Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,880
- 828,445
NAIPONGEZA JAMHURI na KUISHAURI
Wale mnaopenda kuwapopoa kwa mawe wale msiokubaliana nao, nawaomba mnipopoe.
Jamhuri katika kesi ya uhaini inayomkabili “Mtundu” wa Taifa, Tundu Lisu, imeamua kukata rufaa kwa kesi ambayo haijahukumiwa au haijafika mwisho. Wamejuaje kuwa wameshindwa na kuamua kukata rufaa?
Mimi NAWAPONGEZA sana Jamhuri kwa uamuzi huo uliokuja ghafla.
Namwona mtu anataka kunikosoa kuwa Jamhuri wamekatia rufaa uamuzi mdogo siyo kesi nzima. Bado naiona hekima ya kosa la Jamhuri kukatia rufaa uamuzi mdogo badala ya kusubiri hukumu ya mwisho. Najieleza sasa:
1. Mjaluo akiwa anapigana na mkewe na ghafla akaingia mgeni; ugomvi huwa unaisha. Uamuzi mdogo uliofanywa na majaji kuhusu hoja ya kuleta ushahidi mpya, ni kama mgeni aliyekuta ugomvi unaendelea. Badala ya Jamhuri kumaliza ugomvi, imekata rufaa. Hiyo ndiyo njia ya kumaliza ugomvi na lawama zote ziende kwa mgeni aliyeingia.
2. Nia ya kukata rufaa SIYO kukata rufaa. Mjaluo akizidiwa nguvu na mkewe huwa anapiga kelele na kusema “Jamani nishikeni vinginevyo namuua huyu”. Hapo waamuzi huingia kumwokoa mme lakini mke hudhani ameokolewa yeye. Wako wapi wazee wenye hekima waingilie ugomvi huu ili kuokoa heshima ya taifa letu?
3. Naipongeza Jamhuri kwa kutengeneza fursa adimu ya kumaliza jambo hili kwa hekima. Wale mnaohangaika na MARIDHIANO, Hapa ndipo Jamhuri amewapasia mpira na kipa wa Kijaluo ameishatoka golini. Malizia hapa ili machawa watengeneze sinema nyingine. Hii imechuja na wasiojua sheria wameanza kubobea kuliko Katuga.
4. Jamhuri si DPP wala serikali kwa maana ya “Excutive Branch”. Jamhuri ya kweli ni sisi sote akiwamo Tundu Lisu, Katuga, Majaji, Polisi, boda boda na “polisi boda boda” wanaotoa ushahidi.
Hatuna maslahi na ugomvi huu. Ni hasara kwa nchi na mahusiano ya kijamii. Hata Wajaluo wanaelekea kuchoka kusikiliza kesi hii.
Naelewa wito wangu na pongezi vinaweza visiwe na maana. Hata “Ngariba haogopi mkojo”, kwa sasa hivi tunajiumiza wenyewe kwa mashimo yanayowekwa wazi katika ugomvi huu.
Kwaresima Njema
Ramadhani Kareem
Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza