Askari Polisi wa Usalama Barabarani hamuwezi kufanikiwa kwa kuwadhulumu wananchi

haaha mkuu sikutaka kucheka kwa machungu niliokuwa nayo ,Dah ila mkuu anakosea sana kuwafanya hawa jamaa chanzo cha mapato,na ndo inanifanya nichukie utawala huu

Amwambie Mpango aziweke hizo faini kwenye mafuta kama za leseni atupunguzie usumbufu
 
Amwambie Mpango aziweke hizo faini kwenye mafuta kama za leseni atupunguzie usumbufu
Yaan nahisi itakuwa bora ,maana huwa wanapoteza muda ni washenzi sana yaan kuna wakati naona bora uwe mtu wa daladala maana huna amani aisee
 
wameagizwa kukamilisha kiwango fulani cha mapato, iweje traffic offenses ziwe chanzo cha mapato ya serikali? wameshindwa kuchukua mapato ya gesi, makaa ya mawe, mlima Kili, bahari, maziwa hadi waje kwenye pesa za raia? saivi utu haupo tena kama traffic wa zamani ukifanya kosa dogo anakupa warning, na walikuwa sio wengi namna hii kila mahali unasimamishwa tunatembea kama tuko congo kwenye vita..
 
Mkuu, wewe nenda kalipe tu, vinginevyo yatakukuta yale ya road license ya TRA, hizo faini za vyeti zinaonfezeka kwa 25% kila baada ya wiki.

Ukilimbikiza sana urajikuta zimefikia thamani ya gari lako.

Vv
Mkuu nikipata pesa ntalipa wala sijakaataa ila inauma sana mzee mungu ndo anajua ila hawa watu mungu yupo, ipo siku watavuna walichopanda
 
Mkuu nikipata pesa ntalipa wala sijakaataa ila inauma sana mzee mungu ndo anajua ila hawa watu mungu yupo, ipo siku watavuna walichopanda
Usisubiri upate hela ya kulipia vyeti vyote, lipia kimoja baada ya kingine ukianzia kile cha kwanza ili kupunguza riba.

Vv
 
Kuna trafiki amefanikiwa kujenga mjengo si dhani kama hajatumia dhuluma maana kila siku anatega na huchomoki hata kama umekamilika lazima apate cha kusema!
 
wameagizwa kukamilisha kiwango fulani cha mapato, iweje traffic offenses ziwe chanzo cha mapato ya serikali? wameshindwa kuchukua mapato ya gesi, makaa ya mawe, mlima Kili, bahari, maziwa hadi waje kwenye pesa za raia? saivi utu haupo tena kama traffic wa zamani ukifanya kosa dogo anakupa warning, na walikuwa sio wengi namna hii kila mahali unasimamishwa tunatembea kama tuko congo kwenye vita..
Babu acha tu Yaan huyu ngosha kaja katuvuruga kila kitu ,Yaan Askar wamekuwa wengi kuliko magari na baada vituo viwili askar na unasimamishwa,ukipita ni kwa kudra za mungu
 
babu afadhali wangekuwa wanachukuwa buku mbili ,saivi wanataka cha teni aisee yaan buku mbili tano hapokei yaani wangekuwa wanakula cha mbili wala nisingepiga kelele
Una muda gani umeanza kuendesha gari hapa Tz?
 
Usisubiri upate hela ya kulipia vyeti vyote, lipia kimoja baada ya kingine ukianzia kile cha kwanza ili kupunguza riba.

Vv
Haina shida mkuu Tatizo mambo yamekaa vibaya majukumu yamepandiana kwa kweli hujui ufanye lipi uwache lipi ,maana huwezi ukaacha watoto wanarudishwa ada ukalipie chetii acha iyongezeke tu
 
Kuna trafiki amefanikiwa kujenga mjengo si dhani kama hajatumia dhuluma maana kila siku anatega na huchomoki hata kama umekamilika lazima apate cha kusema!
Ndo hawa unakuja kuskia nyumba imeunguwa moto ,pumbavu zao kabisa ,watu tunavuja jasho kutafuta pesa wao wanataka kula kiulaani
 
Mbona tumefanikiwa sana tu... sema pepo ndio Shida kuipata dah! Nikiwaza huwa naumia moyo tu.. ila hakuna la kufanya.. maana sometimes mtu analia hana pesa ya fine na ana mwekundu mmoja ni ngumu. Mshahara wenyewe huu.. piheni kelele kwa wabunge wenu tuongezewe mshahara hapo ni rushwa na makosa mengine yatakuwa ni onyo tu ila tunakunote next time ni cheti tu
 
Mbona tumefanikiwa sana tu... sema pepo ndio Shida kuipata dah! Nikiwaza huwa naumia moyo tu.. ila hakuna la kufanya.. maana sometimes mtu analia hana pesa ya fine na ana mwekundu mmoja ni ngumu.
Kuna jamaa yangu alikuwa ana gari za Abiria ,imebidi tu azihamishe mji,maana kila siku cheti 90
 
Back
Top Bottom