Mwanapropaganda
JF-Expert Member
- Aug 19, 2014
- 4,235
- 2,512
Tabora. Polisi aliyefahamika kwa jina la
Charles mwenye namba H 3416 wa Kituo cha
Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, amejiua
kwa kujipiga risasi akiwa ndani ya kituo.
Kwa mujibu wa taarifa, Charles alikuwa
kazini na alijiua Jumamosi usiku na sababu za
kujiua kwake hazijafahamika.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya
wananchi walio jirani na kituo hicho,
walisema tukio hilo lilitokea saa moja jioni.
Nilikuwa nyumbani ghafla nikasikia mlio wa
risasi katika kituo cha polisi na nilipokwenda
nilimkuta askari Charles amekufa kwa
kujipiga risasi, alisema Furahisha Felix.
Wananchi hao walisema kutokana na hali
hiyo walilazimika kuwauliza baadhi ya askari
waliokuwa naye zamu, ambao nao walidai
hawajui sababu za mwenzao kuchukua
uamuzi huo.
Haiwezekani polisi ajiue na isijulikane
sababu, hilo halipo, lazima kuna jambo
limejificha,alidai mkazi mwingine Amani
Ibrahim.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Tabora, Suzana
Kaganda alisema: Ni kweli askari huyo
amejiua wakati akiwa kituoni saa moja usiku,
tunaendelea na uchunguzi kujua sababu za
kifo chake,alisema Kaganda.
Kamanda Kaganda alisema askari huyo
hakuacha ujumbe wowote kueleza sababu za
kujiua.
Kutokana na tukio hilo, alitoa wito kwa askari
wote kwamba wanapokuwa na matatizo
wayawasilishe kwa viongozi wao badala ya
kujichukulia sheria mkononi.
Matukio ya polisi kujiua
Hili ni tukio la pili la askari kujiua ndani ya
kituo kwa mwaka huu, huko wilayani Mbozi
mkoani Mbeya, polisi mwenye cheo cha
Sajenti, D 4179 Partick Gondwa (54), alijiua
kwa kujipiga risasi akiwa ndani ya kituo.
Askari huyo ambaye, pia alikuwa ni mtunza
vielelezo kwenye kituo hicho cha Polisi
Wilaya ya Mbozi, inasemekana alijipiga risasi
kwa kutumia bastola ambayo nayo ni kielezo
kilichokuwamo ndani ya chumba hicho.
CHANZO: Gazeti la mwananchi.