Jeshi la Israel limekiri kupoteza askari wake 15 katika masaa 24 yaliyopita.Idadi halisi ya waliokufa huenda ni zaidi ya wale 67 waliotangazwa na Hamas hapo jana.
Katika taarifa za leo vikosi vya Hamas vimesema mapambano makali ya ardhini yanaendelea katika viunga vya mji wa Gaza na kwamba wamefanikiwa kuviripua vifaru kadhaa vya jeshi hilo.
Kwa upande wa watu wa Gaza wameshukuru kwamba Mola wao hajawasahau.Wakasema wameona maajabu ya vifaru vya Israel kupigwa kirahisi na bunduki za RPG ikiwa ni miongoni mwa silaha nzito za Hamas ijapokuwa ni silaha duni kulinganisha na silaha walizonazo jeshi la IDF.
Kuna uwezekano iwapo taarifa za vifo vya askari wa Israel zitaendelea kuwekwa wazi askari waliobaki wa miguu wanaweza wakaanza kuasi na kukimbia vifaru vyao.Hiyo ni miongoni mwa sababu za Israel kupendelea kupambana na Hamas huku mawasiliano yakiwa yamekatika.
Katika hatua nyengine Marekani imesema kuanzia sasa itaanza kutumia aina mpya ya silaha za Laser ili kujilinda na makombora yanayoendelea kurushwa dhidi yao kutoka Yemen,Syria na Iraq.
Faida ya silaha hizo ni kuwa hazina gharama kulinganisha na makombora yaliyozoeleka.Hatua hii imekuja wakati aina nyingi ya silaha zinazomilikiwa na majeshi hayo zikiwa pia zinamilikiwa na majeshi mengine na wanamgambo wenye ugomvi nao.
Pamoja na hivyo wachambuzi wa silaha wanasema aina hizo mpya za silaha huwa zinafanya kazi wakati hali ya hewa ikiwa ni nzuri tu.Huwa hazina uwezo wa kuona makombora yanayokuja kukiwa na ukungu au hali nyengine mbaya za hewa.
Suali la kujiuliza ni mpaka lini nchi hizo zitaendelea kuishi kwa uhasama na ubabe huku kila kukicha silaha zinazovumbuliwa huwa zinaingia mikononi mwa maadui zao.
View attachment 2800319
Aina mpya ya silaha ya Lazer Marekani na Israel wanayokusudia kuitumia kujilinda dhidi ya makombora kutoka ardhini wanayorushiwa.