Mbuki Feleshi
Senior Member
- Jan 24, 2011
- 155
- 29
Hasa ukizingatia kua shimo lenyewe limesha achwa na mgodi...dah.............mi inaniuma sana hii
Hii imetokea alfajiri ya leo ambapo askari wa mgodi wa dhahabu wa Geita aliyekuwa katika lindo
maeneo ya pit ya zaman iliyofungwa ya Lonkoni, aliwashambulia kwa risasi wananchi waliokuwa wameingia
maeneo ya mgodi bila ruhusa (maarufu kama watu wa "magwangara" yaani watu wanaoingia maeneo
ya mgodi ili kuokota mawe yasiyohitajika yaliyotupwa ambapo huyaprocess na kupata chochote).
Kwa mujibu wa maelezo ya masecurity hao wanadai watu hao walitumia nguvu kuingia kitendo kilichomfanya
askari huyo awafyatulie risasi na kumpiga tumboni kijana huyo ambaye alijeruhiwa vibaya sana na kupoteza
maisha yake papo hapo.
Inaskitisha sana, siku nzima ya leo hakuna huduma ya television geita baada
ya kukatwa kwa huduma ya cable ambayo ndo huduma pekee ya kuwawezesha
wananchi wa geita kupata habari hii inadaiwa ni njama ya kuzuia habari hii
isisambae na kupelekea kuamsha hasira zaananchi.
Waliozipata habari hizi pamoja na wadau wenzake na marehemu wamekasirishwa
sana na kuahidi kulipa kisasi, kiukweli hali ya amani huku sasa ni tete.
haya mauwaji ya watu kwenye migodi yataisha lini? hasa kwenye migodi ya dhahabu.
Kama sehemu hairusiwi wao kwa nini wanaenda huko? Hao watu unao waita magwangala huwa sio watu wema maana huwa wanaingia katika ngome za migodi wakiwa na siraha.kwa upande wa mwadui watu hao huitwa wabeshi.mfano kuna watu wengi sana walikufa kule kakola kwa kukaidi amri kutoka ndani ya mashimo walimo kuwa wamezamia mpaka.mwisho wa siku wazungu wakaagiza mtambo (bull dozer d9)ifukie mashimo na hatimae watu walifia ndani ya mashimo.pia kule runzewe mgodi wa tulawaka hao magwangala au wabeshi waliwahi kuvamia mgodi na kupiga bomu plant.kama haitoshi wengine kule kahama buzwagi baada ya kuzidi sana kuiba mafuta polisi waliongezwa mgodini hapo,kutokana na hari hiyo wabeshi walimvamia askari polisi wakamuuwa na kumnyang'anya bunduki na kutoweka nayo. Na mengine mengi tu hao wabeshi wamefanya
Acha uongo wewe buzwagi askari alisema na hao wezi wa mafuta wakampa hela nzuri tu wapige zutu then akajifanya mjanja ndo waka mu disipline ila hawakumuua huyo polisi bwana na silaha ilipatikana chini ya umahiri wa buzwagi mine security manager Mr.Mark Sydney.R.I.P Sydney kwa hiyo ajali ya gari iliyochukua roho yako huko majuu
hata kama wameingia bila ruhusa ndio waamue kuua???
Tanzania zaidi ya uijuavyo.
nani kawadanganya kuwa kuna mtu anaweza kuzuia habari? waambieni imeandikwa.... hakika, wakinyamaza hawa, hata mawe yatapiga keleleInaskitisha sana, siku nzima ya leo hakuna huduma ya television geita baada
ya kukatwa kwa huduma ya cable ambayo ndo huduma pekee ya kuwawezesha
wananchi wa geita kupata habari hii inadaiwa ni njama ya kuzuia habari hii
isisambae na kupelekea kuamsha hasira zaananchi.
Waliozipata habari hizi pamoja na wadau wenzake na marehemu wamekasirishwa
sana na kuahidi kulipa kisasi, kiukweli hali ya amani huku sasa ni tete.