Askari wa jeshi la majini la Uingereza ajiunga na Daesh

Askari wa jeshi la majini la Uingereza ajiunga na Daesh

Sinoni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
7,045
Reaction score
12,537
33F03BE400000578-0-image-a-17_1462654221082.jpg


Habari zinasema kuwa, Ali Alosaimi mwenye umri wa miaka 28 alipokea mafunzo ya hali ya juu ya ubaharia nchini Uingereza kwa miaka mitatu kabla ya kuondoka nchini na kwenda kujiunga na Daesh.

Gazeti la The Mail jana Jumapili lilichapisha habari za askari huyo wa baharini wa Uingereza mwenye asili ya Kuwait baada ya kupatikana nyaraka kumhusu katika shehena iliyokuwa na nyaraka za wanachama wa kundi hilo la kigaidi.

Admeri Lord West, mkuu wa zamani wa jeshi la majini la Uingereza amesema ana wasi wasi kuwa huenda kundi la Daesh linataka kuanzisha mbinu mpya ya hujuma zake. Amesema yumkini kundi hilo sasa linataka kuanzisha ugaidi wa baharini kwa kushambulia meli na feri, ndipo sasa limeanzisha kampeni za kuwashawishi askari wa baharini wa Uingereza wajiunge nalo.

Alosaimi anasemekana kupata mafunzo ya hali ya juu katika taaluma ya ubaharia na jeshi la majini katika Chuo cha South Tyneside eneo la Tyne nchini Uingereza kati ya mwaka 2011 na 2013.



UK navy officer joins ISIS: Defence experts warn of terror attacks on ships as highly skilled sailor turns from playboy into jihadi after watching videos of Assad's atrocities in Syria
  • Ali Alosaimi’s high-level skills and exhaustive knowledge of the nation’s shipping fleet represented a terrifying security threat after he fled to Syria
  • His personal details were found among a cache of IS documents
  • They reveal that before leaving for Syria, Alosaimi lived in South Shields
  • Source: Dailymail
 
Nasikia London imepata Mayor. Shida mnawatengeneza wenyewe kwa ujinga wenu halafu mnashindwa kuwa-control mnaishia kulialia mnapopigwa.
 
Uingereza muda si mrefu ataanza kujutia uamuzi wake wa kugeuka dampo la wageni na kuwapa haki sawa na waingereza wa asili. Naona vijamaa vinaitumia fursa kisawasawa na kurudisha utaalamu kwa waliowatuma, back to asili yao.
 
hatari sana huyo anaijua meli vizuri huko baharini usalama mdogo sana...
 
Nasikia London imepata Mayor. Shida mnawatengeneza wenyewe kwa ujinga wenu halafu mnashindwa kuwa-control mnaishia kulialia mnapopigwa.
Naipokea habari hii kwa makengeza, yaweza kuwa ni mbinu ya kuongeza mashambulizi kwa mataifa ya kiarabu, ngoja tusubiri
 
Back
Top Bottom