Askari wa jiji mbaroni wakijifanya maofisa Uhamiaji

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,161
2,000
takukuru+pic.jpg

Mwanza.
Idara ya uhamiaji jijini Mwanza inawashikilia kwa mahojiano askari mgambo wawili wa jiji la Mwanza kwa tuhuma za kujifanya maofisa wa idara hiyo na kupita maeneo ya biashara ikiwemo mahoteli kukagua vibali vya ukaazi wa wageni.

Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Paul Eranga akitoa taarifa leo Ijumaa amesema mgambo hao walikamatwa walipofika kwenye moja ya hoteli za kitalii jijini Mwanza kwa lengo la kukagua wageni waliofikia hapo iwapo wana nyaraka na vibali halali vya kuingia nchini.

Amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni Chacha Kichele, mkazi wa Bugarika Wilaya ya Nyamagana na mwenzake Michael Julius, mkazi wa Kiloleli wilayani Ilemela.

“Walitumia mwanya wa sare zao kufanana na zile za idara ya Uhamiaji kupita kwenye mahoteli kukagua wageni wakijifanya ni maofisa Uhamiaji hadi uongozi wa hoteli moja ulipowashtukia na kutoa taarifa,” amesema Eranga

Mwananchi
 
life is Short

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
4,741
2,000
"Uchwara" ni virusi vya hatari husababisha magonjwa sugu !! na "feki" ni usanii uliyokithiri humu nchini.....
 
siz

Senior Member
Jan 26, 2015
132
195
View attachment 646414
Mwanza.
Idara ya uhamiaji jijini Mwanza inawashikilia kwa mahojiano askari mgambo wawili wa jiji la Mwanza kwa tuhuma za kujifanya maofisa wa idara hiyo na kupita maeneo ya biashara ikiwemo mahoteli kukagua vibali vya ukaazi wa wageni.

Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Paul Eranga akitoa taarifa leo Ijumaa amesema mgambo hao walikamatwa walipofika kwenye moja ya hoteli za kitalii jijini Mwanza kwa lengo la kukagua wageni waliofikia hapo iwapo wana nyaraka na vibali halali vya kuingia nchini.

Amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni Chacha Kichele, mkazi wa Bugarika Wilaya ya Nyamagana na mwenzake Michael Julius, mkazi wa Kiloleli wilayani Ilemela.

“Walitumia mwanya wa sare zao kufanana na zile za idara ya Uhamiaji kupita kwenye mahoteli kukagua wageni wakijifanya ni maofisa Uhamiaji hadi uongozi wa hoteli moja ulipowashtukia na kutoa taarifa,” amesema Eranga

Mwananchi
kuna mgambo wa jiji na askari polisi wa jiji hao wanaofanana na uhamiaji ni askari polisi wa jiji wapo majiji yote tanzania mtoa habari hujui kina cha habari umekurupuka
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom