GE2025 Askofu Bagonza: Uchaguzi bila CHADEMA ni kama uchaguzi bila CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, amesema kuwa taifa linapitia mkwamo wa kisiasa na kiutendaji ambao unahitaji hatua ya dhati ya kujitafakari na kurudi kwenye misingi ya mazungumzo, siyo mapambano.

Akizungumza hivi karibuni kupitia mahojiano maalum na televisheni ya mtandao ya Sauti Digital, Askofu Bagonza amesema mchakato wa ndani wa kisiasa unaoendelea, hususan ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), unaonesha dalili za sintofahamu na upungufu wa misingi imara ya maadili ya kisiasa.

“Kuna mtu amejiunga na chama leo, siku hiyo hiyo anachukua fomu. Unajiuliza, hii ni nini? amesema Askofu Bagonza.

Ameelezea mshangao wake juu ya viongozi waliowahi kuwa sehemu ya tume ya uchaguzi iliyolalamikiwa, kisha kujiingiza katika mchakato wa kugombea, akisema hali hiyo inaleta maswali makubwa kuhusu uadilifu wa mchakato huo.

Akijibu hoja za baadhi ya watu wanaodai kuwa kutoshiriki kwa CHADEMA hakutaleta athari kwa kuwa kuna vyama vingine 18 vinavyoshiriki uchaguzi, Askofu Bagonza ametoa changamoto:

“Ebu wafikirie tuwe na uchaguzi mkuu usiokuwa na CCM, viwe hivyo 18 vingine na CHADEMA halafu aniambie kama huo ni uchaguzi, kwahiyo wanaoona CHADEMA haipo kwahiyo kuna mushkeli, pia wageuze akili zao waangalie kama hakuna CCM kama uchaguzi unaweza kufanyika. Mawazo yangu sina maana kwamba vyama vingine havifai. Ninaamini taifa ambalo linajumuisha kuliko kutawanya, natamani vyama vyote, tena hata vingine ambavyo havijasajiliwa”.

Amesema taifa linahitaji kuwa na "utaratibu jumuishi" ambapo kila Mtanzania anahusishwa kikamilifu bila kubaguliwa – hata wale wasiokuwa na vyama – na kusisitiza kuwa hekima haijachelewa.

“Hekima hata ikichelewa, siku moja inatosha. Kinachotakiwa ni utashi wa kisiasa (political will) wa kutupeleka kwenye taifa la mazungumzo, siyo taifa la mapambano,” alihitimisha Askofu Bagonza.

Kauli yake imekuja wakati wa mchakato unaoendelea wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea ubunge na udiwani ndani ya CCM, huku kukiwa na sintofahamu juu ya ushiriki wa CHADEMA- chama kikuu cha upinzani nchini katika uchaguzi mkuu wa 2025.
 
CHADEMA ndio tumaini pekee la kulivusha taifa letu
 
Wavimba macho hawaamini mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025 unavyoenda vizuri, sasa wanafikiri wanaweza kuukwamisha kwa maneno ya kwenye khanga.
 
NO REFORMS NO ELECTION, Watanzania wanajua vyama vingine nje ya CHADEMA ni Mali ya CCM hivyo uchaguzi bila CHADEMA tafsiri yake ni kwamba CCM inasimama peke yake kwenye uchaguzi na kujipigia kura.
 
Wavimba macho hawaamini mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025 unavyoenda vizuri, sasa wanafikiri wanaweza kuukwamiaha kwa maneno ya kwenye khanga.
Wewe ndo hutaamini utakapoona reforms zimefanyika,kaa kwa Kutulia,hii nchi si ya CCM peke yao,,na hizo reforms sio za chadema peke yao hata wewe utanufaika nazo

Unachukia reforms kwa kuwa uko upande wa CCM,amini nakwambia Kuna siku utakuwa mpinzani na hapo ndo utajua umuhimu wa reforms.
.
Kama kina lowassa na sumaye waliona umuhimu wa reforms,ije kuwa wewe keyboard warrior!?
 
