Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 757
- 1,822
Jeshi LA Polisi Mkoani Arusha linawashikikia askari nane wa kampuni ya ulinzi ya Knight support tawi LA Arusha kwa madai ya kufanya mgomo na kumfungia nje meneja wa tawi hilo,Malima Macha kushinikiza aondolewa kutokana na tabia yake ya kuwadharau na manyanyaso na kushindwa kusimamia maslahi yao.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoani Hapa Jonathan Shanna amesema kuwa askari hao walitenda kosa hilo juzi na kusababisha hali ya amani kuvunjia na shughuli za kiofisi kusimama.
Alisema kimsingi hatua waliofikia haikubaliki hata kama madai yao ni ya msingi kwani askari hapaswi kugoma ama kuandamana na pindi anapogoma tuaamini ni hatua ya uasi na lazima hatua za msingi zichukuliwa.
Alifafanua kuwa wafanyakazi hao wamekuwa na msuguamo wa muda mrefu na mwajiri wao ambaye ndiye meneja wa kampuni hiyo Mkoani Arusha na hoja yao kubwa ni kwamba hawamtaki wakidai anawasharau ,kuwatusi na kushindwa kuwapa mshahara kwa wakati.
Baadhi ya askari hao ambao waliomba majina yao kutowekwa hewani kwa hofu ya kufukuzwa Kazi, wamemtuhumu meneja wao,Malima kwa kushindwa kuwalipa mishahara yao huku pindi wanapokuwa wakiulizia amekuwa akiwatolea lugha chafu zenye utusi na kushindwa kuwasikiliza.
"Kwakweli huyu meneja hatumtaki hapa kwanza amewagawa wafanyakazi ameshindwa kutataua kero za wafanyakazi ,amekuwa akiwatukana na kutoa lugha chafu pindi askaribwanapoulizia malipo yao" Alisema askari ambaye aliomba kuhifadhi jina lake
Kwa upande wake Malima macha alipohojiwa juu ya madai hayo aligoma kuzungumzia suala hilo akidai si msemeji wa kampuni hiyo na alipotakiwa kutoa mawasiliano ya msemeji wa kampuni hiyo aligoma akidai haruhusiwi kutoa Namba za mwajiri wake.