Askari wa barabarani waendelee na moyo huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari wa barabarani waendelee na moyo huu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Sep 11, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 11, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  ASKARI WAENDELEE HIVI

  Katika safari zangu katika mikoa mbali mbali ndani ya Tanzania kwa kipindi cha wiki 2 hivi nimeona mabadiliko sana haswa kwa askari wa usalama barabarani kwa kweli hatua hizi wanazozichukua ni za kupongezwa sana na wanatakiwa waendelee na mipango hii pamoja na kuiboresha kwa kutumia tekinologia za kisasa katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama wanavyokuwa katika vyombo hivi vya usafairi .

  Mfano nilitokea Arusha kwenda Dar siku chache zilizopita kufika moshi askari akakagua gari lile baada ya kusikia harufu Fulani hivi , ilibidi askari hao wachukue basi hilo mpaka kituo cha polisi makao makuu mkoa kwa ajili ya kufanyiwa majaribio zaidi huku kukiwa na abiria ndani .

  Askari mmoja alichukuwa basi hilo akaliendesha kwa kilimita kadhaa kwa kufunga breki za mara kwa mara na majaribio mengine kisha akatoa ripoti kwamba basi liko safi hakuna matatizo kama mwenzake alivyohisi kule standi .

  Kitendo ni kizuri na cha kupongezwa sana lakini bado nilishangaa kwanini anajaribu gari ya abiria huku kukiwa na abiria ndani ? je katika majaribio hayo akasababisha ajari nyingine itakuwaje ? nani atawajibika hapo ? halafu wakati linapelekwa pale askari hao hawakutoa taarifa kwa abiria hata abiria wenyewe hakukuuliza chochote .

  Mimi sio mtaalamu wa sheria za usalama barabarani sana ila kwa hili nimeingiwa na maswali kidogo ingawa zoezi zima ni zuri sana , inapaswa ifanyike hivyo hata kama basi lisipotiliwa shaka wafanye hivyo ghafla tu mara kwa mara naamini abiria watasafiri wakiwa salama zaidi .

  Kuna maeneo mengine kama kibaha maili moja , siku hizi kila asubuhi kuna askari pale ambaye anatoa matangazo kwa abiria wote na wasafiri wengine wawe makini na madereva wanaoendesha hivyo , wakiona hivyo basi waripoti kwa vyombo husika hili ni tangazo zuri lakini tatizo ni kwamba anavyomaliza matangazo hayo hatoi namba za simu za watu wa kuwasiliana nao unajua wengi hawana namba hizi za simu .

  Kingine ninachoona ni kwa magari yote mfano yanayoenda barabara ya arusha kuweka namba za vituo vya polisi vya barabara hiyo kama lolote likitokea kwenye basi basi abiria iwe rahisi kuwasiliana na askari hao , pamoja na wasimamizi wa mabasi hayo nimeona tiketi nyingi zina namba za uwongo za mabasi wasimamizi wa mabasi au ni za zamani wasimamizi walishaacha kazi .

  La mwisho ni vitendo vinavyofanywa na baadhi ya mabasi ambayo unakuta yamejazi abiria kuliko uwezo wake , wanapofika kwenye mizani basi wanashusha abiria wanaingia kwenye gari zingine zaidi ni hiace ili wakapime kisha wanarudishwa kwenye basi kuendelea na safari yao kama kawaida

  Vitendo hivi vinafanyika sana maeneo ya kibaha na njia panda , na askari hawa wanajua vitendo hivi lakini sijui mipango yao ni nini kuhusu kadhia hii , abiria nao wanatakiwa kupata elimu zaidi kuhusu haki zao pindi wanapokuwa ndani ya mabasi hayo .

  Nawapongeza askari wa barabarani kwa marekebisho wanayoyafanya kwa sasa naamini yataleta mabadiliko makubwa pamoja na kupunguza au kuzima kabisa matatizo mengi yanayotokana na uzembe wa mabasi haya .
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Vipi speed limit, hujayaona mabadiliko...from average speed of 120k/hr to 80km/hr?
   
 3. afkombo

  afkombo Member

  #3
  Sep 12, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 93
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Kwa kweli si hatua mbaya,mimi siwezi kuelezea kuhusu hayo mengine lkn kuhusu kujaribu gari likwia na abiria ki-physics ni sawa maana gari ikiwa na mzigo na ikiwa tupu kuna utofauti katika break,ila sijui huyo askari alijaribu hilo basi maeneo gani akiwa na abiria.
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nisahihishe tu, Tanzania hatujawahi kuwa na average speed ya 120km/hr, ni 80km/hr kwa sababu ya barabara.
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ni sahihi kujaribu braking system gari ikiwa na mzigo.
   
Loading...