Askari jwtz vs raia

andry surlbaran

Senior Member
Apr 13, 2011
166
20
jumamosi nilitoka kwenye harusi nikapitia bar mpoja maarufu tu kawe yaitwa hipro pub wakati naingia nikapita kaunta ili kwenda msalani, nikakutana na askari mmoja tuna fahamiana wakati tunasalimiana na habari za hapa na pale (within 3 minutes) toka niingie eneo lile, ghafla nilikatwa mtama nakuangukia ma crate yaliokua pembeni na kuchanika sehemu kadha za usoni na damu ikanitapakaa mwili mzima, yule kijana namfaham ni askari , kumbe wakati nafika pale ati walikua wana quarrel a baadhi ya raia, nikainuliwa na wenzangu wakanipeleka police na kuchukua pf3, wakati nipo police wale police wa kituo cha kawe wakanilazimisha niwape chochote( wakati huo na bleed vibaya sana) nikagoma akaizuia ile pf3 mbaka nimpe kitu nikaingiza mfukoni nikatoa sh.450/= akaipokea na kunitukana, sikujali sana nikachukua bajaj kuelekea mwananyamala hospt nikapokelewa vizuri na kutibiwa nika shonwa nyuzi 4 na kuruhusiwa,.
Katika purukushani hizo nimepoteza miwani, simu, elf.47


swali

nina key evidence zoote nanimepanga kumshitaki na kijana niliekua namsalimia amenitajia jina na namba ya kikosi anachofanyia yule askari alienijeruhi. Sasa!! Je nimshitaki kwenye mahakama za ki raia au niende makao makuu ya jeshi kumshtaki( maana nimeskia wana mahakama zao)
naomba msaada!
 
andry,

Pole sana kwa udhalilishaji na uonevu uliofanyiwa na askari huyo,ushauri kwako ni huu:Peleka mashtaka yako kwenye Mahakama za Kiraia kwani uzoefu unaonyesha ya kuwa, mara zote inapotikea conflict kati ya askari na raia wakuu wa vikosi husika huwakingia kifua askari wao na raia kuonekana ndo wenye makosa.

Tunza hizo key evidence ulizonazo na mshitaki askari huyo ili kukomesha uhuni aloufanya.
 
Pole ndugu kwa masahibu ya hawa askari na sheria mkononi yao,wanajiona wao ndio wao.Kuna jamaa yangu alinipigia simu akanieleza pia kuwa alipigwa na askari wa JWTZ eneo la shule ya sekondari Y.Makamba wakati akipita kwenye barabara hiyo inayokaza tokea External mpaka mita yaTabata,anasema walimshambulia kwa sababu alipita kwa kasi ktk eneo la shule, mi nashindwa kabisa kuwaelewa hawa jamaa,na wakuu wao wanawalinda ukienda kulalamika.
 
na tatizo la mahakama zetu hizi basi hukumu itakuja 2017 yani nashindwa kuelewa!! hata muda huu naandika naumia kweli sehemu za kichwani
 
Kwa utaratibu ukipigwa na askari wa TPDF unapaswa kulipoti kwa RSM wa kikosi chake yeye humtaarifu OC wa kombania yake ili kama kuna vielelzo vya kutosha apelekwe court martial, ukienda kutoa taarifa kwenye mahakama za kiraia kukamatwa kwao na kufunguliwa mashitaka ni mpaka mkuu wake wa kikosi aridhie.
 
Ole wake Askari aniguse eti kisa sheria inamlinda..
Haki ya mama naapa nitamuua, kama siyo kwa mikono basi nitatafuta hata Bastola nimlipulie mbali...

Kha, pole Bandugu..
 
Pole sana ndugu yangu, nakushauri uende kikosini kwake ukatoe taarifa na nia yako ya kutaka kwenda mahakama ya kiraia
 
yani ningekuwa na ubabe kama wao ingekuwa safi sana, maana hawa watu wanaweza kudhalilisha kama mtoto mdogo.
 
kwa utaratibu ukipigwa na askari wa tpdf unapaswa kulipoti kwa rsm wa kikosi chake yeye humtaarifu oc wa kombania yake ili kama kuna vielelzo vya kutosha apelekwe court martial, ukienda kutoa taarifa kwenye mahakama za kiraia kukamatwa kwao na kufunguliwa mashitaka ni mpaka mkuu wake wa kikosi aridhie.

asante, nashkuru sana maaana rsm ni uncle wangu hapa umenikumbusha, asante sanaaaa
 
Back
Top Bottom