Askofu Bagonza: Hili la Dr Bashiru na matumizi ya Dola inamanisha Hata tukipiga tusipopiga kura bado dola itaamua nani mshindi

Ngoja nikuulize sawali dogo tu, ni kwanini huyo Katibu mkuu alisema wazi kuwa wao CCM hawatakubali yaliyowapata KANU ya Kenya na UNIP ya Zambia........

Kama hakumaanisha kuwa chama tawala ni lazima kitumie dola kubaki madarakani?
 
Wachache wenye madaraka wanaamua kutumia vyombo vya dola kulinda vyeo vyao kupitia mgongo wa chama tawala.
CCM kinataka kulinda maslahi yao kupitia mtutu wa bunduki.
Wanawachonganisha wananchi na vyombo vyao vya dola mana watoto wao hawana shida zaidi ya kuogelea kwenye mahela ya walipa kodi na kula raha kama yule RC.
Ndio maana hata Bashiru ameamua kuwatupa wananchi wapiga kura na kuvuruga Misingi ya demokrasia na utawala bora ili tu kulinda nafasi yake ya ukatibu mkuu.
Bashiru Yupo tayari kuona damu za watoto wa taifa hili wakiumizwa na kuteshwa hata kuuawa kwa sababu tu ya kulinda ukatibu wake na chama chake.
Imani na dini amevitupilia mbali kwa sababu ya madaraka amesahau kabisa kuwa yeye ni mwanadam ; kuna leo na kesho, kuna kujibu mbele za Hakimu wa wote kule ahera.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndiyo hasara ya viongozi waropokaji wa awamu hii, hawapimi kwanza hata athari ya kauli zao. Hata yale mambo ya sirini huropoka tu kutokana na ulevi wa madarakani. Hongera Dk. Bagonza kwa kuliona jambo hili lenye ukakasi mwingi na kulitolea kauli iliyojaa hekima nyingi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KARLO MWILAPWA, kama unaamini Dr Bashiru hakueleweka vizuri, mshauri hasiwe anaongea na watanzania kama alivokua anafunsisha wanafunzi wake pale UD asitumie nadharia za kitaaluma ilihali akijua anaongea na watanzania wenye elimu na wasio na elimu.
Atume lugha na nadharia inayoeleweka kisawasawa bila tashwishwi na utetezi eti hajaeleweka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na usomi wake Dr Bashiru has stooped too low,hawajiamini na hawaheshimu maamuzi ya wapiga kura.Ndiyo maana sasa wanaanza kukiri kuwa wanawanunua wapinzani,wameiteka Tume ya Uchaguzi,Polisi na Mahakama hivyo mpige kura au msipige haiwahusu.Wao ni washindi iwe mvua,liwe jua wanashinda kwa 99.9999%.Wanajiona bora kuliko Wananchi, wamelewa mvinyo wa damu za wapinzani wao.
 
Kama mtumishi umemwelewa amesema huwenda akawa anamaanisha vinginevyo Ila masikioni ndivyo alivyosikika, kabla hujamlaumu mtu nivema ukajiuliza wewe mwenyewe ulivyoelewa kwani swala lauelewa nilamtu binafsi hivyo huwezi mlaumu mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bagonza bora atangaze tu nia yake,huko anakoelekea si pazuri anaisakama sana dola
 
Mbona alitafsiri the same day..!

Kiufupi siyo mtu makini alipotosha waziwazi maana ya dola.

Eti dola ni TRA inapokusanya kodi


Itoshe kumuonesha watanzania si wajinga wanauwezo wa kudadavua mambo kuliko ata yeye na degrii zake za sayansi ya siasa amejiumbua kuongea bila kutafakari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fafanua wew sasa uliye elewa kumzidi Askofu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunamshukuru Baba Askofu kwa kutonyamaza. Katika lindi la uvuli wa mauti wa wasiojulikana inakubidi ujikane kufanya afanyayo baba Askofu Bagonza. KUTOA MAWAZO YAKE. Mwenyezi Mungu amlinde. Tunakumbuka yaliyomkuta aliyekuwa anatoa mawazo yake yule mbunge ambaye hata kumtaja ni hatari mbele ya wasiojulikana maana Mwenyezi Mungu amewaumbua ushetani wao unaojulikana na malipo yake hawajayalipa bado
 
Kwenye debate mawazo yako ni ya wale wanaotaka kuonekana kwamba wanapambanua mambo lakini ndani yake ni pumba tupu
 
Umesahau Bushiru alivyopindisha kuhusu Azory Agwanda.

Mara zote kauli ya kwanza huwa ya kweli na hakika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…