Nyoka_mzee
JF-Expert Member
- Nov 26, 2016
- 3,695
- 5,522
Hawa police wa usalama barabarani bado ni kero kwa wenye magari. Wamekuwa si watu wa haki badala yale ni watu wa dhuluma na uonevu. Maana imekuwa sasa hivi ni mwendo wa cheti tu.
Gari ikiwa na mchubuko kidogo tu wa rangi basi jiandae 30,000, imetokea taa za brake zimekufa 30,000. Sasa mimi niko mbele ntaonaje? Na hata mkisema kwamba inanipasa kukagua, basi chukulia asubuhi nimefanya ukaguzi ikaungua njiani wakati natoka, napo hamlifikirii?
Imekuwa kero kwa hawa watu kupindukia. Zamani gari ikiwa ina vibali una uhakika wa kutembea kwa raha. Ila sasa hivi hata gari iwe na vibarl bado utasumbuliwa na kucheleweshwa unapokwenda. Na tena sio sehemu moja , unaweza jikuta umesimamishwa zaidi ya mara kumi.
Jambo hili limenifanya nimkumbuke sana mzee wangu Kikwete, maana usumbufu huu uliopitiliza ulikuwa hamna. Nimeshuhudia askari analifata gari na kuliandikia bila hata ya kosa au kumweleza mtu alichokosea tena mtaaani.
Wito kwenu nyinyi Askari, mkumbuke dhuluma na uonevu si jambo zuri na hamuwezi kufanikiwa kwa kuchukua hela ya mtu kwa uonevu. Kaeni mkijua watu wanasononeka kwenye nafsi zao na mtapata laana. Maisha hayaishii hapo ukijiona wewe mfalme barabarani basi kuna mwingine ni mfalme mahali fulani.