishie kwa sababu ubishi ni hulka ya watu waliopoteza furaha na Imani.

Nani anafuata kuwafuata FURAHA na IMANI?
 
Hata Robert Armstadam"aamini"

Mzee Ponda yuko wapi?
Dodoma alisema Lissu ndio Rais wa Tanzania kilichobaki ni kuapishwa tu, kwanini kawadanganya umma wa makamanda?
 
Hata Robert Armstadam"aamini"

Mzee Ponda yuko wapi?
Dodoma alisema Lissu ndo Rais wa Tanzania kilichobaki ni kuapishwa tu,kwanini kawadanganya umma wa makananda?
Kwani Sasa Lissu ameshindwa? Mbona ameshinda Sana. Mlichofanya ni kugeuza matokeo mkatangaza wa kwenu. Hilo tulilijua litafanyika kwa kuwa hamkubaliki na hili mnalijua, Magu anajua kuwa hakubaliki na MUNGU anajua. Kama mlikuwa mnakubalika, visa vyote hivyo vilikuwa vya nini? Hizo kura feki zilikuwa za nini? Polisi na tume ndio wameshikilia uhai wenu. Mngekuja uwanjani tupambane muone Nini kingetokea.
 
Back
Top Bottom