Askari Wanyamapori waua mtu Iringa

Askari Wanyamapori waua mtu Iringa

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,176
Reaction score
48,460
Katika kile kinachoonekana ni muendelezo wale tuliowakabidhi jukumu la kulinda ama watu au Rasirimali zetu kuua Raia wasio na Hati, Askari wa wanyama Pori wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha wamemuua kwa kumpiga Risasi mtu mmoja kwa tuhuma za kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria.

Askari hao wakiwa kwenye Land Rover mbili walivamia nyumbani kwa Iddy Kiruma kitongoji cha Mbigima, kijiji cha Isele kwenye Kata ya Mlenge, Jimbo la uchaguzi Isimani Wilaya ya Iringa, Mkoani Iringa, na kumpiga risasi ya mguu kiruma. Kwenye Nyumba hiyo pia alikuwemo Shaabani Chalamila ambaye kwenye purukushani hiyo alifanikiwa kutoroka. Kiruma amekufa akiwa mikononi mwa Askari hao haijulikani walikuwa anampeleka wapi kama ni Hospitali au Kambini kwao.

Askari hao baada ya Shaaban kutoroka walikwenda nyumbani kwake na kumchukua mke wake, Anna Mahogola mwenye watoto mapacha walio na umri wa mwaka mmoja na kuondoka naye na mpaka sasa hawajamrudisha na habari tulizo nazo amepelekwa kituo Kikuu cha Polisi Iringa mijini kilomita 60 toka eneo la Tukio. Hao watoto hawajanyonya maziwa ya mama yao tangu Usiku wa saa tisa kuamkia leo.

Polisi wako eneo la tukio!!
 
Enough is enough! Tumechoka na habari za askari kujichukulia sheria mikononi! Unyanyasaji na ukuikwaji mkubwa huu wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na haki ya kuishi! hawa wanastahili kukamatwa na kukabiliwa na mkono wa sheria.
 
Hahahaaaaaaa na badooo askari piga risasi hao mbwa nyoka wanaokwiba nyara za serkali hakuna kuremba
 
Saidi Mwena IGP aliwapa amri Polisi kuwa walipize kisasi. Hiyo ni aluta continual. Kifo cha Liberatus Kikwete alikiita cha kinyama na Uchunguzi ufanyike haraka. Naona aliye uwawa leo sio polisi kwahyo sitarajii uchunguz huru wowote.
 
Kila siku watu hufariki huko vijijini na hakuna mtu wa kuwapigania.
 
Askari hao baada ya Shaaban kutoroka walikwenda nyumbani kwake na kumchukua mke wake, Anna Mahogola mwenye watoto mapacha walio na umri wa mwaka mmoja na kuondoka naye na mpaka sasa hawajamrudisha na habari tulizo nazo amepelekwa kituo Kikuu cha Polisi Iringa mijini kilomita 60 toka eneo la Tukio.

Ni kinyume na sheria kwa mpelelezi au polisi wa aina yoyote yule anapokwenda kumkamata mtuhumiwa na kumkosa kumkamata mkewe kwa minajili kuwa kufanya hivyo kutasababisha mtuhimiwa kujitokeza.

Unless huyo mkewe naye anatuhumiwa, waliomkamata watakuwa wamefanya hivyo kinyume na sheria.
 
Mimi si mwanasheria ila sidhani kama ni haki tuhuma za mume kuhamishiwa kwa mke. Hata kama Huyo mama angekuwa mtuhumiwa ni kifungu kupi cha haki za binadamu kinaruhusu kumtenga mtoto wa mwaka mmoja na mama yake? Sidhani kama misingi ya haki za binadamu inazingatiwa.
 
Kazi kwenu wanasheria. Fuatilieni hiyo.
 
Katika kile kinachoonekana ni muendelezo wale tuliowakabidhi jukumu la kulinda ama watu au Rasirimali zetu kuua Raia wasio na Hati, Askari wa wanyama Pori wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha wamemuua kwa kumpiga Risasi mtu mmoja kwa tuhuma za kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria.

Askari hao wakiwa kwenye Land Rover mbili walivamia nyumbani kwa Iddy Kiruma kitongoji cha Mbigima, kijiji cha Isele kwenye Kata ya Mlenge, Jimbo la uchaguzi Isimani Wilaya ya Iringa, Mkoani Iringa, na kumpiga risasi ya mguu kiruma. Kwenye Nyumba hiyo pia alikuwemo Shaabani Chalamila ambaye kwenye purukushani hiyo alifanikiwa kutoroka. Kiruma amekufa akiwa mikononi mwa Askari hao haijulikani walikuwa anampeleka wapi kama ni Hospitali au Kambini kwao.

Askari hao baada ya Shaaban kutoroka walikwenda nyumbani kwake na kumchukua mke wake, Anna Mahogola mwenye watoto mapacha walio na umri wa mwaka mmoja na kuondoka naye na mpaka sasa hawajamrudisha na habari tulizo nazo amepelekwa kituo Kikuu cha Polisi Iringa mijini kilomita 60 toka eneo la Tukio. Hao watoto hawajanyonya maziwa ya mama yao tangu Usiku wa saa tisa kuamkia leo.

Polisi wako eneo la tukio!!

Si unajua hapa TZ Wanyama ni bora kiliko binadamu? Wametimiza kazi waliyoewa kwani wale wangine walio ua kule sijui selous walichukuliwa atua gani?
 
Kila siku watu hufariki huko vijijini na hakuna mtu wa kuwapigania.

Sulihisho ni dogo tu acheni uwindaji haramu; hata wewe Allen Kilewella inaonekana ni muindaji haramu na dnio sababu mnateteana.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hawa Askari waonevu na wasiokuwa na busara wote dawa yao ni kikundi cha Uhamsho tu.
 
Back
Top Bottom