Askari wa Al-shabab ajisalimisha kwa Serikali

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
91815888ad6b2b02e890b5d720af8d99

Mogadishu, SOMALIA
Kutoka pembe ya Afrika Idara ya Taifa ya Ujasusi ya Somalia (NISA) imesema kinara wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab, Aden Abdi, anayejulikana pia kama Aden Obe, ameliasi kundi la al-Shabaab na kujiunga na upande wa serikali.

Kwa mujibu wa NISA kinara hiyo amekuwa akiwasiliana kwa muda mrefu na NISA akitaka kujisalimisha. Afisa mwandamizi wa jeshi la serikali Ali Yakub Nur, amewaambia wanahabari kuwa NISA iliwasiliana na jeshi kutaka lishirikiane na Abdi ili ajisalimishe.

Pia amesema aliiambia NISA kuwa alikuwa na ugomvi na kundi la al-Shabaab, na alikuwa tayari kujiunga na jeshi la serikali. Pia ameongeza kuwa alijisalimisha akiwa na mlinzi wake maalum, na wote sasa wako mikononi mwa majeshi ya serikali.

Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakishirikiana na askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika maarufu kama AMISOM wameimarisha vita dhidi ya magaidi wa al-Shabab katika maeneo ya kati na kusini mwa Somalia ambapo wamefanikiwa katika kuwaangamiza magaidi wengi.

Darmpya
 
anayejua Ku tag naomba amtag Bibie Faizafoxy

maoni yake ni muhimu kwa ustawi wa dini yetu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom