Medical Dictionary
JF-Expert Member
- Mar 12, 2012
- 1,060
- 309
Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Kati kwa kushirikiana na Askari wa Misitu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, wamewakamata watu saba wanaodhaniwa kuwa majangili, wakiwamo askari watatu wa Magereza Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 55.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka mjini Kibaya wilayani Kiteto, Kamanda wa Kikosi hicho, Paschal Mrina alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Julai 23, mwaka huu majira ya saa 6 mchana wakiwa kwenye gari la Magereza aina ya Toyota Land-Cruiser lenye namba za usajili STK 4394 likiwa linasafirisha nyara hizo.
"Nakutaarifu ni kweli tumewakamata wakiwa na gari la magereza likiwa na Twiga wawili, Pundamilia wawili, Swalapalapala majike wawili na Mbuni wawili wenye thamani ya shilingi milioni 55,543,686.20. Huu ni ujangili wenye taswira ya kuhujumu uchumi kwani twiga na swala palapala majike hayaruhusiwi kuuawa," alisema.
Mrina aliwataja waliokamatwa kuwa ni Mrakibu wa Msaidizi wa Magereza, Kimaro Joseph Sauli, WDR Richard Barick Peter na Koplo Silvester Dionis Bukha.
Aliwataja watuhumiwa wengine ambao ni raia ni kuwa ni Abubakari Ngaula, Hamza Mdachi, Saidi Iddi na Hosseni Gola, Wakazi wa Kiteto ambao alisema walikutwa na bunduki aina ya SAR ya magereza na Rifle.
Alisema wakiwa katika operesheni ya kudhibiti vitendo vya ujangili waliwakuta watuhumiwa hao katika maeneo ya uwindaji na baada ya kulitilia shaka gari hilo, walilisimamisha na kuwakuta na nyara hizo.
Alisema wakati wakiwa katika harakati za kuwadhibiti dereva wa gari hilo ambaye hakufahamika jina lake alitoroka kusikojulikana.
Alisema katika upekuzi wao, waliwakuta watuhumiwa hao wakiwa na kibali kilichoombwa na Hassan Omari kilichowaruhusu kuua nyati mmoja na pundamilia wawili.
Alisema lakini walipofika kwenye eneo la uwindaji walikiuka sheria na kuua wanyama ambao hawakuwa wamewaombea kibali na pia hawaruhusiwi kuuwawa.
Mrina alisema kuwa watuhumiwa hao, wanatarajiwa kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Manyara kujibu mashtaka ya kuhujumu uchumi.
Alisema kikosi hicho kimeweka kambi katika hifadhi ya misitu hiyo yenye mkondo unaotoka hifadhi ya taifa ya Tarangire kuelekea Mikumi ili kudhibiti ujangili unaondelea kutikisa hifadhi hizo.
Akizungumzia kuhusu changamoto zinazowakabili katika operesheni hiyo, alisema kazi yao inakuwa ngumu pindi magari ya serikali yanapotumika kwenye uhalifu na kwamba ni vigumu kuyatilia shaka.
"Umeona mwandishi changamoto ni magari kama haya kubaini kuwa yanatumika ni vigumu lakini kumbe umdhaniaye siye kumbe ndiye, sasa askari kama hao ndiyo wangekuwa mstari wa mbele kudhibiti ujangili, lakini badala yake wamekuwa nstari wa mbele katika kuhujumu, lakini sisi hatutaangalia sura ama cheo mhalifu ni mahlifu tutamdhibiti," alisisitiza Kamanda huyo.
Alisema hifadhi zilizopo kwenye mkondo huo zimekuwa zikutumiwa na majangili wanaoingia kinyemela kuangamiza nyara hizo za serikali.
Alisema miezi miwili iliyopita, watu wawili walikutwa na maboga wakiwa katika harakati za kuwaua tembo kwa kutumia sumu inayowekwa ndani yake.
Mlolongo wa matukio ya ujangili ambayo umekuwa ukiwahusisha askari wa majeshi mbalimbali nchini umeendelea kutikisa.
Miongoni mwao ni Sajini wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Azizi Athuman Yusufu ambayo inadaiwa alikamatwa Januari 20, mkoani Arusha akiwa pembe mbili za ndovu na bunduki aina ya Riffle yenye namba 458.
Mwanajeshi huyo pia inadaiwa kuwa alikuwa akitumia gari ya mkufunzi wa kijeshi kutoka Zimbabwe anayefundisha nchini.
Mwisho.
ABIRIA ATELEKEZA MENO YA TEMBO
Nalo Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamsaka mkazi wa Tunduru Mjini kwa tuhuma za kutelekeza vipande vya meno ya tembo 21 na mkia vyenye thamani ya Sh. 30,316,000 kwenye basi la abiria la kampuni ya Wahida lililokuwa likitoka Tunduru kwenda Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Deusdeti Nsimeki alisema kuwa tukio hilo lilitokea Julai 21, mwaka huu majira ya saa 11:40 alfajiri katika kituo cha mabasi cha mjini Tunduru.
Nsimeki alisema kuwa polisi wakiwa doria kwenye eneo hilo, walifanya upekuzi kwenye basi hilo aina ya Scania lenye namba za usajili T 315 ABS na kukamata begi na sanduku.
Alisemba baada ya kufanya upekuzi walikuta kwenye nguo kukiwa na meno hayo yenye uzito wa kilo 34.45 na mkia huo.
Kamanda huyo alisema pia walikuta tiketi moja ya kusafiria iliyokuwa na namba ya simu na walipofuatilia zaidi kwenye kitabu cha tiketi ilikuwa imeandikwa jina moja ambalo limeifadhiwa kwa uchunguzi zaidi.
Nsimeki alisema inadhaniwa kuwa mtuhumiwa huyo alipogundua polisi wanaendelea kumfuatlia, aliamua kuteteleza mizigo yake hiyo.
SOURCE: NIPASHE|Imeandikwa na Cynthia Mwilolezi, Arusha na Gideon Mwakanosya, Songea.