"Askari mmoja alirarua gauni langu, nikabaki uchi mbele ya baba”

"Askari mmoja alirarua gauni langu, nikabaki uchi mbele ya baba”

lukanima

Member
Joined
Apr 6, 2013
Posts
52
Reaction score
34
Simulizi kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi (24 Juni 2013):

Ilikuwa Juni 18, mwaka huu katika Uwanja wa Soweto wanachama na wapenzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walikukusanyika ili kuwaaga watu wanne waliokufa kufuatia bomu lililolipuka Juni 15, katika uwanja huo.


Tangu bomu hilo lilipolipuka siku hiyo (Jumamosi), viongozi wa Chadema akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe walifanya mikutano uwanjani hapo Juni 17 na 18, Japo tayari polisi walishazungusha utepe katika eneo lililolipukia bomu.

Siku hiyo, saa 9 alasiri wakati mkutano ukiendelea na viongozi wa chama hicho wakitoa maelekezo ya jinsi ya kuaga maiti, polisi waliokuwa wamefurika eneo hilo waliwashambulia kwa mabomu ya kutoa machozi ili kuwatawanya.

Malisa anayeishi Kata ya Ngarenaro jijini humo alifika uwanjani hapo kumwokoa baba yake Godwin Malisa ambaye ni mlemavu, alijikuta akipata kipigo cha mbwa mwizi.

“Nilikuwa namfuata baba yangu ambaye ni kada wa Chadema. Kutokana na ulemavu wake nilihofu angepata matatizo kama vurugu zingezuka,” anasema Wema na kuongeza:

“Nilikuta uwanja ukiwa umefurika wananchi wakiwasikiliza viongozi wa Chadema. Viongozi hao ni Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye alihutubia na kumwachia Tundu Lissu (Mbunge wa Singida Mashariki) naye akamwachia Said Arfi (Mbunge Mpanda Kati). Alipomaliza kuwataka wanachama hao waelekee Hospitali ya Mount Meru, ndipo mabomu yakaanza kulipuliwa.”

Anaendelea kusema: “Nilimwambia baba tuondoke lakini tulikuwa tumeshachelewa, kwani polisi walikuwa wametuzingira. bomu la pili liliangukia mbele yetu. Askari mmoja akasema ‘laleni chini’, tukalala tukidhani tutakuwa salama. Lakini walikuja askari na kutupiga marungu mwili mzima mimi na baba,”

“Ghafla akatokea askari mwingine akawakataza wasitupige, tukadhani tumeokoka. Mara wakatokea askari wengine, hapo ndipo kilikuwa kipigo kitakatifu. Nilijaribu kuwazuia wasimpige baba kwa kuwa ni mlemavu, wakanikebehi kuwa huyo ni hawara yangu. Walinipiga mpaka mkono na mguu ya kushoto ikavunjika.

“Tulikuwa kwenye kibaraza cha nyumba wakati askari wanatupiga. Askari mmoja alirarua gauni langu chini na juu, hadi nikabaki uchi mbele ya baba. Mwingine akakoki bunduki na kuielekeza katikati ya mapaja yangu ili alipue sehemu za siri, wenzake wakamkataza. Mwingine alisema kuwa atanibaka. Baba alinikumbatia akasema watuue wote, mimi niliomba wasituue maana nimeacha mtoto mchanga nyumbani.”

Anasema askari walikuwa wakimbeza kwa kumuuliza kwa nini yeye ni mwanachama wa Chadema.

“Walisema ‘unajifanya wewe Chadema, sasa ndiyo utajua kuwa CCM inatawala. Chezea CCM wewe.’ Mimi niliwaambia sina chama chochote nimekuja kumwokoa baba yangu. Wakati huo wote walishanivua hereni, simu wakachukua na fedha zilizokuwa ndani ya pochi na kuitupa chini ikiwa tupu.”

Hata hivyo Wema anasema alikuja askari wa kike aliyekuwa akipiga picha za matukio na kuwasaidia. Wakati huo watu wote wameshatawanyika uwanjani hapo na askari wameshaanza kujipanga baada ya kuitwa kwa filimbi.

“Alitusikitikia na kusema, ‘kwa nini mnang’ang’ania kuwa Chadema? Angalieni sasa mlivyoumia na viongozi wenu wamewakimbia.’ Akaokota kanga iliyoachwa uwanjani na kuja kunifunika,” anasema na kuongeza:

“Kisha likaja gari la polisi tukabebwa na kuingizwa humo. Mwendo tuliondoka pale ulikuwa wa kasi huku wakiendelea kulipua mabomu na kutukanyaga bila kujali. Tulishtukia tuko Hospitali ya Mount Meru, tukabwagwa hapo na gari hilo likaondoka.”

Wema anasema walitibiwa kwa siku kadhaa kabla ya kuruhusiwa ili kuugulia nyumbani.

Maelezo ya baba yake

Baba yake Wema, Godwin Malisa japo hakupata majeraha makubwa, anaendelea kuugulia maumivu makali ya mwili mzima.

