Habari zilizotufikia hivi punde tu zinasema kwamba askari 3 wamefariki dunia huku wengine 3 wawili wakiwa majeruhi na hali zao ni mbaya baada ya kupata ajali mbaya iliyosababishwa na tairi la gari yao iliyokuwa katika msafara wa viongozi wa CCM mkoani Singida kupasuka na kupinduka katika eneo la Mkiwa, wilayani Ikungi.
Mwenyezi Mungu apokee roho zao hao MAREHEMU na awape nafuu ya haraka MAJERUHI.
Na mwanga wa milele uwaangazie!Wapate pumziko LA milele
Sio utani,maana mwendo wanao mpitisha nao kiongozi anaye itwa wa ngazi ya juu ni wa hatari zaidi ya hicho wanacho kiogopa wakipita kwa mwendo wa wastani na mara zote wana usalama ndio wahanga,Mungu apishie, mbali yaliyo tokea kwa Marehemu Sokoine yasije yakajirudia,Askari ndio wanao tukumbusha raia kuwa mwendo kasi unaua ila wao na hasa kwenye misafara huo msemo hauwahusu,Mungu azilaze pema roho za Marehemu na kuwapa wafiwa nyoyo za uvumilivu......
.....Mwendo kasi unauwa endesha kwa MAKINI !!!!!