Askofu apekuliwa uwanja wa ndege akidhaniwa kabeba 'unga' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu apekuliwa uwanja wa ndege akidhaniwa kabeba 'unga'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Nov 21, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Moses Mashalla, Arusha
  ASKOFU Mkuu wa Kanisa la International Evangalism (IEC), Eliud Isangya anadaiwa kushikiliwa na kisha kupekuliwa kwa saa kadhaa muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa kudhaniwa kuwa alikuwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Cocaine.

  Askofu Isangya ameshikiliwa miezi michache baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwanyooshea vidole baadhi ya viongozi wa dini kwa kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya hapa nchini, kauli ambayo ilipingwa vikali na viongozi hao.

  Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya gazeti hili, mizigo mbalimbali ya askofu huyo mwenye makazi yake mkoani Arusha ilishikiliwa na kasha kupekuliwa na maofisa usalama waliokuwa uwanjani hapo baada ya kutaarifiwa kuwa ndani ya mizigo hiyo alikuwa amehifadhi madawa ya kulevya aina ya Cocaine.

  Vyanzo hivyo vilidai ya kuwa upekuzi huo ulifanyika baada ya askofu huyo kutua uwanjani hapo akitokea kwenye safari zake za kusambaza injili nje ya nchi ambapo maofisa hao wa usalama walikuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu baada ya kupokea taarifa kwamba ni miongoni mwa viongozi wa dini wanaodaiwa kujihusisha na biashara hiyo haramu.

  Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro, Absolom Mwakyoma alipoulizwa juu ya madai hayo alisema ya kuwa hana taarifa za kina juu ya tukio hilo kwa kuwa ni mpya na kuomba apewe muda kufuatilia kisha atatoa taarifa kamili juu ya tukio hilo baadaye.

  "Mimi ndio nazisikia hizo taarifa kutoka kwako, hii ni mpya kwangu, nipigie baadaye nifuatilie kisha ntakupa maelezo," alisema Mwakoya.

  Hatahivyo, alipopigiwa simu yake ya kiganjani baadaye, Mwakyoma alisema kuwa bado wanafuatilia tukio hilo makao makuu kwa kuangalia jina la Askofu huyo kwenye orodha ya watu walioshikiliwa hivi karibuni.

  Naye Kamanda wa kitengo maalumu cha kupambana na dawa za kulevya hapa nchini, Godfrey Nzowa alipohojiwa alithibitisha taarifa hizo huku akisisitiza kuwa upekuzi ulifanywa kwa Askofu huyo ulikuwa ni kawaida tu.

  "Ni kweli nimeulizia jina la Askofu huyo maofisa pale uwanjani wameniambia ni kweli alipekuliwa lakini upekuzi ulikuwa ni wa kawaida tu hususani kwa abiria wanaotoka nje ya nchi," alisema Nzowa.

  Kwa upande wake, Askofu Isangya alipoulizwa juu ya madai hayo alikiri kushikiliwa na kisha kupekuliwa ndani ya uwanja huo, lakini alibainisha ya kuwa katika upekuzi huo maofisa hao walipekua mizigo mbalimbali aliyokuwa nayo na hawakufanikiwa kuona chochote.

  Alisisitiza ya kwamba hivi karibuni kumekuwa na njama mbalimbali zinazofanywa na mahasimu wake kwa kumzushia kila aina ya uwongo huku akidai kuwa njama hizo zina lengo la kumchafulia jina lake mbele ya jamii.

  "Ni kweli nilipotua tu wakanishikilia na kisha kunipekua, lakini hawakukuta chochote, walidai wana mashaka na mimi kwamba nimebeba madawa ya kulevya, nilipowauliza iweje leo napekuliwa mizigo yangu na si kawaida wao wakadai ni hali ya kawaida tu. Lakini niseme hizi ni njama za baadhi ya watu kutaka kunichafulia jina langu tu," alisema kwa unyonge.

  chanzo. Gazeti la Mwananchi

  HII KALI JAMANI HATA ASKOFU NAE ANABEBA UNGA? HII BIASHARA IMEINGILIWA NA WENYEWE...........
   
 2. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,278
  Likes Received: 665
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa alitaka kujenga Airpot yake kule Sakila wakambania
   
 3. nsangaman

  nsangaman JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Askofu Eliud ni mafia ati,tembelea Voice-Sakila
  Kaka yake aelezea umafia wake
   
 4. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwani yeye nani asipekuliwe? Hawa ndo wamekuwa wakijifanya wachunga kondoo kumbe wanakuja kuharibu jamii na mitamaa yao. Yeye siyo indespensable bwana!
   
 5. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Okay, so what is next
   
 6. Kadamfu

  Kadamfu Senior Member

  #6
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  89%ya wachungaji na mapadre ni wauza unga .kupekuliwa lazima
   
 7. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Huyu jamaa ni miongoni mwa mabilionea wa bongo,jamaa ana uwanja wake mwenyewe wa ndege na ana ndege yake.
   
 8. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa biashara ya uaskofu tu au kuna lingine?
   
Loading...