“Kuna mtu amejiunga na chama leo, siku hiyo hiyo anachukua fomu. Unajiuliza, hii ni nini? amesema Askofu Bagonza.
Huyu askofu wa CHADEMA aache upumbavu. Lowassa alipewa fomu ya urais na ujumbe wa kamati kuu ndani ya masaa 24 huko CHADEMA mara baada ya kujiunga kwa hiyo wao ndo waasisi wa hilo kama anaona haifai. Ndani ya CCM hakuna ubaguzi. Mwanachama aliyejiunga leo ana haki sawa na aliyejiunga mwaka 1978.
 
Wewe ndo hutaamini utakapoona reforms zimefanyika,kaa kwa Kutulia,hii nchi si ya CCM peke yao,,na hizo reforms sio za chadema peke yao hata wewe utanufaika nazo

Unachukia reforms kwa kuwa uko upande wa CCM,amini nakwambia Kuna siku utakuwa mpinzani na hapo ndo utajua umuhimu wa reforms.
.
Kama kina lowassa na sumaye waliona umuhimu wa reforms,ije kuwa wewe keyboard warrior!?
Sasa hivi nchi ipo bize na Uchaguzi Mkuu. Maboresho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tutayafanya baada ya Uchaguzi kwakuwa yapo kwenye Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM!

Zaidi ya hapo, HAKUNA reforms zozote!
 
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, amesema kuwa taifa linapitia mkwamo wa kisiasa na kiutendaji ambao unahitaji hatua ya dhati ya kujitafakari na kurudi kwenye misingi ya mazungumzo, siyo mapambano.

Akizungumza hivi karibuni kupitia mahojiano maalum na televisheni ya mtandao ya Sauti Digital, Askofu Bagonza amesema mchakato wa ndani wa kisiasa unaoendelea, hususan ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), unaonesha dalili za sintofahamu na upungufu wa misingi imara ya maadili ya kisiasa.

“Kuna mtu amejiunga na chama leo, siku hiyo hiyo anachukua fomu. Unajiuliza, hii ni nini? amesema Askofu Bagonza.

Ameelezea mshangao wake juu ya viongozi waliowahi kuwa sehemu ya tume ya uchaguzi iliyolalamikiwa, kisha kujiingiza katika mchakato wa kugombea, akisema hali hiyo inaleta maswali makubwa kuhusu uadilifu wa mchakato huo.

Akijibu hoja za baadhi ya watu wanaodai kuwa kutoshiriki kwa CHADEMA hakutaleta athari kwa kuwa kuna vyama vingine 18 vinavyoshiriki uchaguzi, Askofu Bagonza ametoa changamoto:

“Ebu wafikirie tuwe na uchaguzi mkuu usiokuwa na CCM, viwe hivyo 18 vingine na CHADEMA halafu aniambie kama huo ni uchaguzi, kwahiyo wanaoona CHADEMA haipo kwahiyo kuna mushkeli, pia wageuze akili zao waangalie kama hakuna CCM kama uchaguzi unaweza kufanyika. Mawazo yangu sina maana kwamba vyama vingine havifai. Ninaamini taifa ambalo linajumuisha kuliko kutawanya, natamani vyama vyote, tena hata vingine ambavyo havijasajiliwa”.

Amesema taifa linahitaji kuwa na "utaratibu jumuishi" ambapo kila Mtanzania anahusishwa kikamilifu bila kubaguliwa – hata wale wasiokuwa na vyama – na kusisitiza kuwa hekima haijachelewa.

“Hekima hata ikichelewa, siku moja inatosha. Kinachotakiwa ni utashi wa kisiasa (political will) wa kutupeleka kwenye taifa la mazungumzo, siyo taifa la mapambano,” alihitimisha Askofu Bagonza.

Kauli yake imekuja wakati wa mchakato unaoendelea wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea ubunge na udiwani ndani ya CCM, huku kukiwa na sintofahamu juu ya ushiriki wa CHADEMA- chama kikuu cha upinzani nchini katika uchaguzi mkuu wa 2025.
Sasa anawapigia chapua Chadomo wenzie wakati yeye ndio aliwashauri wasuse?

Suseni CCM wanaendeleza mafuriko ya kuchukua fomu.

Wakishindana CCM pekee inatosha.
 
Kamanda bagonza chama chako cha Chadema hakina umuhimu wowote kwenye mchakato wa uchaguzi, nadhani wakati umethibitisha yani watu wamejiandaa vizuri kupiga kura Oktober
 
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, amesema kuwa taifa linapitia mkwamo wa kisiasa na kiutendaji ambao unahitaji hatua ya dhati ya kujitafakari na kurudi kwenye misingi ya mazungumzo, siyo mapambano.

Akizungumza hivi karibuni kupitia mahojiano maalum na televisheni ya mtandao ya Sauti Digital, Askofu Bagonza amesema mchakato wa ndani wa kisiasa unaoendelea, hususan ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), unaonesha dalili za sintofahamu na upungufu wa misingi imara ya maadili ya kisiasa.

“Kuna mtu amejiunga na chama leo, siku hiyo hiyo anachukua fomu. Unajiuliza, hii ni nini? amesema Askofu Bagonza.

Ameelezea mshangao wake juu ya viongozi waliowahi kuwa sehemu ya tume ya uchaguzi iliyolalamikiwa, kisha kujiingiza katika mchakato wa kugombea, akisema hali hiyo inaleta maswali makubwa kuhusu uadilifu wa mchakato huo.

Akijibu hoja za baadhi ya watu wanaodai kuwa kutoshiriki kwa CHADEMA hakutaleta athari kwa kuwa kuna vyama vingine 18 vinavyoshiriki uchaguzi, Askofu Bagonza ametoa changamoto:

“Ebu wafikirie tuwe na uchaguzi mkuu usiokuwa na CCM, viwe hivyo 18 vingine na CHADEMA halafu aniambie kama huo ni uchaguzi, kwahiyo wanaoona CHADEMA haipo kwahiyo kuna mushkeli, pia wageuze akili zao waangalie kama hakuna CCM kama uchaguzi unaweza kufanyika. Mawazo yangu sina maana kwamba vyama vingine havifai. Ninaamini taifa ambalo linajumuisha kuliko kutawanya, natamani vyama vyote, tena hata vingine ambavyo havijasajiliwa”.

Amesema taifa linahitaji kuwa na "utaratibu jumuishi" ambapo kila Mtanzania anahusishwa kikamilifu bila kubaguliwa – hata wale wasiokuwa na vyama – na kusisitiza kuwa hekima haijachelewa.

“Hekima hata ikichelewa, siku moja inatosha. Kinachotakiwa ni utashi wa kisiasa (political will) wa kutupeleka kwenye taifa la mazungumzo, siyo taifa la mapambano,” alihitimisha Askofu Bagonza.

Kauli yake imekuja wakati wa mchakato unaoendelea wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea ubunge na udiwani ndani ya CCM, huku kukiwa na sintofahamu juu ya ushiriki wa CHADEMA- chama kikuu cha upinzani nchini katika uchaguzi mkuu wa 2025.
Bagonza, mahaba yake kwa chadema yana mpotosha sana, theology aliyoisoma ameiweka pembeni kabisa
 
Wavimba macho hawaamini mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025 unavyoenda vizuri, sasa wanafikiri wanaweza kuukwamiaha kwa maneno ya kwenye khanga.
Bila reforms uchaguzi haufanyiki. Hata nyie mlioko CCM mnalifahamu hilo vizuri kabisa.
 
Bagonza, mahaba yake kwa chadema yana mpotosha sana, theology aliyoisoma ameiweka pembeni kabisa
Jibu hoja zake, usimuatack yeye binafsi. Kama alichokiongea ni uongo, kosoa af uoneshe ukweli ulipo.
 
Back
Top Bottom