Askofu Bagonza akosoa kauli ya 'Aliyepewa mimba asirudi', ahoji makosa ya viongozi yangekuwa mimba, wangekuwa na ngapi?

Status
Not open for further replies.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Dk Bagonza amepingana na uamuzi wa Serikali kuhusu wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito kutokuruhusiwa kurudi shuleni kuendelea na masomo. Dk Bagonza amesema viongozi wengi tulionao ni matokeo ya second chance katika elimu kwani wengi walifeli na wakatafuta njia mbadala kuhakikisha wanafika hapo hivyo haoni kama ni hekima kuwanyima second chance wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito



Sent using Jamii Forums mobile app


Huyu ni KKKT kweli? Nadhani ni mwanasiasa wa kupinga kila kitu. Aulizwe hivi katika shule zinazomilikiwa na KKKT wanaruhusu mwanafunzi mwenye mimba kuendelea na masomo? Jibu ni kwamba hawaruhusiwi.

Sijui ana umri na uelewa gani huyu askofu. Kwa kumbukumbu zake ni lini wanafunzi waliwahi kuruhusiwa kuendelea na shule tangu awamu ya Mwl Nyerere? Jibu ni kuwa hapa TZ haijawahi kutokea mwanafunzi mjamzito kuruhusiwa kuendelea na shule ya msingi au sekondari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hv huyo Askofu atakuwa anasimamia kitabu gani? Ni Biblia agano la kale au la ssa!?

Mhe Rais alichosema ni kwamba watakaopata mimba hawataruhusiwa kwenye mfumo rasmi wa shule za Serikali. Hi haina tofauti kabisa na makatazo yaliyopo kwenye vtabu vyetu vitakatifu kwamba "Usizini".

Sijawahi kuona popote kwenye vitabu hvi palipohalalisha zinaa, sio kwa watoto wa Shule au watu wazima. Tendo hili limehalalishwa kwa wanna ndoa pekee.

Ssa mnavyomtaka Rais atamke rasmi kwamba watakaopata mimba wataruhusiwa kuendelea na masomo, mnataka arejee kitabu gani?

Binadamu tu wenye dhambi lakini tusitimie hali hiyo kuhalalisha matendo yanayokatazwa kiimani, kijamii, Kimaadili na kisheria.

Nnao uzoefu wa Shule zetu za Seminari. Kanuni zinazotumika kule ni Kali sana kiasi kwamba wanafunzi wanaofanikiwa kuziishi huwa wanatoka wakiwa na maafili mazuri ya kimaisha kila njanja.

Nnavyosikia ushauri huu ukitolewa hadharani tena na Askofu napata mashaka na kondoo anaowachunga. Dhambi hii ingeshauriwa na wanasiasa nisingeshtuka Sana, lakini Askofu, Sheikh?, Duh!

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeandika kwa kutumia Akili ya mtawala wako rudia tena kumsikiliza Askofu Bagonza anamaanisha nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii hoja ni ya kijinga kabisa. Ni kama zama zile wapo waliosema kuhimiza matumizi ya Kondomu kutachochea ngono, lakini watu walipoanza kuathirika kwa UKIMWI ndipo wakaelewa kwamba kuna tatizo walilitengeneza. Siamini kwamba kuna wanafunzi wanatamani kupata mimba ili wakatize masomo!
Hawa ndo wanao ongelewa na baba askofu.
 
Naomba kukumbushwa! Hivi ni kweli JPM alikataa wasisome au wasisome kwenye Shule za serikali ( mfumo rasmi)

Nakumbuka akisema waendelee na elimu ya watu wazima kama vile! Hebu niiumbusheni ili tuepuke uchochezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mheshimiwa Askofu, mfumo wa "sevond chance" ulikuwaje? Nani kaufuta sababu magufuri amekataa wasiendelee na shule za umma zinazosomesha watoto Bure!!! Ndio maana ameruhusu NGO's na wengine wanaotetea kufungua Shule za wazazi!!!
 
Askofu Benson Bagonza anafahamika vizuri hata kabla hajawa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe. Akitumia matoleo na sadaka za wakristu tena masikini aliunga mkono na kusaidia wagombea wote wa upinzani katika jimbo la Karagwe na Kyerwa mwaka 2000, 2005, 2010 na 2015. Mtandao wake wote unafahamika na hana jipya huyo.

Dayosisi ya Karagwe imemshinda na amewaletea waamini mgawanyiko mkubwa, leo anaanza kumsakama Mhe. Rais wetu kwa kutumia lugha ya picha. Ashindwe kwa Jina la Yesu aliye HAI pamoja na hila zake zote. Muache Rais wa wanyonge aendelee kutupigania Watanzania.
 
Big up Askofu yaani kuna watu sijui wana shida gani kichwani yaani adhabu pekee ya mtu akizaa asiruhusiwe kusoma??? Alafu whats next??? Yaani wamekosa adhabu ingine mpaka washabikie adhabu inayoua elimu Tanzania kaz kwelikweli
 
Askofu Benson Bagonza anafahamika vizuri hata kabla hajawa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe. Akitumia matoleo na sadaka za wakristu tena masikini aliunga mkono na kusaidia wagombea wote wa upinzani katika jimbo la Karagwe na Kyerwa mwaka 2000, 2005, 2010 na 2015. Mtandao wake wote unafahamika na hana jipya huyo. Dayosisi ya Karagwe imemshinda na amewaletea waamini mgawanyiko mkubwa, leo anaanza kumsakama Mhe. Rais wetu kwa kutumia lugha ya picha. Ashindwe kwa Jina la Yesu aliye HAI pamoja na hila zake zote. Muache Rais wa wanyonge aendelee kutupigania Watanzania.
Kwahyo kusupport wapinzani ndio dhambi?? Kwani sio watanzania??? Acheni kejeli hizo huyu kaongea kutokea mtazamo wa kidini mbona Allah midhambi yote tunafanya ila bado tukimuomba msamaha na kujitakasa anatusamehe ???? Sasa kwanni hamtoi second chance au hata adhabu tofauti na ya kuwafungua kusoma milele mnafaidika nni nyie mnaoshabikia sera hii???
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom