Askari asababisha ajali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari asababisha ajali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkaa Mweupe, Jan 25, 2010.

 1. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Katika hali isiyokuwa ya kawaida, asubuhi hii askari polisi al maarufu kama tiGo alisababisha ajali iliyopelekea kujeruhi watu wawili wapanda pikipiki.

  Kisa hiki kilitokea maeneo ya Ubungo usoni mwa jengo maarufu la Ubungo Plaza. Askari huyo ambaye alikuwa peke yake akiendesha pikipiki, alilipita Canter lililosheheni magunia ya mkaa na kuliamuru lisimame. Dereva wa canter alisimama bila kuzingatia kuwa ilikuwa ni asubuhi na kila mtu yuko kwenye jitihada za kuwahi kibaruani.

  Canter iliposimama ghafla kulikuwa na pikipiki kadhaa zikilifuata kwa nyuma pamoja na magari. Lahaula dereva mmoja wa pikipiki alikamata breki za ghafla zilizopelekea yeye na abiria wake kuanguka barabarani.

  Cha kushangaza pamoja na tafrani hii, askari aliyesababisha madhara yote haya hakuonyesha kushtushwa na jambo lililotokea. Alikuwa anaendelea kubishana na dereva wa canter katika kutafuta kinachohisiwa ni rushwa kutoka kwa dereva huyo.

  Jamaa wa pikipiki waliiokota pikipiki yao na walifanikiwa kuiwasha na kuendelea na safari yao.
   
 2. I

  Isae Member

  #2
  Jan 25, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Nafikiri hawa askari wetu wawe waanagilifu kwani Leo hii katikaeneo la Red cross barabara ya Ali Hassan Mwinyi imetokea incident kama hiyo. Unajua asubuhi hamna tarffic jam hivyo magari yanakwenda speed sasa traffic akasimamisha daladala ghafla na nyuma kulikuwa na daladala nyingine na dreva alikuwa anaaangalia green light hakujua tfrffic kasimamisha gari hivyo akamgonga mwenzake na kioo cha mbele kikapasuka na baadhi ya watu kuumia
   
Loading...