Askari wawili wa wanyama pori wauawa Runzewe

Chibingwa

Member
Jan 17, 2008
49
7
ASKARI wawili wa jeshi la wanyama poli wameuawa jana jioni baada ya kupigwa na wananchi wa kijiji cha Nyamonge kata ya Runzewe wilayani Bukombe baada ya kuzaniwa kuwa ni majambazi.
Baada ya askari hao kuuawa pikipiki waliyokuwa nayo iliteketezwa kwa moto. Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio wananchi waliwatilia mashaka askari hao baada ya askari wanne wakiwa na pikipiki kufuka kijijini hapo wakiwa na silaha na baadae kuondoka.
Baada ya askari hao kuondoka muda kitambo askari wawili walirejea kijijini hapo wakiwa na pikipiki moja bila siraha na ndipo wananchi walipowaweka chini ya urizi na kuanza kuwashambulia.
Mkuu wa wilaya ya Bukombe ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo amethibitisha kuuawa kwa askari hao.
 
Ahaaaa nilitaka kupata afueni nikidhani ni askari wetu hawa wengine wazee wa PT
Hao wa wanyama pori mwenyezi mungu awarehemu..
 
Hiyo watakuwa wamefanya makusudi tu. Kama walishawamaki kuwa ni maaskari wa wanyama pori toka mwanzo kwa nini wawapige?
Othewise kwa kuwa siku hizi serikali yetu inacheza na majambazi kwa kuwa wako juu ya sheria. Basi hiyo ni hatua nzuri kumaliza majambazi nchini.
 
Nilizan askari walinda geto

Dah.....nilizani ni askari wa Chagonja.........

Ahaaaa nilitaka kupata afueni nikidhani ni askari wetu hawa wengine wazee wa PT
Hao wa wanyama pori mwenyezi mungu awarehemu..

Nanyi mkishika dola,mtawatumia hawahawa mnaoona wanawapiga na kuwanyanyasa! Hakuna Taifa lisilo na Polisi. Hakuna Polisi anayewaacha wananchi wakafanya vile wanavyotaka.

Hata huko kwa Baba zenu ambako Demokrasia ilizaliwa na kubarehe,Polisi wanafanya hata zaid ya wanavyofanya huku kwetu.

My take; Do not blame Policemen, blame the gvt that monitors an Army (in case it makes poor in orders & routines.
 
Pathetic
 
Hawakuwa na sare, vitambulisho wala radio??!!!!

Mbona taarifa haiko sawa, au mambo ya kutanguliza mzigo tutaufuata baadaye na kugeukana??!!!
 
Nilizan askari walinda geto
Inabidi lianzishwe jukwaa la wachafuzi wa lugha. Nili-za-n ndiyo nini katika lugha yetu tamu ya Kiswahili? Ama ndiyo matokeo ya 0.3 GPA kuruhusiwa kuendelea na kidato cha tatu na yale matokeo ya Mulugo?
 
Nanyi mkishika dola,mtawatumia hawahawa mnaoona wanawapiga na kuwanyanyasa! Hakuna Taifa lisilo na Polisi. Hakuna Polisi anayewaacha wananchi wakafanya vile wanavyotaka.

Hata huko kwa Baba zenu ambako Demokrasia ilizaliwa na kubarehe,Polisi wanafanya hata zaid ya wanavyofanya huku kwetu.

My take; Do not blame Policemen, blame the gvt that monitors an Army (in case it makes poor in orders & routines.

Ni kweli polisi ni hao hao. La msingi ni, je wanatumikaje? Na wao wako tayari kutumikaje? Serikali ilitakiwa iwatumie vizuri, lakini pia walikuwa na nafasi ya kukataa kutumika vibaya.
 
Kwa jeshi lenye nidhamu kama la Tz, utawaonea utakaposema "wakatae kutumika vibaya". Ni jambo ambalo sio rahisi kias hicho.
 
Back
Top Bottom