“Kilichonisikitisha ni kitendo cha kumpiga na kumdhalilisha mwanangu mbele yangu. Askari wengine walikuwa wakijaribu kuvunja hili gongo ninalotembelea kwa sababu ya ulemavu,” anasema Malisa na kuongeza:

Alalamikia kauli ya Pinda

“Nimesikitishwa na kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyoitoa hivi karibuni Bungeni Dodoma ya kuwataka askari waendelee kupiga wananchi. Kwa hali hii sisi wanyonge natuna pa kukimbilia.”

Akisimulia zaidi, Malisa anasema, siku hiyo licha ya watu kuwa wengi katika uwanja huo, Jeshi la Polisi halikufuata kanuni zake za kutoa ilani kwa wananchi kabla ya kuanza kushambulia.

Licha ya Jeshi la Polisi mkoani Arusha kusema hakukuwa na majeruhi siku hiyo, inaelezwa kuwa wengi walijeruhiwa kwa kupigwa na polisi.

​
My Take: Wakati haya yanatokea waziri mkuu alikuwa hajatoa hadharani tamko la kupiga. Tutarajie nini baada ya tamko lake?
 
kweli tunapo elekea karibuni tutafika. watu hawana hata chembe ya huruma. Mungu naomba uwajeuze wao waliompiga huyo dada pamoja na baba yake wawe mawe ya kusagia. wote tuseme ameni
 
Khaa!! Kwangu mimi tokea zamani hii naiita vita ya maslahi ndiyo maana naona nikazane na jembe langu:heh:
 
Akili zao ni ndogo tu hawa askari,maisha yao magumu wanategemea sana rushwa lakini tutawakomboa tu-waige mfano wa majeshi kama ya Misri waliamrishwa kupiga kwa kujali utu,democrasia wakapinga Amri na leo hii Mubaraka huyo... Tunaona anaburuzwa kortin

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
hivi askari waliopo arusha wengi wao huwa wanapelekwa askari wenye mani gani????? au huwa hawana mungu kabisaa???
 
Can any one of you take this story and post to Netherlands, Norway, German, Switzerland.... And AMnest International?

"Watanzania tuna Matatizo haya makuu 2 na Hawa watawala wanajua hilo na watatuonea saanaaaa.

A - Kukosa mshikamano na Coordination

B- Uoga

Maelezo:

Kukosa mshikamano na Coordination.

Kuna kauli inasema hivi:- Mtanzania mmoja akionewa ni watanzania wameonewa. Waarabu wametumia hii slogan na wamefanikiwa.....

Mfano, wakati Madaktari wanagoma kwa ajili ya kutetea Hospitali zetu zipate vifaa na dawa - tupo kimya, mpaka akaja kutekwa Ulimboka.....

Mfano: Kauliwa kijana Morogoro kijana na Iringa Mwangosi ---- Mikoa mingine iliyoamka kama Mbeya, Arusha, Manyara, Moshi, Mwanza, Bukoba,,,, tupo kimyaaaa...

Ikaja kutokea Mbeyaaa --- mpaka Sugu kaenda kusuluhisha

Ikaja Iringa -- Wamachinga....

Ikaja baba lao Mtwara, ..... Wananchi walipigwa mabomu ya kutosha, risasi za kutosha ... Mikoa mingine kimyaaaa

Sasa circle imerudi Arusha... Mikoa mingine kimyaaa.

Hatujui WHo next....... Hawa watawala wataendelea kutuuwaaa. Hatuna coordinatination.

Wananchi tuamke, tusitegemee USA wala UK, ---- maana wao wanataka rasilimali zetu na wanapewa Buree na watawala..

Uoga wetuuuuuu

Uoga

Uoga

What to do....

Wakiliamsha Mtwara... inapokelewa DAr, inasambaa Handeni, Moshi mpka Manyara Kupitia Arusha

Mbeya wanapokea na Mwanza..... Hawa watawala watashika adabu.

Tuamke Watanzania.... Vinginevyo...... sasa wataanza kuuwa Viongozi wa Ukombozi...."​


 
Hakika maumivu ya Watanzania na DAMU ya raia wasio na hatia hakika haitaenda bure jamani!

Ole wake yule aliyenyanyua mkono wake kwa raia wema kama Wanainchi walipata vilema vya kudumu bila sababu!

KAMA HUYU MUNGU TUNAYEMWAMINI NA KUMTEGEMEA ATAKUWA AMELALA HAKIKA TUTAJUA!

Wema maumivu yenu hayataenda bure!
 
Hata Mandela alifanyiwa hivi hivi na makaburu sisi tunafanyiwa na mkoloni mweusi.
 
Hakika maumivu ya Watanzania na DAMU ya raia wasio na hatia hakika haitaenda bure jamani!

Ole wake yule aliyenyanyua mkono wake kwa raia wema kama Wanainchi walipata vilema vya kudumu bila sababu!

KAMA HUYU MUNGU TUNAYEMWAMINI NA KUMTEGEMEA ATAKUWA AMELALA HAKIKA TUTAJUA!

Wema maumivu yenu hayataenda bure!
 
Kwani Polisi hawafahamu kuwa Mtanzania yoyote kwa wakati wowote anaweza kuamua kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa?Au kwa sababu walikuwa wametumwa na mabosi kufanya unyama huo?
 
Duh...uh..........hawa jamaa ..Khaah...ka...ndio maana Aksri wanagongwa na magari arusha, watepewa na sumu sasa..
 
Back
Top Bottom