Askari Polisi auawa kinyama na kutupwa mtaroni

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
ASKARI wa jeshi la polisi Mkoa wa Kilimanjaro katika kituo kidogo cha Kia wilayani Hai, Sajent Juma Ango ameuawa kinyama na watu wasiojulikana na mwili wake kutupwa mtaroni karibu na kituo cha polisi Bomang'ombe.

Mwili wa Askari huyo aliyekuwa kitengo cha upelelezi kituo cha polisi Kia ulikutwa ukiwa na majeraha kadhaa katika sehemu za kichwani na usoni kando ya mgahawa wa Chakula uliopo eneo hilo .

Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Hai ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wikayani humo ,Lengai Ole Sabaya alisema kuwa mwili wa askari huyo ulikutwa mnamo jana Aprili 13 mwaka huu majira ya saa mbili asubuhi baada ya vijana waliokuwa wanafyeka pembezoni mwa barabara kuu ya Arusha Moshi kuuona mwili huo.

"Ni kweli nimepokea taarifa za askari wa kituo kidogo cha polisi Kia kuuawa na mwili wake kukutwa mtaroni kando ya barabara kuu ya Moshi Arusha maeneo ya Mgahawa wa Chakula karibu na ofisi za dalali wa viwanja ya Kambele mijini Bomang'ombe"alisema

"Taarifa nilizozipata ni kuwa marehemu siku ya jumapili ya pasaka alikuwa katika baa ya Msami mpaka majira ya saa nane usiku akiwa anakunywa pombe"alisema Sabaya

Kamanda wa polisi mkoani hapa,Salumu Hamduni alisema kuwa tukio hilo lipo na upelelezi wa tukio hilo haujakamilika na pindi utakapokamilika taarifa kamili zinatolewa .

Kamanda aliongeza kuwa kwa sasa jeshi hilo lipo katika hatua ya uchunguzi ili kubaini wahusika wa tukio hilo na kwamba mwili huo umehifadhiwa katika hospital kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Ends...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ASKARI wa jeshi la polisi Mkoa wa Kilimanjaro katika kituo kidogo cha Kia wilayani Hai, Sajent Juma Ango ameuawa kinyama na watu wasiojulikana na mwili wake kutupwa mtaroni karibu na kituo cha polisi Bomang'ombe .

Mwili wa Askari huyo aliyekuwa kitengo cha upelelezi kituo cha polisi Kia ulikutwa ukiwa na majeraha kadhaa katika sehemu za kichwani na usoni kando ya mgahawa wa Chakula uliopo eneo hilo .

Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Hai ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wikayani humo ,Lengai Ole Sabaya alisema kuwa mwili wa askari huyo ulikutwa mnamo jana Aprili 13 mwaka huu majira ya saa mbili asubuhi baada ya vijana waliokuwa wanafyeka pembezoni mwa barabara kuu ya Arusha Moshi kuuona mwili huo.

"Ni kweli nimepokea taarifa za askari wa kituo kidogo cha polisi Kia kuuawa na mwili wake kukutwa mtaroni kando ya barabara kuu ya Moshi Arusha maeneo ya Mgahawa wa Chakula karibu na ofisi za dalali wa viwanja ya Kambele mijini Bomang'ombe"alisema

"Taarifa nilizozipata ni kuwa marehemu siku ya jumapili ya pasaka alikuwa katika baa ya Msami mpaka majira ya saa nane usiku akiwa anakunywa pombe"alisema Sabaya

Kamanda wa polisi mkoani hapa,Salumu Hamduni alisema kuwa tukio hilo lipo na upelelezi wa tukio hilo haujakamilika na pindi utakapokamilika taarifa kamili zinatolewa .

Kamanda aliongeza kuwa kwa sasa jeshi hilo lipo katika hatua ya uchunguzi ili kubaini wahusika wa tukio hilo na kwamba mwili huo umehifadhiwa katika hospital kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Ends......

Sent using Jamii Forums mobile app
hii taarifa tiyari ipo hapa JF
 
Wanaume tunazidi kuisha kwa tukio hilo la mwanaume mmoja kuuwawa kinyama tugemee wanaume wengine zaid ya watano kutia kwa mbaloni kwa kile kinaitwa uchunguzi then kwa kile kinaitwa upepelezi bado unaendelea zaid ya miaka hata kumi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Mkusanyiko huu.
Tanzania wajinga ni wengi sana
FB_IMG_1586800487771.jpg
FB_IMG_1586800483681.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom